Millennials ndio Kizazi kilichofeli zaidi katika malezi ya watoto

Kizazi cha Mwalimu/Ujamaa-Waliozaliwa Nyerere akiwa rais.
Kizazi cha ruksa/soko huria; 1985-1995
Kizazi cha ubinafsishaji; 1995-2005
Maisha Bora; 2005-2015
Kizazi cha miondombinu na wasiojulikana; 2015-2025
Kizazi cha October 29/Uchawa: 2025-
 
Sijui kuhusu exact etymological chain, ila ulivyoelezea ina make sense.

Kwa sababu katika Kiswahili Barubaru ni kijana mdogo mwenye nguvu, aghalabu kijana aliyepata balehe karibuni, anayeweza kutumia nguvu zaidi kuliko akili pengine. Kwa hivyo kuna namna ya kuendana na ulivyosema. Ila ni kijana, wa kiume, ambaye ndiyo kwanza kapata balehe, mwenye nguvu, mwenye kuweza kutumia nguvu zaidi ya akili, kwenye lahaja nyingine neno linahusiana na Varuvaru. Rough. Barbarian.
 
Gen Z bongo ana soma na kibatari πŸ˜†
Style yetu naona iwe
-Watoto walio zaliwa kipindi cha Kikwete
-Watoto walio zaliwa kipindi cha jiwe
-Watoto walio zaliwa kipindi cha kazi na utu kipindi cha elninyo ya jua na joto kali etc
Sisi Bishoo Nyangema anajiita 2Pac πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Watoto wengi waliozaliwa 200-2015 ni zao la silent generation na few millenials. Usitulaumu kwa makosa ya wengine. Watoto wetu wengi wanaanzia 2015 kuja mbele.
 
Ukiyakuta sasa yana kejeli/Laumu kizazi cha 2000 lazina ushangae.

Like, Its your sons and doughter, N You failed to raise them as a parrent.
 
Kumekuchaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ukiyakuta sasa yana kejeli/Laumu kizazi cha 2000 lazina ushangae.

Like, Its your sons and doughter, N You failed to raise them as a parrent.
Ndio Kizazi chenye kutumia matusi zaidi kuwakanya watoto . Hawaoni aibu kutukana mbele ya watoto wakati kizazi cha 55 -75 ni mwiko kutukana mbele ya watoto
 
Kizazi cha Mwalimu/Ujamaa-Waliozaliwa Nyerere akiwa rais.
Kizazi cha ruksa/soko huria; 1985-1995
Kizazi cha ubinafsishaji; 1995-2005
Maisha Bora; 2005-2015
Kizazi cha miondombinu na wasiojulikana; 2015-2025
Kizazi cha October 29/Uchawa: 2025-
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ umetisha sana, Lol
 
Kumekuchaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Sasa watu wamepigana vita zao, wakavipa vizazi vyao majina yao kutokana na vita zao.

Na sisi tunataka kudandia majina yao hapohapo kama tuna fit kwenye historia yao jamani?

Kwani sisi hatuna mambo yetu na vita zetu?

Hili jambo nalo tutasema ni gumu sana linahitaji wawekezaji wa nje na fedha za kigeni?
 
Una nini lakini? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mambo mengi tumeiga, mengi tunafanya kwa sababu tunaacha vya kwetu, hatujui vya kwetu au hatuna uwezo wa kuwa na vyetu.

Hili la majina naona ni dogo tu, kama lina athari basi ni kidogo tu.
 
Rafiki yangu dini zimeshindwa kabisa kutengeneza jamii yenye maadili mazuri, watoto wote wenye tabia za kishenzi wanatokea ukanda wa watu wanaojiita washika dini

Lakin ukienda jamii za kifugaji kama wasukuma watoto wa huko bado Wana maadili mazuri sana
 
Mambo mengi tumeiga, mengi tunafanya kwa sababu tunaacha vya kwetu, hatujui vya kwetu au hatuna uwezo wa kuwa na vyetu.

Hili la majina naona ni dogo tu, kama lina athari basi ni kidogo tu.
Kuna mambo unaweza kuyaona madogo, lakini kifalsafa, kisaikolojia, ni makubwa sana.

Yana establish dominance, deep kwenye mawazo kabisa mnajikataa kuwa katika dunia hii, nyie si watu kama Wamarekani.

Yani mmepewa uhuru fulani, lakini mmekuwa kama yule kuku ambaye ameshazoea kufungwa kamba kwa muda mrefu, hata kamba ikikatwa anabaki palepale kashazoea hali ya kufungwa kamba.

Leo mmewaweka juu kama mwenge.

Halafu kesho mnakaa nao mezani hao Wamarekani, mna negotiate mkataba.

Watawapiga tu.
 
Kwa mantiki hiyo, waafrika(watanzania) turudi mezani tuanze upya maana kama ni hiyo dominance na nguvu tulishawapa, walishaichukua, wanaitumia kwa namna ambayo hata tukimbie marathon wao wakiwa wamelala fofofo bado hatuwafikii.

Nini ambacho tunajivunia kama taifa, Nyerere alisema hata bei ya korosho wanapanga wao. Tunajivunia nini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…