Miloud Hamdi atemwa Ismaly, Yanga ndio nafasi pekee ya kumrudisha ndio hii

Sina uhakika sana kama Yanga Yanga walimwacha Miloud na wakaenda kumleta mwanafunzi Folz afanye field kwenye timu yetu, ila kama walifanya hivi walikosea
Bora kama walimtaka Folz wangemleta coach msaidizi kama mwaka apate uzoefu
Mkuu pamoja na video ya wakala wa Miloud bado umegoma kuamini kama viongozi wamezingua?
 
Gamondi ni master, Singida ya sasa hivi wapinzani wajiandae atafukuzisha mtu kazi
 
Nimeona mkuu
Hakika walizingua ila ni jambo la kawaida kwenye uongozi, wao waliamini umri wa Folz wakimpa kikosi Bora nae atakuwa na kiu ya kufanya vizuri, wakaja kukuta sifa yake kuu ni kununa
Kwasasa ni kupambana tu tufuzu hatua ya makundi, itakuwa aibu sana kama ikitokea Yanga pekee ndio imeshindwa kuingia makundi kwa Tanzania.
 
Hapa tunajadili wenye akili sio wewe kichwa panzi senene mkubwa.

Mashabiki wa yanga wengi tumejaa akili na uwezo mkubwa

Shida kwa wanasimba kama wewe si umeona unavyoongea mashudu tu hapa?
Akili zote sahivi mmempa hersi "mungumtu" wa yanga. Jamaa huwa hakosei. Huyu kocha mlipigia makofi na kumpamba kwa kila kitu kisa tu alikuwa endorsed na hersi
 
Kwasasa ni kupambana tu tufuzu hatua ya makundi, itakuwa aibu sana kama ikitokea Yanga pekee ndio imeshindwa kuingia makundi kwa Tanzania.
Hao wa Malawi mnawatoa hakuna timu pale first half game itakua inasoma 2-0
 
Tugange yajayo hamna haja ya kumrudisha huyo Miloud, Hersi aangalie kocha mpya mwengne kama ni CV ataipatia hapa hapa
Kwa upuuzi alioufanya wa kumtimua Miloud na kumleta Folz, hapana. Akae pembeni wengine wamsaidie kazi.
 
Yes, hii Miloud ilimuumiza sana. Aliitamka akasema alinyamaziwa kimya na viongozi wa Yanga.
 
Nasikia kumbe hata baadhi ya wachezaji ndani ya klabu walikuwa hawamkubali. Sasa sijui shida ilikuwa ni mbinu zake, au ni ile style yake ya kujifanya hacheki na mtu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…