Mimi baba wa watoto watatu ratiba yangu ya asubuhi na jioni

Sijaona sehemu/ratiba ya mazoezi ya viungo
 
Hii nimeipenda!! Nitaifanyia kazi, malezi ni mchakamchaka sana, usipojitahidi utakuza mabumunda.
 
Vipi akitoka job akapitia mishe zake za pembeni! Sio lazima awe na mcheps, anaweza kuwa na goli lake linamuingizia 10k anapitia huko kuangalia maendeleo ya hustles zake.
 
Unachepuka sa ngapi
 
Kwanini mkeo asiandae nguo zako na watoto usiku,angalau zako bas ikibidi ndio iwe asubuh
Aandae watoto, na ahakikishe wameenda shule wakiwa safi
Sasa kama wewe saa 11 uko nyumbani,mke anarudi saa ngapi na nani anaandaa chakula cha usiku,

Mke akishindwa kumuandaa mume na watoto mpaka kuhitaji usaidizi wako,iko siku atakuambia upike kuna wageni,mke hapaswi kuwa hivyo hapa wanakusifia na kucheka na wewe lakini shughuli ya familia yako unaijua wewe mwenyewe.
Mi mawazo yangu tu
 
Mkuu, Mm kwa ratiba yangu nmefanya hayo, kila mmoja kwa ratiba zake ajitahidi kufanya kilicho sahihi. Ndiyo maana nmeukiza hapo ratiba za wengine ili tujifunze.
 
Yaani kila siku mambo mapya aiseee kazi kazi tuuu mpka unasema hiki nini aiseeeee
 
Wife jioni huwa anapika, akimaliza tunakula na watoto, then inategemea either yeye au mimi huwa tunaosha kabisa vyombo, tunapiga story, tunaangalia movies au tamthilia kama zipo then by saa nne tano hv tayari chagani. Kuna wadau hapo wameshauri tuwe tunapiga pasi usiku, ntalifanyia kazi hilo. Ndoa yangu ina miaka 7 now.
 
Nikiamka ninasign in ofisini remotely kisha ninatafuta bar ya karibu nikanywe wakati ninafanya kazi zangu kwa pc (sometimes ninafanyia home sitoki kabisa).

Sina kabisa muda wa kusaidia kazi za nyumbani. Mimi kazi yangu ni moja tu: KUHAKIKISHA HELA HAZIISHI NYUMBANI KWANGU
 
Hongera mkuu, mm siwezi fanya hivyo nahisi roho inanisuta
 
Mazoezi unafaanya sangapi
 
In fifty years; itakuwa vigumu sana kutofautisha wanaume na wanawake.
 
Nnaamka saa 1:45
naoga na kuswaki
nnavaa nakwenda kazini
saa4 chai
saa9 chakula ccha mchana
saa 11 niko geto(unless itokee dhalula)

hapo tuonane kesho yake
mala moja moja kutoka usiku na wana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…