Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

haina noma ila kwenye mali labda tulizochuma wote, kama alinikuta nazo BIG NOOOOOO
Sasa kitendo cha kuchuma wote mali maana yake amekusaidia majukumu yako, mfumo dume unataka mume umhudumie mkeo kwa mali ulizochuma mwenyewe, bila kutegemea akusaidie majukumu yako
 
Apana sio halali kuendelea na mfumo dume, kila mmoja apambane chakula kiwekwe mezani mkizinguana mkashindwana, kila mmoja apite kushoto .

Ndio maana tunaukataa mfumo dume kwa kuwapa mabinti zetu elimu na kuwafanya wajiamini na kujipambania kama tufanyavyo wanaume .


Humu watu wanataka mfumo dume kimaneno ila kimatendo wanapambana binti zao waende shule za maana wajitambue, na kuwa na maarifa ya kujipambania.
 
Toa mashoga hapo, ushoga hauhusiani na matatizo au kutokua na akili, sijuagi kwann huwa mnahusisha nalo hili.

Mbona mashoga ndo wanao ongoza ku run dunia kwa sasa, wakiwa wana deliver vitu mbali mbali vinavyorahisisha maisha ktk nyanja zote.
"Ushoga ni ukosefu wa akili" Wewe ni mjinga kama wajinga wengine .
Hapa sijazungumzia wale wanaofanya ushoga kama sexual identity yao bali wale wanaofanya ushoga ili kutafuta urahisi wa maisha na hao ndio wengi sasa mimi sijui kuwatofautisha kwa majina ndio maana nikawa address tu kama mashoga, mimi huwa siwalaani mashoga na at times huwa nawatetea lakini huwezi kuwaweka kundi moja watu kama kina Steve Jobs au Tim Cook na hawa vijana wa mitaani wanaofanya ushoga kama kazi ili wapunguze ukali wa maisha na si kwamba eti wanapenda, ndio maana nikawaweka kundi moja na machawa maana wao wanaona hizo ni kazi lakini ukweli ni kwamba hawana akili kiasi cha kuwalinganisha na baadhi ya wanawake
 
Oohh kwa michango yako huwa nadhani na wewe ni muumini wa mfumo dume mkuu, kiukweli wanaume wengi ni wanafiki sana wanataka mfumo dume kwa wake zao ila kwa mabinti zao hawautaki, ukiwauliza vipi unataka binti yako naye amtendee mumewe kama vile unavyotaka mkeo akutendee wewe hawana majibu
 
vipi mfumo dume unatambulika kisheria? hapa na maan ya kwamba ikitokea tumeachana, mali tulizochuma wote tunagawana, ila mali zangu alizo nikuta nazo au zake nilizomkuta nazo hatugawani.
Sasa kitendo cha kuchuma wote mali maana yake amekusaidia majukumu yako, mfumo dume unataka mume umhudumie mkeo kwa mali ulizochuma mwenyewe, bila kutegemea akusaidie majukumu yako
 
Huo mfumo umepitwa na wakati ukiiendekeza kila siku utakua na makasiriko ,mwisho wa siku unakufa bila furaha, watu huwa wanabadilika.
 
Kiongozi hata mimi pia sikubaliani na mfumo dume. Palipo na mfumo dume hakuna UPENDO. Na sisi wanaume tumeelekezwa kumpenda mwanamke. Kupenda ndani yake kuna kujali, kumlinda, kumuelekeza kwa staha, kumtekelezea mahitaji yake na vyote vinavyoendana na upendo. Mwanamke ameelezwa amtii mwanaume.

Naongezea hapo kama mwanaume ambaye hana upendo kwa mwanamke haina haja ya kumtii na
hili pia lipo automatic mtu ambaye hana upendo kwako huwezi kumtii kwa hiyari labda kwa kuogopa. Mwanaume asiye na upendo kwa mwanamke huyo ni sawa na muuaji.

Tunapo tekekeleza maagizo ya Mungu katika kuishi mwanaume na mwanamke inakuwa ni mzunguko (circle) mwanaume ampende mwanamke, mwanamke amtii mwanaume, watoto wawaheshimu wazazi na watu wote wapendane. Hakika kama tungefuata haya wote kwa pamoja usingesikia jambo baya katika jamii zetu. Hiyo kwa ufupi formula tuliyowekewa na Mungu, ni rahisi sana kuifuata kama binadamu akiamua.

Kuhusu 50/50 sikubaliani nayo kwa sababu ina muumiza mwanamke mwenyewe na kuharibu mfumo mzima tuliowekewa na Mungu. Niweke wazi hapa katika 50/50 simaanishi fursa ya jambo fulani kati ya mwanamke na mwanaume kama vile elimu, kazi, afya, umiliki wa mali, biashara, n.k. Mwanamke na mwanaume wote wanahitaji fursa sawa kama nilizo eleza hapo juu.

Ila sikubaliani na MFUMO DUME (Kumyanyasa mwanamke) ❌ na pia sikubaliani na kuweka mazingira ya kumfanya mwanamke awe kiburi na jeuri cross ❌, haya yanasababisha kutengeneza watoto wasio na heshima, adabu na baadaye kuja kuwa wezi, mafisadi, n.k.

50/50 inayoongelewa na wengi ni kumfanya mwanamke awe juu ya mwanaume hususa katika familia (yaani kuwa kichwa cha familia huku mwanaume akiwepo) jambo ambalo ni kosa ❌.
 
Mfumo dume ni jambo ovu pia.
 
Nina majibu manne kwenye hii paragraph yako.

1.

Majukumu ya nyumbani hayana uhusiano wowote kwenye kufanikisha maendeleo.

Na ndio maana hata tunapo waoa mnatukuta tayari tupo kwenye progress tushafanya achievements kadhaa na hivyo tunaamua kuoa kwa lengo moja tu la kupata familia.

Kwa maana hiyo tunaona jinsi mwanaume alivyoweza kufanya maendeleo hayo pasipo kuwa na mwanamke huyo wa kumsaidia kazi za nyumbani.

Hiyo inatupa tafsiri kwamba uwepo wa mke kufanya kazi za nyumbani haina mchango wowote kwa mume kuweza kufanya maendeleo ambayo baadaye huyo mwanamke naye ahesabike kuwa ni sehemu ya maendeleo.

Hata nyinyi mara nyingi tunawaona vipaumbele vyenu katika kuolewa huwa mnataka muolewe na mtu ambaye tayari amejipata eidha ana pesa au kazi ya uhakika.
 
Lakini hoja nyingine

2.
Kama kazi za nyumbani ndio kiwe kigezo cha kutaka ulipwe, vipi kama tukisema malipo yako yalifanyika kupitia mali?

Vipi nikisema ile mali ndio thamani yako wewe ambayo wazazi wako walikuthaminisha, na mimi baada ya kutoa hiyo mali ni lazima ufanye majukumu ya nyumbani ili kuifidia ile mali?
 
Lakini

3.

Vipi kama nilikuwa mtu wa huruma nisiyependa kukuona ukihangaika na hivyo kuamua kutafuta mfanyakazi wa kukusaidia?

Bado utaendelea kudai 50/50 ya mali kwenye kazi ambazo hufanyi wewe??
 
4.

Wapo wanawake wenye pesa na kazi zao nzuri waliolewa na wanaume choka mbaya.

Wanaume hao hawana kazi, mke ndio anaye hudumia familia kwa kila kitu.

Huyo mume anaweza akawa anafanya vikazi vidogovidogo pale nyumbani kipindi mke yupo kazini.

Kwa hiyo unavyoona wewe huyo jamaa siku wakiachana na mke wake, anayo hiyo haki ya kudai 50/50 kwa kigezo cha kazi za nyumbani kipindi wife yupo job?
 
Sasa kama hilo lipo kwanini ukatae kutangulia mbele kwenda kupambana na jambazi kwa kigezo cha maumbile??

Ni kweli wanawake wanasita sita sana na hiyo kwasababu ya sisi kuwadekeza.

Kumbe udhaifu wa wanawake upo kwenye hesitation.

Hata kwenye mgawanyo wa mali tunapaswa kufanya kila linalowezekana msipate chochote ili tuwape ujasiri wa kutafuta vya kwenu.
 
Kwanza nataka nijue, nawewe ni mmoja wapo wa hao wanaofanya kazi ngumu??

Halafu kuhusu makomandoo wa kike kuna kitu hukijui.

Hao makomandoo wa kike unafikiri wana hitimu kozi yenye mafunzo sawa na makomandoo wa kiume?

Unafikiri komandoo wa kike ni sawa na komandoo wa kiume?

Hao ni makomandoo wa kike dhidi ya wanawake wenzao ambao walishindwa kufuzu hayo mafunzo.

Unafikiri kwanini kwenye parade za majeshi yote huwaoni makomandoo wakike wakivunja mawe kwa kichwa??
 
Inawezekana ukawa na majukumu mengi kakini yasiwe magumu.

Na mwingine akawa na jukumu moja likawa gumu kuliko hata yule mwenye majukumu mengi.

Mfano wewe upo nyumbani majukumu yako ya kila siku ni usafi wa ndani, kupika, kuosha vyombo, na baadaye kumuandalia mumeo maji ya kuoga.

Ukimaliza hapo kinachofuata ni kuangalia Sinema zetu na kuchati tu kwenye simu.

Hii haiwezi kufanana hata na mtu anayefanya kazi ya zege.

Ni kweli kupigana na jambazi haiwezi kuwa ni jambo la kila siku lakini lilipaswa kuwa katika sehemu ya sera zenu kwenye kunadi 50/50

Hiyo ni kuonesha kuwa 50/50 sio mkakati wa kimaslahi unaodiki kwenye vitu simple bali ni fairness katika kila aspects
 
Na mahali tulipe wote.
 
Hii 50/50, imekuwa strategy ya muda mrefu ya mabeberu kusambaza ushoga duniani.
Je, waweza furahi kuona kijana wako wa kiume akijihuaisha na ushoga?
Faida kuu ya mfumo dume ni kuandaa vijana madume kweli kweli.
Siyo kijana wa kiume ajionaye kuwa sawa na Binti Kwa namna yoyote.
 
Ni kweli wamekuwa wakitumia 50/50 kama gia ya wema lakini imekuja kubadilika baada ya kuingiza masuala yasiyofaa katika jamii.

50/50 naikubali katika fursa kama vile mwanaume na mwanamke wote wanaweza kusoma, kupata kazi, kumiliki ardhi, biashara, n.k.

Lakini napo pia kama ni kazi lazima kuangalia uwezo maana kuna kazi ukimpa mwanamke ni kama unamnyanyasa alkadhalika na upande wa pili pia. Mfano kama kazi zinazohitaji nguvu zaidi au mazingira magumu, hizo zinawafaa wanaume zaidi kutokana na asili ya miili ilivyoumbwa.

Tunapokuja katika familia au ndoa mwanaume na mwanamke kila mmoja amepewa majukumu ambayo yanafaa kulingana na uumbaji wa Mungu ulinyofanyika na ametoa maelekezo namna tunavyopaswa kuishi.
 
vipi mfumo dume unatambulika kisheria? hapa na maan ya kwamba ikitokea tumeachana, mali tulizochuma wote tunagawana, ila mali zangu alizo nikuta nazo au zake nilizomkuta nazo hatugawani.
Mkuu sijui kama umeelewa hoja yangu, mfumo dume hauangalii mali mmechuma wote au la mfumo dume unataka umhudumie mkeo, and yes mkiachana mnagawana mali bila kujali mmechuma wote au umechuma peke yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…