Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Hata kama huna akili jaribu kuongea kama una akili.

Na kisha tenda wema nenda zako. Ukiwa na duka mtaani kwenu, usiishi kwa matarajio kwamba ukimsaidia jirani yako basi lazima aje kwako kununua huduma. Kama kuna mahali wanauza bidhaa kwa bei nafuu zaidi yako wana uhuru wa kwenda huko. Na kama anatengeneza vitu unavyouza huwezi kumwambia asifanye hivyo ili anunue kwako.

Tuliwasaidia Msumbjiji, South Afrika, Angola, Zimbabwe, Namibia nk,kupata uhuru. Leo hii bidhaa zao na mazao lazima wanunue kwetu? Nini maana ya free market economy kulingana na kanuni za SADC?
 
Kuna mizigo inatoka south africa inakuja tanzania kupitia tunduma, kua malawi ashindwe kutumia south africa!!? Si maamuzi tu na kuamua!!?
Na unaju Malawi ni njia inayotumiwa na Tanzania pia kuleta bidhaa toka South Africa? Sio lazima upitie Zambia
 
hapo kwenye FREE MARKET economy umemaliza kila kitu,....kama kweli ni FREE, jibu rahisi ni kuwa bandari, mazao na barabara ni zetu,.. hivyo tuko FREE kumuuzia na kumuudumia tumtakaye bila kuladhimishwa na yeyeto,...wamalawi na wao wako FREE hata kutumia bandari ya south Africa au msumbiji na sisi hatutawauliza kwanini hawataki kutumia vya kwetu,......mkuu kwa heshima na taadhima hao watu hawafai hata kidogo,......
 
We mwendawazimu kweli, wao wamezuia bidhaa za kilimo za Tz kuingia ndani ya mipaka ya nchi yao., sasa kwanini sisi turuhusu, iwe kwa kupitisha au vyovyote vile..,

Hao South Africa wanatuzuia kuingiza ndizi kwao, ila sisi wanaleta maApple kila siku, kwanini na sisi tusizuie hadi wao watakaporuhusu?

Pia kama unakataa bidhaa moja wapo ya kilimo, basi kataa zote, hata mbolea usiitake..
 
Unakosea maana ya FREE MARKET. Tofautisha kati ya freedom of choice to serve, discrimination na spiting

Leo ukienda hotel ya wachina ambapo wana "freedom of entry is reserved", wakasema hawahudumii watu weusi, utasema wana haki kufanya hivyo kwa sababu wana freedom of entry reserved?

Huwezi kutumia freedom ya kuhudumia kama adhabu. Yaani mtaani kwako mangi akatae kumuuzia mkeo chumvi kwa sababu kamtolea nje alipomtongoza, halafu wewe useme hiyo ni freedom ya mangi?
 
Huelewi, kaa kimya, soma ujifunze
 
Wenyewe wamekubali kwamba hii ni TIT FOR TAT
 

Attachments

  • 20250418_123530.jpg
    217.5 KB · Views: 27
Bashe amesahau kuongea na Mama

1.Tuwafukuze hawa Wamalawi wote waliojaa hapa kwetu.

2.Piga marufuku gari zote za Malawi zisikanyage ardhi yetu.
K8matwifa haikubaliki, nasi tunaweza wekewa vikwazo hasa kule tunakokopa matrolioni ya hela
Pinga pinga kazini
Kweli .
Yaani watanzania huwa hawaeleweki , Trump ameweka vikwazo vya kijinga kwa nchi za nje anaungwa mkono na raia wake, sisi huku tunaunga mkono jirani.
Hilo suala n
Linafaida na hasara. Mtu azuie mazao yako ila wewe umruhusu si ujuha huo!
 
Kama tunavyoijadili hii ishu Tz huko malawi pia leo hii ndio mada inayojadiliwa zaidi.
kuna muda inatakiwa kuonyesha msimamo kama nchi.
Bashe alikuwa uso wambuzi akati anatoa ile statement ile ndio inavyotakiwa "hucheki na yeyote" .
pia waziri ameonyesha busara kutoa room ya wiki moja yakupata suluhisho nakama wataendelea kukomaa bas tusubir kuona atakaetoa mlio
 
Jifunzeni vita ya uchumi kwa marekani na China
Ttump alipoweka vikwazo vya bidhaa za China China kajibu ila ameongezea kuwa IP za USA haxitafanya kazi China, hivyo kampuni za zChina zizalishe bidhaa sawa na zinazozalishwa na USA. Je hii vita ina usawa, mbona China kazidisha makali kuliko mwen-ie Trump. Kwa hio vita haichagui siraha, ukiona kuna upenyo piga hapo hapo.
Mda mwingine ni fundisho kwa wakati ujao hasa atakaepoteza.
 
Hakuna point ya kujibu pale, na sitaki kukuheshimisha kwa kukujibu ili uonekane umeongea vitu vya maana
Namna pekee ya kuonyesha hakuna point ya kujibu, ni kujibu, otherwise ni kukosa hoja.

1.) kama wamezuia bidhaa za kilimo za Tz kuingia ndani ya mipaka ya nchi yao., sasa kwanini sisi turuhusu, iwe kwa kupitisha au vyovyote vile..,

2.) Hao South Africa wanatuzuia kuingiza ndizi kwao, ila sisi wanaleta maApple kila siku, kwanini na sisi tusizuie hadi wao watakaporuhusu?

3.) kama unakataa bidhaa moja wapo ya kilimo, basi si inabidi ukatae zote?, Mbolea included?.
 
Halaf hao SA na Malawi ndo washkaji zetu ambao huwa tunakipiga pamoja huko Kivu chini ya ☂️wa SADC au ndo tumeimbiliziwa "BABAAA! YAFARAKANEEEE! .
Sijui nin kmetokea tena. Anyway binafsi simuoni Bashe naiona serikali.

Hapa abiria ni mwendo wa kulala botin kimyaa!!
Haijalishi tunakoelekea au kuna dhoruba kias gani,kikubwa tuu tujue tuko baharini na team nahodha are everything.

Team nohodha hawataki kelele za abiria,tukizingua tunatoswa baharini.

Lakin tusihofu enyi sisi abiria hatuta angamia yupo mkuu kuliko akili za binadamu/crew ya manahodha, yeye ndiyo KIONGOZ na MWAMUZI WA HAKI.
 
Mkuu inategemeana wataalamu wa uchumi na diplomasia wamezingatiwa kias gani ktk maamuz hayo.
Pia hilo la jino kwa jino inawezekana tumewa-underlook malawi. Hivi unadhan ingekuwa uganda au rwanda tungeamua haraka na kwa jeuri hivyo??.
Kama halina madhara kiuchumi fresh tui ila kama inatucost bhasi ngoja tuseme, Amen!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…