Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

Moja kati ya sifa ya ma atheist ni kwamba yanakuwaga majitu yenye akili Na kufikiri sana, hilo ninalitambua. Ni watu ambao hawapendi maelezo sahili ya vitu vitata. Ndio maana mnayakataa maelezo rahisi kumhusu Mungu. Lakini msiishie kukataa kila kitu tafuteni maelezo ya uhalisia wa Mungu sasa.

Labda waliochukua jukumu la kutusambazia na kutuelekeza kuhusu Mungu na mambo ya kiroho enzi hizo waliwakuta watu simple minded ndio maana kila wakiwaelekeza hata kwa lugha nyepesi na vimifanomifano, wale watu wanaelewa kidogo uhalisia ila mifano ndio wanaikazia sasa!. Mfano vitu kama Bwana wa majeshi, mfalme mwenye nguvu vilitumika baadae kwa watu ambao akili yao iliwaza vita na ukombozi. Wa zamani zaidi wana vitu kama Ancient of days [hawa watamchukulia kama ana madevu meupe na baraghashia] sikumbuki vingine. Ni vile tu lile wazo la mungu linaeleweka kulingana na akili ya yule anayeambiwa. Inategemea na uelewa wake na imagination yake. Lakini Mungu mwenyewe alianza na kitu abstract tu moja kwa moja - IAM THAT IAM!

Moja ya lengo la hii mada ni kulithibitisha uhalali wa lile wazo la 'umungu' tuanze kwanza kwa kutambua kuwa hilo ni wazo halali halafu baada ya hapo ndio tutajadili na kuendelea kumtafuta na mambo yanayohusiana na yeye yapojepoje. So ukifanya kosa la kulikataa wazo mojakwa moja huwezi kulisoma zaidi wala kukua katika ufahamu wake. Kwa hiyo mimi leo nikikuambia; Ichukue hiyo natural selection, halafu badala ya kuiacha kama a 'mindless/purposeless phenomenon of nature', ikubali kwamba iko na inafanya machaguo yake kwa akili kulielekea lengo fulani. Natural selection sio mungu mind you, hiyo ni sehemu tu ya hekima yake Mwenyezi.
 
Yaani we jamaa, ivi mfano ukienda huko kwenye ma dark matter ma dark energy. Unapoambiwa balance ya kani za expansion na contraction zilivyo bado tu unabaki na wazo la mindless chaos of matter. Tofauti ya kuzidi kwa atomu tano tu ingetosha kufanya ulimwengu ucollapse -gravity ingezidi. Na kama gravity ingepungua kwa kijisehemu kidoooooooogo sana kasi ya kusambaa ingezidi na tusingepata chochote! Bado tu hutaki kukiri kuwa haya mambo yanaongozwa? Kani zote zinaongozwa na akili ndio sababu mambo ya maana yanajitokeza baadae bro.

Hata hivyo mtaelewa tu maana meshaanza kuona vitu ambavyo lazima vitawapelekea kuwaza kuwa kuna kitu zaidi ya juu ya maada. Eti ooh ukichukua dark matter ukaweka kwenye kaboksi kadogo inakuwa na uzito mdogo, ukilikuza boksi marambili uzito unajidouble!! halafu eti ooh sayansi ni vitu vinavyoshikika tu. Mtaelewa tu. Mojawapo wa kazi za roho ni kudizaini, kufinyanga na kuongoza vitu kama ma bigbang. Kutunga kanuni zitakazouongoza ulimwengu kuanzia mwanzo leo na hadi mwisho na kupatia. Kwa lugha ya kawaida tunayoielewa tukaambiwa 'And let there be light' lakini kiukweli hapo utakuta ni maformula, ma kani mazitomazito na li akili likuuubwa sana, kubwa mno. Ni noma.
 
Na kabla hatujaendelea zaidi hii itawahusu wote masdinero masproblemas na Kiranga hivi mlishawahi kufanya zoezi la kutilia shaka kila kitu? Nalipendekeza maana naona kama linaweza kusaidia.

Jaribu kukaa mwenyewe na kutilia shaka kila kitu ulichoelekezwa kila elimu uliyopewa. Tilia shaka dini, tilia shaka Mungu, Sayansi, Philosophy kila kitu hadi cosmology. Kisha anza kuyakubali mambo kwa kupitia ushahidi wa vitu unavyothibitisha mwenyewe sio kusoma maandishi na picha.

Kwa faida ya wote nitatoa mfano wa ugunduzi/realization yangu mfano mimi; Nikizungumzia baiolojia mfano mimi ninao ushahidi ninawaona watu, wanyama, mimea. Nimeviona viseli kwenye hadubini, nimekaona ka plasimodiamu. Nikaamua kujenga ukweli kutokana na msingi huo mwisho nikafikia kwambaa;
Theory of everything (Nadharia [yangu] ya kila kitu)
We are of God and we live for mankind. (Sisi ni wa Mungu na tunaishi kwa ajili ya wanadamu). Anything done in that statement is right, anything contrary to this statement is left. Living and doing according to this statement is healthy and therefore right. Always healthy things are right.
 
Natilia shaka kwamba wewe upo.
 
Natilia shaka kwamba wewe upo.
Hii haina afya, hivyo sio sahihi maana ukipelekwa kwa daktari wa akili ukaulizwa kuhusu statement 'Natilia shaka kwamba wewe upo' uliwezaje kumuambia huyo uliyemtilia shaka na bado ukategemea majibu toka kwake? Huoni unajichanganya imani yako na maneno yako? Atahitimisha you re incoherent and even seeing things, or unseeing things to be exact!

Sentensi yako ingekuwa sahihi kimantiki ungeiweka katika nafsi ya tatu kama unavyofanyaga kila siku kuhusu Mungu
ungesema ivii 'Masdinero natilia shaka kama Uhakika yupo' hapo sawa.
 
Ongea na Mungu mwambie kule Ukraine watu aliowaumba Putin anawaua kinyama bila huruma yoyote. Mbona Mungu kanyamaza!

Mwanzo 1:27, na Tuumbe Mtu kwa sura na mfano wetu akatawale duni, utawala wa duni alipewa Mwananadam na mwanadam anawajibika kwa kila uharibifu wa Dunia, ndo maana ilimcost Mungu kuwa mwanadam.

Sasa basi, katika maombi Yesu alifundisha, kuna sehemu inasema tuombe ufalme wake uje, kwa hiyo ni kwamba tuna mamlaka na kuamua nini kifanyike duniani, tunaweze kabisa mzuilia Mungu, Mungu anaweza kila kitu mpaka aseme vinginevyo, na ameamua kufanya kazi na wana damu.

Ubaya wowote unaofanyika duniani ni sababu ya mwanadamu, Mungu hausiki hata kidogo.
 
Kwani wapi nimesema nategemea majibu kutoka kwako?

Na hata nikitegemea jibu, kwani wewe hujui kwamba hata ma online bot yanaweza kujibizana na wewe?

Haiwezekani kupata autoreply from an online bot bila ya mtu kuwapo?

Na wewe si uliyeniambia nitilie shaka kila kitu?

Sasa mbona nafuata ushauri wako na kutilia shaka uwepo wako, halafu unanishangaa kwa kufuata ushauri wako mwenyewe?
 
Who is God?

Does God exists in physical or spiritual world?
 
Asante sana sana kumuelewesha. Exactly hiki ndicho tunachokimaanisha tukisema 'we make shit happens'. Tunayo nafasi ya kufanya mambo tunavyoamua na tutapambana na matokeo yake mbele kwa mbele.

Lakini tukijitiisha na kuamua kufanya mambo kulingana na mapenzi ya Mungu hiyo ndiyo itakuwa tumepatia. So utawala wa dunia tumepewa na uwezo wa kuamua tunajichagulia
 
Poa bhana endelea halafu tafuta kuvikubali kwa uthibitisho.

Kwanza ukilinganisha na mimi wewe mashaka yako yameanzia mbali. Mimi nilianza kujitilia shaka mwenyewe kwanza kama nipo! nikaenda hadi nikaestablish kwamba nipo. Ndio maana ninawaza na ninajiuliza kama nipo. Na kwa kuwa mtu ni 'mawazo yake' kama alivyosema Munga Tehenan katika kitabu chake cha UCHAWI. Basi mimi nipo.

Ndo nikakua nikatilia shaka kama wengine wapo au kingine chochote kipo. Mfano nahisi ulishaskia lile swali kwamba 'How do you know that the moon is there, when no one is looking at it'. Kuna watu wana uwezo wa kukuaminisha kwamba watu wote duniani wakisahau wakaacha kufikiri kuhusu mwezi - mwezi utakuwa haupo! hadi formula watakuchorea!!. Watakuambia vyote unavyoona ni akili yako inavijenga muda huohuo paap!! Basi nikakataa huo ujingaa nikaestablish kwamba mimi nipo watu wengine wapo na vitu vipo. Basi nikaisoma miti na wanyama na mimi nikapata kwamba vinaishi kwa lengo, kazi na kanuni kadhaa ambazo hadi sasa bado najifunza. Nilianza na vinavyoshikika na mimi.

Sijawahi kuthibitisha galaxy nyingine zipo wala viatomu lakini kwa hivi nilivyovithibitisha sipati tabu kupokea maelezo ya vitu vingine kwa ukweli wake. Mfano huu ukweli wa kwamba mifumo inaundwa kwa lengo maalumu na inalitumikia hilo lengo. Hilo lengo ni kila kitu katika mfumo, ni zaidi ya mfumo, lipo juu katika mfumo na lipo pote katika mfumo at the centre and the circumference thereof. Lengo linaupenda mfumo. Lengo ndio mfumo lakini huwezi kusema mfumo ndio lengo na ukawa sahihi kwa asilimia mia.
 
Who is God?

Does God exists in physical or spiritual world?
God is what IS. Hafananishwi. Think of the highest concept of beauty, truth, life, light, love, intelligence, purity etc, those are some of the properties of God.

About being in spiritual or physical world. You know you are thinking in physical terms so your answer is a bit complicated. It is like this;
The spiritual realm is above the physical, but it is also before the physical. It is the centre and the circumference thereof. Meaning the spiritual world interpenetrates the whole physical world while being above and before. God is spiritual so is in the spiritual world and that is another way of saying EVERYWHERE.
 
Roho ni nini?

Thibitisha roho ipo kweli nje ya habari za kufikirika tu.
Leo umebanwa tena kwenye 18 hadi umetoka nnje ya mada ambavyo nilikubananishaga mimi hadi ukaishia mitini [emoji1787][emoji1732][emoji851]
 
Umethibitisha vipi kwamba upo? Na una uhakika gani uthibitisho wako ni thabiti?
 
Leo umebanwa tena kwenye 18 hadi umetoka nnje ya mada ambavyo nilikubananishaga mimi hadi ukaishia mitini [emoji1787][emoji1732][emoji851]
Nje ya mada wapi? Na unajuaje hapa ni nje ya mada si wewe tu hujajua kutenganisha nje na ndani mpaka uko wapi?
 
Umethibitisha vipi kwamba upo? Na una uhakika gani uthibitisho wako ni thabiti?
Kwangu mimi ilikuwa rahisi tu kama nilivyosema inaanzia kwenye tafsiri ya 'mimi ni nani'. Kwa kuwa nilishadefine mapema kwamba mimi au ule umimi ni lile wazo la mimi, ule ufikiri wangu kwamba mimi ni. Ninazo sehemu mbalimbali za mwili ili niweze kuinteract na mazingira na watu wengine.

Yaani mtu kama mtu ni lile wazo la uyeye ule ufikiriaji wake au mawazo yake. Ndo maana utaskia 'tumuulize Kiranga tumsikie anasemaje' -Ujue tunalitaka wazo la kiranga ndio kiranga mwenyewe huyo.
Mdomo ni mdomo wako na unaweza kuwa kiranga bila mdomo tutayapata mawazo yako kwa namna nyingine utaandika.
Mikono ni mikono yako tutawasiliana na kiranga hata asipokuwa na mikono.
Kichwa ni kichwa cha kiranga hadi ubongo ni ubongo wa kiranga sasa kiranga mwenyewe ni nani? lile wazo hai la kiranga, ule ufikiri wake ndio kiranga mwenyewe.

Mimi sikupata tabu kujua kama nipo kwa sababu nilichukulia kule kukaa tu na kuwaza kama sipo au nipo tayari inaonesha nipo maana wazo la mimi ni hai na nipo nachanganua mambo hayo. Nilijua wengine wapo kwa sababu kuna mda unakutana na watu wabishi na tunakuwa na mawazo tofauti kabisa kuhusu uhalisia. So Kiranga yupo na Interlacustrine R yupo pia.
 
Unajuaje kwamba wewe upo kweli na si wazo tu?
 
Unajuaje kwamba wewe upo kweli na si wazo tu?
Hahahahaaaah huhuhuuuuuh! amaa kweli basi tuanze na swali la mtu ni nani labda. Mtu ni nani bwana Kiranga.

Nimeona umepuuzia jinsi mimi nilivyomtafsiri mtu, hebu tukusikie na wewe unasemaje. Mtu ni nani au ni nini?
 
Au ndo tutarudi kulekule mwanzo kwenye swali la je? wazo kwako ni 'kitu halisi' kwa kiasi gani.
 
Hahahahaaaah huhuhuuuuuh! amaa kweli basi tuanze na swali la mtu ni nani labda. Mtu ni nani bwana Kiranga.

Nimeona umepuuzia jinsi mimi nilivyomtafsiri mtu, hebu tukusikie na wewe unasemaje. Mtu ni nani au ni nini?
Kwa nini unakuja kwa mtu kama hujaweza kujithibitisha wewe upo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…