Mishahara kuchelewa, kipimo kingine cha uwezo wa Rais Samia

Mwisho wa mwezi ni tarehe 30, leo ni tarehe 24, unawezaje kulalamika?
Pili, ukiona mwajiri anakulipa mshahara mapema sio kwamba anakupenda sana, anacheza na akili zako, kama huamini jaribu kuhesabu ni siku ngapi zitapita kabla ya kukulipa mshahara utakaofuata.
 
Wapi mnakoenda? Na unaenda na nani?
 
Mark my word....Soon mishahara yenu itaanza kulipwa tarehe 2 of the next month [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
serikal haijawah kushindwa kulipa mishahara yake.
24 ni mapema sana...
acha kulalamika vitu vya kitoto.
Nafikiri mdau anazungumzia kuchelewa na sio kushindwa kulipa.

Najaribu kumuelewa kdg, hamaanishi kwamba hela hakuna, Bali Mama amekuwa mpole kiasi ambacho watumishi hawaogopi kuchelewesha mshahara, na Kama unaweza kuchelewa mshahara was nchi nzima na watu wore wanaona na wanajua jee Mambo mengine yanayogusa watu wachache na yasiyojulikana yatachelewa kwa kiasi gani!?
 
...lakin kama pia unaona ni ishu. tafuta biashara kuliko kukaa unasubiria mshahara wa serikal.. halad ulichelewa unalalamika.
boss hanuniwi
Hata mfanyabiashara huwa anacheleweshwa kupata hela pale ambapo wateja wanakosekana. Mara kumi hata mtumishi wa umma huwa inatabirika, biashara huwa hazitabiriki. Au mmesahau wale waliobaki na mbaazi majumbani mwao juzi tu hapa?
 
Utetezi mwingine wa kipuuzi huu!!
 
Watumishi mnadeka sana.. Tarehe 24 unakuja kulia lia humu!
 
Kila mwisho wa mwaka huwa inachelewa jpm ana husika vipi sasa
Mnachotetea hata sikielewi. Mishahara hulipwa hata before 23rd mwezi wa 6 za kila mwaka miaka yote ya JPM akiwa rais. Serikali hulielewa hilo na hulipa mishahara mapema ili kujiandaa kwa ajili ya mwaka mpya wa fedha.
 
Upumbavu wako ndio unakufanya uwe mtumwa wa mishahara

Wekeza kula mazao ya mshahara sio kula mshahara

NB "Kuna marekebisho makubwa ya madaraja na kulipa baadhi ya malimbikizo hivyo mvumilie mpaka jumatatu"
wakati mwingine ushukuru mtu wa aina hii maana anaachia fulsa wasio na ajira nao waichukue pesa yake maisha yaendelee.

wafanyakazi wanaofanya na biashara ni wajanja lakini ni wauaji pia,maana wanataka koye kote.
 
Mwenye busara hujibu hoja kwa hoja. Ukiona mtu anajibu hoja kwa matusi kichwani kuna vitu haviko sawa. Hebu tingisha kichwa kidogo unahisi nini?
Nimekujibu hivyo kwa sababu hukuwa na hoja ya maana. Mwezi ni siku 30 na siyo tarehe 30. Kimsingi nchi zote zilizostaaribika huwa na fixed date ya kulipa mshahara. Sisi kwetu kwa muda mrefu tumekuwa tukilipwa on 24th hivyo kwenda mbele ya tarehe hiyo inaamsha tahadhari, hasa kipindi hiki.
 
Acha kulalamika wewe. Hiyo ni issue ndogo sana ndugu.
 
Kwahiyo leo watumishi mnamkumbuka Magu jinsi alivyokuwa mwema kwenu?

Hivi watumishi nchi hii mna akili timamu kweli ?
Yaani nianze kumkumbuka Magu kwa lipi eti kisa mshahara haujalipwa tarehe 24?never never,hata tukilipwa tarehe 30 sina shaka na mh rais Samia,najua na waziri kasema mwezi huu mishahara ya madaraja mapya inaanza kulipwa na ndio sababu ya kuchelewa.
 

Yani siku moja tu umeshaanza kulia lia njaa..mshaara wenyewe unaoulilia unaweza kukuta ni laki 5..funguka akili tafuta uhuru wako mwenyewe wa kiuchumi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…