Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kiubinadamu wakati umefika wa kuacha kufikiria waisrael wangapi walikufa wakati wa shambulio la Hamas na wapalestina wangapi wameshakufa tangu Israel ianze kulipiza kisasi.
Au majengo mangapi yamegeuzwa kifusi.
Kinachotakiwa sasa ni kufikiria watu wanaokufa njaa na kiu kwa kunyimwa chakula na maji kwa makusudi.
Maji, umeme na chakula vimezuiwa kuingia Gaza huku watu milioni 2.3 wanavihitaji haraka.
Ni wajibu wa kibinadamu kufikishwa mahitaji hayo haraka. Watetezi wakubwa ni wale wanaopakana na Israel na maeneo ya wapalestina.
Upo umuhimu wa kuikumbusha Israel inavyovunja haki za kibinadamu na kuipa kisogo mikataba walioingia pamoja nao. Pamoja na ukumbusho huo waipe Israel masaa 24 kufungua mipaka bila mashariti ili vyakula na maji na mafuta viwafikie watu ambao wameanza kufa kwa kuishiwa na vitu hivyo.
Kama ikiendelea kuleta ngonjera na kukazia kiburi chake waweke wazi kuwa baada ya muda huo wataacha kulinda mipaka hiyo na watakaopenda kuvuka kupeleka misaada watakuwa huru kufanya hivyo.
Si akili nzuri wala ubinadamu kumuachia mtu afe kwa kukosa chakula na maji wakati vitu hivyo vipo isipokuwa ananyimwa tu.
Nchi hizi zijifunze jinsi nchi za ulaya na Marekani zilivyolalamika na kuilaumu Urusi kuzuia ngano mpaka ikabidi waingie mkataba wa usafirishaji wa nafaka.
Walifanya hivyo kwa kuhofia madhara ya njaa kwenye nchi zao.Kwanini sasa wanaiunga mkono Israel iwanyime chakula na maji wapalestina wa Gaza. Bila kutekeleza wajibu wao wasitegemee akina Biden na Sunak na wenzao kuwatetea wapalestina.