Mitandao ya kijamii siku hizi imekuwa chanzo kikubwa cha stress na msongo wa mawazo kwa vijana

Umesema kweli mkuu.
Mie kisa changu, wakati niko chuo cha hoteli menejimenti, tulikuwa na kundi sogozi (group) la darasa letu. Sasa mtihani wa semester ya mwisho kabisa ya kozi yetu nikawa ninatakiwa kufanya mtihani wa kutimiliza (supplimentary), yaani kila nikikumbuka siku ile matokeo yalivyotoka, watu ambao hawana supp, wakawa wanatupia picha za majoho wanasherekea kuwa tayari wamekamatia vyeti vyao. Sasa hapo mie ndio nina supp sijui kama nitaitoa au ndio nita i carry nisihitimu mwaka huo husika. Ilikuwa kila nikiona watu wanavyoshangilia kwenye group mie nasononeka, mwishowe nili left kwenye group.
 
Sana unakua unamuumiza kisaikolojia
Ila mara nyingine bora kuuchuna tu, maana unaweza kujikuna upele tu kumbe kidole unachotumia kujikuna kina pete ya dhahabu tayari kama mtu ana roho nyepesi anakwazika.

Pia mara nyingine ishi maisha yako bila kujali watu.

Nakumbuka tulivyokuwa sekondari, siku moja nimekaa na machizi, basi mshkaji mmoja akawa anaondoka anaenda nyumbani.

Nikamwambia nitakupigia simu baadaye (enzi hizo land line kabla ya mobile). Tulikuwa na kawaida ya kupigiana simu mara kwa mara kwa sababu tulikuwa marafiki halafu majirani.

Basi jamaa alimind sana.

Akaniambia ulichofanya si poa, pale umekaa na washikaji kibao kwao simu ni kitu wanachotamani sana kuwa nacho kwa mawasiliano ya muhimu, lakini hawana, halafu wewe umesema utanipigia kupiga story tu.

Nikasema this is too much. Siwezi kujichunga kila ninalosema na ninalofanya ili nisimkwaze mtu tu.

Kuna watu wengine hata ukiwasalimia tu watasema, usipowasalimia pia watasema. Ukiomba mchango wa harusi watasema kila siku michango, ukisema harusi yangu sitaki mchango watasema unajivuna.

So sometime just live your life.
 
Kiduku Lilo ni hazina ya taifa. Serikali ikipungukiwa kwenye bajeti huwa inamfuata kuchukua mkopo.

Watu wenye mtizamo wa maisha kwa namna hiyo wanafaa sana. Ukiwaza kitajiri lazima mambo yako utayapeleka kitajiri, ukijijaza na mambo ya kifukara mtazamo wako kwenye kila kitu utakua hivyo hivyo.
 
Watu wenye mtizamo wa maisha kwa namna hiyo wanafaa sana. Ukiwaza kitajiri lazima mambo yako utayapeleka kitajiri, ukijijaza na mambo ya kifukara mtazamo wako kwenye kila kitu utakua hivyo hivyo.
Nilikuwa na option ya kununua tairi la gari la bei rahisi na la bei ghali.

La bei rahisi likipata pancha unaweka gari pembeni barabarani, unabadili tairi au unaita breakdown.

La bei ghali lina mechanism ya kupeta kama maili 50 baada ya pancha, linakufikisha nyumbani au gereji unabadili vizuri.

Nikasema ngoja niende na la bei ghali lililo salama zaidi, ingawa bei yake si mchezo.

Na kweli, juzijuzi kuna siku nimekanyaga kisumari gani sijui, dashboard ikaniambia upepo umepungua sana. Lakini nikapeta mpaka home, nikafika gereji, nikabadilisha tairi salama.

Ningefikiri kimasikini ningeweza kuingia gharama zaidi.
 
Hahahahahahhahahaha mkuu eti nikijikuna[emoji23][emoji23][emoji23]
kumkasirikia/kumfanyia kinyongo mtu alie nacho hio sasa ni roho mbaya..
Mimi binafsi ni kwamba kama natamani kitu katika maisha yangu mtu akiwa nacho simchukii/roho hainiumi kwa ajili yake
Ila kuna hali inakuja kuwa ivi mimi ntapata lini/hivi kuna uwezekano kabisa siku nikawa nacho..naamini kadri tunavyowabariki wengine na sisi tunabarikiwa
 
Unavyosema wewe ni jambo la kawaida kabisa. Na pengine hiyo ni chachu ya maendeleo. Na pengine hata hao wanaojionesha nao ni chachu ya maendeleo.

Wenyewe wanasema "fake it until you make it".

Ila kwangu mimi nimeamua kuweka mbele mambo ya experiences zaidi, bila kupost post.

Hata picha kupiga ni nadra sana.

Kuna watu wanateka siku hizi.
 
Hahahahaha na watakuteka kweli
 

We jamaa uliwahi kupost chumba kimejaa Perfume, ulinichanganya sana.

Mpaka nikawaza kama huyu jamaa assets zangu zinazidiwa na dressing table ya perfume tu, sasa mimi naishi ili iweje!

Hata hivyo nikasema niichukue kama changamoto, I thank God things look greener now.
 
Pole sana Mkuu
 
Mwenye nacho na awe nacho.....
asienacho atulie tu no harm....
tunapaswa kufahamu kwamba hatufanani kama vidole vya mkononi......
hakuna haja ya kuchukia yule aliyebarikiwa
kwa sababu anayetoa ni mmoja huyo huyo...
....aliyekupa ww gunia la sukari.....ndio ameninyima mimi hata kijiko kimoja kidogo cha sukari.....
hesabu zote kapiga yy
 
Yes ni kweli ila kaa wengine sio rahisi kama unavyofikiria wewe
 
Umeongea point kubwa sana
 
Nilichokigundua utakuta wale ambao mara nyingi wanapost picha za kuonyesha furaha na kuwa na Mali Kwenye social media ndio hali halisi ni kinyume chake.
Ukiona mtu anaweka sana picha ya Me/Ke na kuonyesha jinsi gani anampenda mkewe kiuhalisia wapo Kwenye ugomvi mzito.
 
Hahahhaaa mitandao inawafanya wadada wengi wamekuwa inferior
Akiangalia wadada wenzake wanapost wapo soft
Chuchu saa sita
Kiuno nyigu

Halafu yeye akijitizama ni kama mimi basi anapoteza ujasiri,
Anaanza kumuabudu mtu na editing apps !

Kumbe you're beautiful the way you are!
 
That's the spirit my man.

Zile colognes kwa sasa zimezidi mara mbili.

Nilikuta watu wanaongelea perfumes na colognes, na mimi kama kawaida yangu si mgumu wa kuchangia kwenye hoja ninayoipenda.

Na tangu siku ile sijawahi tena kupost zile picha.

Maana ilikuwa mpaka Nyani Ngabu mtu wa ma cologne hajaamini kama picha ya kwangu, alifikiri nimeiokota kwenye internet.

Na mimi nilijua watakuwapo watu wa kuhoji, kwa hiyo nilivyopiga picha niliweka kikaratasi nimeandika "Kiranga".

Nikamwambia Nyani Ngabi hebu zoom katikati ya picha chini utaona salamu zako hapo.

Mwenyewe alizima fegi, alimeza moshi na kuutolea masikioni.

Jivin'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…