Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania

Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania

Huyu ni mfanyabiashara na anatafuta soko popote duniani anapoona kuna fursa ya sera dhaifu za uwekezaji na soko la uhakika.

Kwa jinsi tunavyopigwa kwenye biashara ya vifurushi huku Nape anashangilia hakuna mtu hatotaka kuwekeza kwenye biashara hiyo kama ana uwezo.
 
Kakurwa kasema unapomshukuru mtu kwa kilicho haki yako huna maana.
Huyo Mzee ni wa hovyo kuwahi kutokea duniani...eti tutatumia dola kubakia madarakani na hapo ni kuelekea General Election ni jitu la hovyo sana, UDSM mpokonyeni degree zote mlizowahi kulipa hili jitu.
 
Wataalam hii imekaaje kwa mtazamo wenu itakuja kutuondolea shida ya gharama na network coverage/speed. Au maumivu yatakuwa bado yapo palepale?

Source: bbc swahili.

Huduma ya mtandao ya Elon Musk ya Starlink inatarajiwa kupatikana nchini Tanzania katika robo ya kwanza ya 2023, huku wachambuzi wakisema maendeleo hayo mapya yatakuza uchumi wa kidijitali.

Kulingana na gazeti la The Citizen Tanzania, huduma hiyo, ambayo inamilikiwa na Kampuni ya SpaceX, imekuwa ikitoa muunganisho wa intaneti kwa kutumia maelfu ya satelaiti angani ambazo huwasiliana na vipitishio vilivyoteuliwa vya ardhini.

Waliozungumza na The Citizen wanasema kuwa huduma hiyo mpya itachochea tu sekta ya kidijitali iwapo itauzwa kwa bei nafuu na kutoa mtandao wa kasi.

Kwenye tovuti yao rasmi, Starlink ilitangaza mpango wao wa kuleta huduma hizo kati ya mwezi Januari na Machi kulingana na idhini ya udhibiti.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jabiri Bakari alithibitisha kwa The Citizen kuwa Kampuni ya Starlink ilituma maombi.

Alipoulizwa iwapo anafahamu kuhusu kuwasili kwa Starlink Corporation, Dk Bakari alijibu: "Ndiyo, ninafahamu kuwa kampuni hiyo ilituma maombi kupitia tovuti.

Mataifa pekee ya Kiafrika ambayo hadi sasa yameiruhusu Starlink kufanya kazi ni Nigeria na Msumbiji.

Hii ilifanyika baada ya kupata vibali vya udhibiti kutoka kwa mataifa yote mawili.

Ikiwa Starlink itakuwa na athari kubwa au la itategemea jinsi biashara hiyo inatarajia kutoa huduma kwa haraka na kwa bei nafuu, kulingana na mwanauchumi Abel Kinyondo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

"Huduma ya mtandao sio anasa bali ni hitaji la msingi. Kasi yake ya juu na uwezo wake wa kumudu inaweza kumaanisha kasi kubwa na upatikanaji wa haraka wa habari,” alisimulia.
 
Hii huduma nime agiza vifaa vyake ebay naweza kutumia sehemu yoyote . ni rahisi kucofigure na app ya kutafuta setelite hipo kwenye simu
IMG_0081.jpg

IMG_0082.jpg

IMG_0083.jpg
 
Watu wa Teknolojia watu udadavuzi wa faida za kampuni kama starlink kuwekeza hapa kwetu!! Mshana Jr mizimu inasemaje…?
 
Tajiri mwenye vituko bilionea Elon Musk amevutiwa na mazingira ya uwekezaji Tanzania.

Wahafidhina wanasiasa wa chama dola kongwe cha CCM wenye maono mafupi suala hili la uhuru wa kupata habari msizikwamishe kama ilivyo ada yenu.

Raia wana kiu kubwa ya kujifunza mengi kupitia huduma za intaneti zilizo bora na nafuu kwa bei, maana huduma za intaneti siyo anasa bali ni muhimu katika ugunduzi wa tekenolojia mapya za kusaidia kilimo, uvuvi, ufugaji, biashara, elimu pia katika kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla wake.

WADAU WA SEKTA YA KILIMO WANENA JAMBO

19 November 2022

Department of Animal, Agriculture and Range Sciences

Sokoine University of Agriculture

Elon Musk set an eye to Tanzania​


Elon Musk’s internet service Starlink is set to be available in the country in the first quarter of 2023, with analysts cautiously saying the new development will boost the digital economy. The service, which is owned by the SpaceX Company, has been providing internet connectivity using thousands of satellites in space which communicate with designated ground transceivers. The new service will only stimulate the digital sector if it is reasonably priced and provides fast internet.

Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA) director general Jabiri Bakari confirmed to The Citizen that the Starlink Company had made an application.

The Citizen news paper of Saturday, November 19, 2022 reported “Elon Musk’s satellite internet service Starlink set to be available in Tanzania (Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Tabora & Mwanza) between Jan – April 2023”

With this expectation, SUA and other stakeholders we can get ready to promote widely the digital agriculture to workout with the threat of food shortage in the coming years. There will be 9.7 billion people in the world by 2050. Feeding them will require increasing current food production by up to 98%.

Digital Agriculture can help with the daily management of farms and improve traceability, security and automation. It includes monitoring animals, prescriptive fertilizer programs and geospatial mapping etc. Furthermore, with Digital Agriculture different farm operations can be remotely controlled from mobile phone and dashboard while getting real-time information from elsewhere.

The agricultural industry is one of the sectors that can be positively affected by the digital and technological transformation. The transformation has facilitate the development of new technologies that will improved the accessibility, quality, quantity of agriculture produces.

Digital and technological transformation in agriculture will change the current agriculture production system in the near future. We have to get ready.
Dr. Charles Moses Lyimo
Department of Animal, Aquaculture and Range Sciences
Source : https://www.coa.sua.ac.tz/animal/news/elon-musk-set-an-eye-to-tanzania
 
Sema hawa watu serikalini hawafahamu kuwa internet ya bei rahisi itawazalishia kodi zaidi. Assume kwa sanabu ya internet ya bei chee kitu kama Netflix kiwezekane kwa bongo movies, watu waangalie mipira kwa kustream, muziki wasikilize hivyo nk nk. Ni pesa nyingi na ajira watazalisha kuliko kodi kubwa na kufanya internet iwe ghali.
 
Back
Top Bottom