Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania

Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania

Habari ya 2022… nikajua kibali kimetoka..
CB2C75D1-3001-4346-B91F-65202209A021.jpeg
 
Najiuliza kwa nini kaichagua tanzania? Mleta mada naomba unipe jibu kama unaifahamu sababu.
 
Duh Jamaa mjanja amaa kweli ukiwa na wazo la biashara soko lako walenge maskini wa kipatoo. Ambao ndiyo kundi kubwa.
 
Coudrey ambaye alimshauri Elon kuileta Starlink Afrika Mashariki hususani Tanzania ili Watu wawe na internet ya uhakika ya kuwawezesha kupata taarifa na kuwa na kesho iliyo bora ambapo Elon alinukuliwa akijibu “Tunasubiri kibali kutoka Tanzania”

Kwa upande wa Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye ambaye Watanzania wengi walimtag kwenye tweet hizo ili kupata kauli yake alinukuliwa akisema “Walishajibiwa siku nyingi wana documents wanatakiwa kukamilisha ili mchakato uendelee, hawajakamilisha documents”
 
Kuna uwezekano mkubwa wafanyabiashara wanaoifadhili CCM kwenye chaguzi, hasa makampuni yote makubwa ya mitandao ya simu Tanzania, yakaingilia kati hii issue kwa manufaa yao kibiashara, na washirika wao CCM kisiasa.

Binafsi, sijaona mantiki ya jibu la Nape kwamba kuna documents wanatakiwa kujaza, na hasa nikikumbuka tabia ya watendaji wa CCM kuwasumbua wawekezaji kila siku mpaka wanaamua kuondoka.

Hizo documents Nape anazotaka wajaze inawezekana zina masharti yakijinga ambapo muwekezaji ataona bora apeleke internet kwa viongozi wa nchi wanaojitambua, sisi tuendelee kubaki na ukiritimba wetu.
 
Na mm nilihisi kuna kazibe tuu sehemu ila sikujua ni nani, ila huko kenya na rwanda nako si kuna makampuni makubwa tuu ya simu mbona wamekubali nasikia? Au ndio ukiritimba tuliozoea Tanzania maana mtu kama Elon documents gani hizo zidelay muda wote huo
Hiyo ngoma inaenda kudondokea Kenya au Rwanda, si mnakumbuka hata deal la Volkswagen lilivyosepa mbele ya Macho yetu?
Tanzania huwa wanadhani ukianza mchakato basi tayari umesha win.
Kenya na Rwanda wao huwa hawaamini hivyo, ndiyo maana tunawaona Kenya pamoja na mikataba yote na ujenzi kuanza lakini bado wanalipambania bomba la Mafuta wakiamini kuna lazima tutabugi tu halafu bomba lihamishiwe kwao na lililoanza kujengwa kwetu tubaki kulitumia kupitisha maji kutoka ziwa Victoria
 
Wanaoitaka starlink ije wengi wao hawana uwezo wa kuihudumia. Hiyo ni nzuri kwa watu ambao wako remote areas, hapa mjini hata vodacom kwa 120,000 unapata unlimited 30Mbps
Kama mtu anatumia zaidi ya Elfu 20 kwa mwezi - kwa gharama za intanet tu.
Watashindwa kuungana watu 10 kwa gharama ya Elfu 20 walipie? -Tena ni unlimited
 
Kama mtu anatumia zaidi ya Elfu 20 kwa mwezi - kwa gharama za intanet tu.
Watashindwa kuungana watu 10 kwa gharama ya Elfu 20 walipie? -Tena ni unlimited
1. hao watu yabidi waishi sehemu moja ku share modem

2. waki share internet, surfing speed itagawanywa, kama wapo 10 na wako kwenye data plan ya 50Mbps jua kwamba kila mmoja atadaka 5Mbs kama waki surf kwa mda mmoja, sasa umeruka nini umekanyaga nini
 
Back
Top Bottom