Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania

Mitandao ya simu ipige faida ya internet kwa mara ya mwisho. Elon Musk kuleta internet ya Starlink Tanzania

Sema hawa watu serikalini hawafahamu kuwa internet ya bei rahisi itawazalishia kodi zaidi. Assume kwa sanabu ya internet ya bei chee kitu kama Netflix kiwezekane kwa bongo movies, watu waangalie mipira kwa kustream, muziki wasikilize hivyo nk nk. Ni pesa nyingi na ajira watazalisha kuliko kodi kubwa na kufanya internet iwe ghali.

watu wa kufikiria hayo ndio hawa akina nape[emoji38][emoji38]
 
Sema hawa watu serikalini hawafahamu kuwa internet ya bei rahisi itawazalishia kodi zaidi. Assume kwa sanabu ya internet ya bei chee kitu kama Netflix kiwezekane kwa bongo movies, watu waangalie mipira kwa kustream, muziki wasikilize hivyo nk nk. Ni pesa nyingi na ajira watazalisha kuliko kodi kubwa na kufanya internet iwe ghali.
Ehee hivi unafikiri ccm inawaza maendeleo ya taifa lengo lao la internet kuwa ghali Ni kutaka watu washindwe kutoa free speech na kupata taarifa
 
Kuna mtu kapost vipicha vya starlink nawatahadharisha vimbelembele atalia mtu na kuanza kulaumu serikali ya mama samia
 
Sema hawa watu serikalini hawafahamu kuwa internet ya bei rahisi itawazalishia kodi zaidi. Assume kwa sanabu ya internet ya bei chee kitu kama Netflix kiwezekane kwa bongo movies, watu waangalie mipira kwa kustream, muziki wasikilize hivyo nk nk. Ni pesa nyingi na ajira watazalisha kuliko kodi kubwa na kufanya internet iwe ghali.
Umeongea sahihi
 
TCRA watapiga wapi sasa akija na bundle za bei nafuu?
Itakua sio vibaya Ila hawatomruhusu maana wao wanafanya biashara ili wapige hela, sasa akileta habari za India GB 1 kwa Tshs. 200 ambayo ni sawa na Rupia 7 kwa India atakua ameua soko la bundle,

Kaambiwa huku GB 1 ni 2500 hadi 3000 E Musk kaona huku ndio kwa kutengeneza pesa za kwenda Mars, ngoja niende nikawekeze huku bei ya GB 1 sawa na dollar 1
 
Huwezi kukaa mars week nzima ukatoboa.

Idea zake ni theoretical sana, life in mars.
Eti duniani kuna siku haitakua salama
Jamaa anacheza na akili zetu
Hapo sikubaliani na wewe, kweli ni mawazo ya mbali ila, ni mawazo ambayo inabidi tuanze kuyafikiria. lazma awepo muanzisha gurudumu.

kuna hatari tofauti tofauti ambazo zinafanya kuishi duniani peke yake isiwe mpango mzuri kwa binadamu kama tutaendelea kuishi kwa miaka mingi sana.

Mpaka saahizi wanasayansi wanasema kuna matukio matano makubwa ya upotevu mwingi wa maisha(kwa zaidi ya asilimia 85) wa viumbe hai duniani ambayo tayari yameshatokea, na bado kuna sababu/hatari nyingi ambazo zinafanya watu kama kina musk wanaangalia mbali(mf. super volcanoes, vimondo, mabadiliko ya tabia nchi, vita, n.k.)

Kwa sisi waafrika tuna matatizo mengine yanayohitaji tutatue kwanza ili tuishi saahizi, ila kwa wenzetu waliotembea kidogo kimaendeleo, huko ndo sayansi na teknolojia inadai binadamu tutembee.
 
Boss wa Makampuni ya Marekani ya SpaceX, Tesla na Twitter, Elon Musk (51) ambaye ni miongoni mwa Matajiri wa dunia amesema kilichobaki kwenye mpango wake wa kuuleta mradi wa Starlink nchini Tanzania ni kibali tu kutoka kwenye Serikali ya Tanzania .

Maoni Yangu

Nadhani tumezoea kununua vifurushi vya bando za internet ili tuweze kutumia huduma nzima ya internet nchini kwetu Tanzania, ila suala hilo huwa no tofauti sana kwa nchi za wenzetu ambapo wao huwa wananunua Kasi ya huduma ya internet na wala sio bando

Kama utakuwa tunauziwa kasi ya internet hii itamaanisha utakuwa na limitation katika kasi tu pekee ila kwenye masuala ya bando hutakuwa na kikomo embu tazama kwa mfano

Labda unauziwa internet yenye kasi ya 3.5Mbps sasa hapo kasi yako itakuwa inafikia mpaka hapo na wala hutazidi tena kwenda mbali zaidi na huduma yako itaweza kufika mpaka pale muda wake utakapoishia kama wiki mwezi au mwaka

Tanzania tumekuwa tukiuziwa Huduma hii kwa kununua kiasi cha bando mfano unanunua kiasi cha Megabyte 500 au Gigabyte 1 na kuendelea na huduma yako inakwisha mara tu utakapomaliza kifurushi chako

Kama bwana Elon Musk atakapofanikiwa kuleta satellite zake katika anga letu la Tanzania tutafahidika kwakuwa tutakuwa tunanunua Internet kwa gharama nafuu na yenye kasi kubwa sana inayokidhi na kuendana na pesa unayolipia

[emoji625]Moudyswema
[emoji625]Tanzaniascienceyetu
[emoji625]AstronomyKiswahili
 
Back
Top Bottom