Coudrey ambaye alimshauri Elon kuileta Starlink Afrika Mashariki hususani Tanzania ili Watu wawe na internet ya uhakika ya kuwawezesha kupata taarifa na kuwa na kesho iliyo bora ambapo Elon alinukuliwa akijibu
“Tunasubiri kibali kutoka Tanzania”
Kwa upande wa Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye ambaye Watanzania wengi walimtag kwenye tweet hizo ili kupata kauli yake alinukuliwa akisema “Walishajibiwa siku nyingi wana documents wanatakiwa kukamilisha ili mchakato uendelee, hawajakamilisha documents”