Mizengo Pinda: Tuanze mchakato wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi
Misimamo iliyopitiliza kwenye dunia ya sasa ndiyo mambo ya "Kilongi" chief, siku hizi issues zinaisha kwa mazungumzo na "compromises", Ni mwendo wa kula na kuliwa, wewe ukitaka kula tu basi dunia ya sasa inakutema! Mambo ya akina Fidel castro, Che Guavara, Mugabe hayana nafasi kwenye ulimwengu wa sasa

Kwa hiyo nyie mnaoogomea katiba mpya ya wananchi hamna misimamo iliyopitiliza?
 
Wajunga ndo waliwao, kipindi cha uongozi wake mbona akuwaza ivyo na alikua na cheo kikubwa sana cha kuleta hoja km iyo bungeni pia ktk kipnd chake mchakato wa katiba mpya pamoja na mchakato wa Tume huru ya katiba mpya
 
Kwa nini mnapenda kupinga, kukashfu na kubeza kila kitu, as long as kinatoka upande ambao hamkubaliani nao? Kwa style hii itachukua muda mrefu sana wapinzani kutoboa
Kwaakili hizi ndio maana ccm anawakomesha milele wee unaamini kila porojo zao pole Chadema wako mbele ya muda sana
 
"Kuna mambo ambayo sisi CCM kama chama tawala lazima tubebe dhima. Tutoe uongozi. Kwa, mfano hili la Tume Huru ya Uchaguzi kizuizi ni nini? Hili ni jambo ambalo lazima tukubaliane na wenzetu wa upinzani na tuanze mchakato wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi"

Chanzo: Darmpya
Naipenda tume huru, lakini composition ya Tume ipo kikatiba sasa huyu mamba si aseme wazi kwamba tunahitaji mabadiliko ya Katiba???

Lakini najiuliza, huyu mamba si alikuwa PM wakati tunahangaika kutaka mabadiliko ya Katiba? Waliishia wapi yeye na Mkwere????

Lakini najiuliza zaidi, kwa nini huyu mamba anataka Tume huru wakati huu na sio nyakati nyingine Kuna agenda gani ndani ya chama chao wanameguka au mzee anataka kuunda chama maana huyu aliunga mkono juhudi na akaanza kurudishwa kwenye ramani tofauti na wenzake???

All in all, shamba la bwana Heri, mahindi ya bwana Heri na Nyani wa bwana Heri basi mambo yote ni heri.
 
Huyo mzee Pinda ameona CCM imebaki yenyewe kwenye chaguzi na hakuna wapiga kura tena, hivyo kuficha aibu anataka tume huru ya uchaguzi ili watu waingie hiyo Hadaa, ili washiriki uchaguzi tena. Cha ajabu anaongelea tume huru ya uchaguzi, lakini utakuta wajumbe wa hiyo tume ni hao hao wanaccm!
 
Hili suala la tume huru ya uchaguzi ni suala la msingi sana.

Kilichotokea 2020 hakikuwa na afya kwa nchi yetu ipo siku kutaiangamiza nchi.

2008 kenya waliuana law sababu ya tume ya uchaguzi kufanya upumbavu.

2010 Zimbabwe wakauana kwa sababu ya tume ya uchaguzi kufanya upumbavu.

Ivory coast waliuana kwa sababu ya tume ya uchaguzi.

Tunataka mpaka nini kitokee ndiyo tujue umuhimu wa tume ya uchaguzi.
Kuna fisi hazitakuelewa.
 
Kuna fisi hazitakuelewa.
Uchaguzi wa 2000 Kyle Zanzibar uliondoka na roho za watu.

2020 watu wengi kutokana na uchaguzi walijeruhiwa, kufunguliwa makesi, kuuwawa, na uchaguzi kukosa maana ya uchaguzi.


Tunataka mpaka nani aumizwe na hii hali ndiyo tuone umuhimu wa tume kufanya chaguzi kwa uwazi na uhuru ?
 
Tume huru ya uchaguzi lazima ianze na katiba, uwezi kutunga Sheria iliyo kinyume cha katiba. Mzee Pinda atusaidie yeye hiyo tume huru inaundwaje endapo katiba inabaki ileile?

Je hiyo tume itatokana na wananchi au itatokana na wanasiasa? Nadhani kujadili kuwa na tume huru ni makosa na nimchongo wa TCD kupunguza Kasi ya mambo yanayoendelea Sasa. Tumekwama na tumekuwa watu wakulumbana Kwa miaka Sasa, malumbano yalianza baina ya viongozi lakini Sasa yamekwenda Hadi Kwa wananchi wa chini, hakuna mwenye Imani na mfumo wa kisiasa na hata waliopitishwa na mfumo uliopo wa siasa hakuna mwenye uwezo wakusimama mbele ya wananchi kusema walimchagua.

Hoja ibaki moja TU ya katiba mpya, ndani ya katiba mpya mengine yote yatapata ufumbuzi. TCD waache agenda za michongo, wasimame kuhesabiwa kwa kudai Kati mpya SIYO kuitia Katiba viraka.

Mwisho, wanapojadili Tum huru wajiulize bunge lakupitisha hiyo sheria ya kuunda tume huru ni lipi? Bing la Sasa linaweza kupitisha sheria ya Tume huru? Bunge la chama kimoja lipitishe sheria ya kuunda tume huru.....labda wapewe maelekezo.

Tukitaka tume huru tutengeneze bunge jipya la katiba , la sivyo hata bunge la kubadili sheria Kwa sasa halikidhi vigezo vya mabunge ya kidemokrasia
Hivi alisema hayo kweli?
 
Huwa najiuliza sana watu wanaojiita wacha Mungu,na wanaotuongoza ktk dini zetu wanao unga mkono yafanyikayo na anaeiunda tume isiyo huru,kinyume uhuru ni kukandamizwa,jambo ambalo ni chukizo kwa Mungu wanaedhani wanamjua ama kutufundisha tumjue,sijui huwa wanamaanisha mini ama yamkini tunaodhani wanamjua Mungu ndo hawamjui kabsaaaaa,
Unajiitaje mcha Mungu huku unakubali jambo lisilowaweka watu huru,lisilo huru,
 
Kwa hiyo nyie mnaoogomea katiba mpya ya wananchi hamna misimamo iliyopitiliza?
Wapi tumegomea? Samia kasema changamoto za kiuchumi zinazotokana na Corona zikiisha Katiba itapatikana, ni kitu gani kigumu sana kusubiri? Hata dunia itatushangaa tukianza hekaheka za Katiba kipindi hiki kigumu ambacho dunia inapita
 
Mama Samia kuwa Makini na watu Hawa, Pinda na Kinana usiwasogeze kwenye Uongozi wa Chama, Taarifa kutoka Korido za Lumumba zinasema Ama Kinana ama Pinda kuwa Makamu Mwenyekiti, Jihadhari.
Pinda ameanza kukuchokonoa ili upate pigo la kuonekana hutaki Tume Huru ya Uchaguzi.
Kinana atakupiga na kitu Kizito kichwani, unawajua Wasomali? Vigeugeu.
Watch out.
 
Wala haikukosekana kwa sababu ya kushupaza shingo kwani katiba pendekezwa iliyochakachuliwa na wahuni ipo, na inangoja kura ya maoni. Ila kwakuwa wewe ni bendera fuata upepo ukisikia Ukawa ndio waliokwamisha katiba unarukia humo humo.
Nilikuwepo, ile katiba ilikuwa ni kianzio kizuri! Jambo kubwa lililokataliwa na Kikwete lilikuwa ni Muungano wa serikali 3, lakini mengine karibu yote yalikubaliwa yakiwemo ya kuondoa vyeo vya wakuu wa mikoa, wilaya na kuunda tume huru ya uchaguzi!! Huwezi ukashinda kila kitu
 
Iliwahi kusemwa kuwa ni kheri Pinda akae kimya lakini akipanua mdomo unatapika, Ameanza sasa.
 
Uundwaji wa tume huru ya uchaguzi ianzie chini kabisa kwenye vijiji na mitaa kuja kwenye kata hadi wilayani na baadaye taifa.

Mchakato huu usihusishe kabisa watu wa vyama vya siasa na wachaguliwe moja kwa moja na wananchi na wajumbe wake wawe ni wananchi ambao hawajawahi kujishughulisha kabisa na siasa za vyama.

Mwisho, wajumbe wake kutoka katika kila wilaya ndio wachague uongozi wa tume huru ya uchaguzi ya taifa.

Nje ya hapo itakuwa ni tume huru kwa jina tu lakini kiuhalisia itakuwa ni hii hii ya ccm. Tutakuwa tumetoa gongo kwenye kopo na kuimimina kwenye chupa ya soda na mwisho wa siku itabaki ni gongo ile ile.
 
Tume huru ya uchaguzi lazima ianze na katiba, uwezi kutunga Sheria iliyo kinyume cha katiba. Mzee Pinda atusaidie yeye hiyo tume huru inaundwaje endapo katiba inabaki ileile?

Je hiyo tume itatokana na wananchi au itatokana na wanasiasa? Nadhani kujadili kuwa na tume huru ni makosa na nimchongo wa TCD kupunguza Kasi ya mambo yanayoendelea Sasa. Tumekwama na tumekuwa watu wakulumbana Kwa miaka Sasa, malumbano yalianza baina ya viongozi lakini Sasa yamekwenda Hadi Kwa wananchi wa chini, hakuna mwenye Imani na mfumo wa kisiasa na hata waliopitishwa na mfumo uliopo wa siasa hakuna mwenye uwezo wakusimama mbele ya wananchi kusema walimchagua.

Hoja ibaki moja TU ya katiba mpya, ndani ya katiba mpya mengine yote yatapata ufumbuzi. TCD waache agenda za michongo, wasimame kuhesabiwa kwa kudai Kati mpya SIYO kuitia Katiba viraka.

Mwisho, wanapojadili Tum huru wajiulize bunge lakupitisha hiyo sheria ya kuunda tume huru ni lipi? Bing la Sasa linaweza kupitisha sheria ya Tume huru? Bunge la chama kimoja lipitishe sheria ya kuunda tume huru.....labda wapewe maelekezo.

Tukitaka tume huru tutengeneze bunge jipya la katiba , la sivyo hata bunge la kubadili sheria Kwa sasa halikidhi vigezo vya mabunge ya kidemokrasia
Huwezi kutunga katiba mpya ili uweze kupata tume huru ya uchaguzi.

Kuna masuala mawili:

Ipigwe kura ya maoni kuwataka wananchi waridhie mabadiliko kwenye katiba ili tume huru ya uchaguzi ipatikane kwa mwenyekiti na makamu wake kuteuliwa na raisi na kisha kupitishwa na Bunge.

2. Baada ya hapo ipigwe kura ya maoni kubadili kifungu cha 4(4) kwenye ibara ya 74(7) kinachompa madaraka raisi wa JMT kuteua mkurugenzi wa uchaguzi ambae pia ndie katibu wa tume.

Uteuzi wa mkurugenzi huyo wapaswa kuridhiwa na vyama vyote vya siasa na kisha uteuzi wake kuidhinishwa na Bunge baada ya raisi kufanya uteuzi huo.

Tukumbuke kuwa ni mzee Ali Hassan Mwinyi ndie aleanzisha tume huru ambayo ilikuwa chini ya jaji mstaafu marehemu mzee Francis Nyalali ambae alikuja na mawazo mazuri kabisa ya wananchi kupitia kura ya maoni.

Ni CCM na hayati Mwalimu ndo walopindisha mwaka ule kwa kusema wapinzani hawako tayari na kisha kuwaruhusu CCM kujibadili na kuwa chama dola ili kujilinda na hali kama inotokea leo.

Tukitaka kupata khasa dawa ya kutibu tume huru ni lazima turudi mpaka mwaka 1991 pale mzee Mwinyi alipoteua tume huru ya uchaguzi chini ya marehemu mzee Nyalali ambae alikuja na maoni yaso na shaka kabisa, tusome mapendekezo yale na tuanzie pale.

Madhumuni ya tume ya marehemu Francis Nyalali yalikuwa ni kukusanya maoni juu ya kuendelea kuwa na mfumo wa chama kimoja au kuwa na mfumo wa vyama vingi.

Lakini ilipaswa kuongezwa kipengele kinachohusu maoni juu ya kuwa na tume huru ya uchaguzi au tume iloteuliwa na raisi ambae ni mwenyekiti wa CCM.
 
Back
Top Bottom