Kamugisha naomba kutofautiana na wewe kidogo hoja kwa hoja kama ifuatavyo;
Tume huru ya uchaguzi lazima ianze na katiba, uwezi kutunga Sheria iliyo kinyume cha katiba. Mzee Pinda atusaidie yeye hiyo tume huru inaundwaje endapo katiba inabaki ileile?
Pinda kasema kuwa "...hata TUME UHURU YA UCHAGUZI tatizo ni nini? Tukae (wao CCM) na wenzetu wa vyama vingine tukubaliane...."
Key word hapa ni "Kukubaliana" ambayo obvious ni process. Na process hii ni pamoja na kuangalia sheria yetu mama (katiba), sheria ya uchaguzi na ya tume ya uchaguzi zinavyoweza kupatana kwa pamoja...
This means kuwa "amendments" ya katiba haiepukiki. Na ku - amend kitu si sawa na kuki - overhaul na kukifanya kipya...
Je hiyo tume itatokana na wananchi au itatokana na wanasiasa? Nadhani kujadili kuwa na tume huru ni makosa na nimchongo wa TCD kupunguza Kasi ya mambo yanayoendelea Sasa. Tumekwama na tumekuwa watu wakulumbana Kwa miaka Sasa, malumbano yalianza baina ya viongozi lakini Sasa yamekwenda Hadi Kwa wananchi wa chini, hakuna mwenye Imani na mfumo wa kisiasa na hata waliopitishwa na mfumo uliopo wa siasa hakuna mwenye uwezo wakusimama mbele ya wananchi kusema walimchagua.
Hapana. Tukianza na TUME HURU YA UCHAGUZI is a good step kwenda kwenye KATIBA MPYA. Binafsi sioni tatizo....
Tukumbuke kuwa hawa CCM ni chama cha siasa na lengo lao kama "chama cha siasa" linabaki lilelile la kama vyama vingine, yaani KUONGOZA DOLA..
Wao ndiyo wenye dola sasa. Miaka yote hii, wametumia njia OVU na za HILA kushinda chaguzi na kutusababishia shida hizi tunazopitia sasa...
Sasa kitendo cha kukubali na kuanza kuachia kidogo kidogo baada ya pressure kwa maoni yangu ni hatua nzuri kuelekea kwenye utengamano halisi, na maana yake ni hii, akili njema hao CCM inaanza kuwarudia...!
Hoja ibaki moja TU ya katiba mpya, ndani ya katiba mpya mengine yote yatapata ufumbuzi. TCD waache agenda za michongo, wasimame kuhesabiwa kwa kudai Kati mpya SIYO kuitia Katiba viraka.
Katika siasa Beatrice sometimes ni ngumu kupata yote kwa mpigo. Na kama ukitaka kupata yote at a go, basi you have to pay a big price...
Hebu tukubaliane twende na hili kwanza maana ni zuri kwa kuanzia. Hii haina maana ya kuwa madai ya katiba mpya yatakufa..
Na kumbuka kuwa, ili kuipata NEC mpya HURU pekee kutakwenda sambamba na mabadiliko makubwa ya katiba ili ku - accommodate huo "UHURU WA HIYO TUME.."
Mwisho, wanapojadili Tum huru wajiulize bunge lakupitisha hiyo sheria ya kuunda tume huru ni lipi?
Ndiyo maana ya wito huu wa kukutana na kujadiliana jinsi ya kuipata hiyo NEC guru..
This means that, hayo yatakuwa considered na wote kuamua the right way to go....
Bing la Sasa linaweza kupitisha sheria ya Tume huru? Bunge la chama kimoja lipitishe sheria ya kuunda tume huru.....labda wapewe maelekezo.
Inaweza isiwe kama tutarajiavyo sote. Lakini twendeni kwenye huo wito majadiliano tutaona huko. Kama ni kuwapa "benefit of the doubt ", tutawapa...
Lakini wakumbuke kuwa, kuamua mustakabali wa kiutawala na kiaiasa wa nchi/taifa ni lazima kila mdau ashiriki kwenye maamuzi hayo...
Tukitaka tume huru tutengeneze bunge jipya la katiba , la sivyo hata bunge la kubadili sheria Kwa sasa halikidhi vigezo vya mabunge ya kidemokrasia
"Bunge la katiba" kwa ajili ya NEC huru pekee, ni ngumu. Badala yake tunaweza kutengeneza tume ndogo itakayoshirikisha stake holders wote i.e vyama vya siasa, NGOs, taasisi za dini nk nk wakapendekeza maeneo ya kufanyiwa amendments kwenye katiba na muundo wa NEC HURU yenyewe utakuwaje...
Kama kuna "nia njema" kwenye hili, kila kitu kinawezekana kwa njia ya majadiliano...!!