Mizengo Pinda: Tuanze mchakato wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi
Tume huru ya uchaguzi ni hitaji la muda mrefu kabla hata Magufuli na Samia hawajawa viongozi wakuu hoja yangu ni kwanini kauli hiyo aitoe sasa? Mbona hakuitoa alipokuwa PM au alipokuwa Swahiba wa Magufuli? Huo ndio unafiki ninaouzungumzia.
Una swali la ajabu sana. Ulitaka atoe wakati gani? Kila mtu yuko huru kutoa maoni yake wakati ambao anaona inafaa.
 
Tume huru ya uchaguzi ni hitaji la muda mrefu kabla hata Magufuli na Samia hawajawa viongozi wakuu hoja yangu ni kwanini kauli hiyo aitoe sasa? Mbona hakuitoa alipokuwa PM au alipokuwa Swahiba wa Magufuli? Huo ndio unafiki ninaouzungumzia.

Better late than never.

Kama hoja ya kuwa na tume huru haina mashiko, basi tume isiyo huru mara hii iundwe na upinzani peke yake?

Kwanini kuwa hollow kiwango hiki?
 
Halafu kumbukeni ni Mizengo Pinda peke yake ndani ya CCM aliyewahi kumwambia Magufuli wakiwa Mwanza, kwamba "hata kama tunatamani uongoze kwa muda zaidi au kuongezewa, lakini katiba hairuhusu".
 
Kwanza KATIBA MPYA alafu hayo mengine yatafanyiwa reformation na takwa kuu la katiba mpya.
 
Kwa nini mnapenda kupinga, kukashfu na kubeza kila kitu, as long as kinatoka upande ambao hamkubaliani nao? Kwa style hii itachukua muda mrefu sana wapinzani kutoboa
Tatizo kubwa ni elimu,, kuna watu ambao ni very Uneducated,, yaani advantage yao ni kujua kutype too,, lakini reasoning yao ni absolutely NIL[emoji23][emoji23]
 
Binafsi napenda tupate katiba mpya ila inahitaji mchakato mrefu, tuanze na jambo muhimu ambalo utekelezaji wa kuwa na Tume huru, na iwe huru kweli kweli, muswada wa marekebisho ya katiba unaweza andaliwa na kupelekwa bungeni NOW!
Najiuliza leo hii tumeshashuhudia Mahakama kutokuwa huru, Bunge ndiyo kabisaa, sasa hii Tume ya uchaguzi itatoa wapi kuwa huru bila Katiba mpya?
 
Watu wanaelewa, hii ni danganya toto, badala ya kuongelea katiba uanze kuwashughulisha watu na tume ili waache katiba wakati tume itapatikana ndani ya katiba,
Farao alipoanza kushindwa alitoa ruhusa nusu nusu ila baadae alilazomika kutoa full freedom kwa kuwa Musa alikataa hizo nusu nusu.
Katiba ni long process, na inahitaji bunge liipitie kifungu kwa kifungu, kwani si kwamba hiyo katiba itapitishwa kwa kila mtu aidhinishe,, NO,, Wawakilishi wa wananchi ambao ndo wabunge lazima waipitie katiba fungu moja baada ya jingine,
Pili,, ili katiba itungwe, lazima kanuni ama sheria zitungwe kueleza namna ya kupata bunge la katiba, au kamati ya kuandika katiba, etc,
SASA UPINZANI HAUNA WABUNGE,

hivyo logic inakuelekeza huwezi kupata katiba hadi uwe na tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwezesha kufanya uchaguzi kupata wawakilishi ambao ndo wataanzisha mchakato wa katiba mpya,, LONG PROCESS.

UNLESS labda marekani watuletee katiba iliyoandokwa tayari[emoji23][emoji23]
 
Mawazo yako ya kilongi sana mkuu, sijui hata kwenye maisha kama unafanikiwa kwa kutumia hii policy yako.
Lakini anakwambia kweli, wewe fuso kwa msimamo huo mkiendelea nao, nakuhakikishia utatimiza miaka 90 bado umo JF ukidai katiba mpya,, hell of a waste of your time and energy..
 
Misimamo iliyopitiliza kwenye dunia ya sasa ndiyo mambo ya "Kilongi" chief, siku hizi issues zinaisha kwa mazungumzo na "compromises", Ni mwendo wa kula na kuliwa, wewe ukitaka kula tu basi dunia ya sasa inakutema! Mambo ya akina Fidel castro, Che Guavara, Mugabe hayana nafasi kwenye ulimwengu wa sasa
Acha blah blah nyingi. Tunataka katiba mpya ya nchi yetu.
 
Misimamo iliyopitiliza kwenye dunia ya sasa ndiyo mambo ya "Kilongi" chief, siku hizi issues zinaisha kwa mazungumzo na "compromises", Ni mwendo wa kula na kuliwa, wewe ukitaka kula tu basi dunia ya sasa inakutema! Mambo ya akina Fidel castro, Che Guavara, Mugabe hayana nafasi kwenye ulimwengu wa sasa
Yaani ni GIVE and TAKE..

UKAWA kutoka kwenye bunge la katiba 2014 ilikuwa kosa kubwa mno,, kwasababu tu ya ishu ya serikali mbili au tatu,

Majority wakitaka mfumo wa serikali 2,minority wakitaka 3.

Demokrasia huwa inafuata majority, bila kujali kama majority wanachagua kitu gani,, sasa minority huwa inabidi kukubali tu,, na sio kuzila na kutoka nje, demokrasia ya wapi hii ya minority kutaka kuforce ajenda? [emoji44]
 
Kama ulikuwepo unasemaje hiyo katiba ilishindikana kwa sababu yetu?


Mbona tumenunua ndege kipindi cha Corona, wakati ndege ni bei ghali kuliko katiba mpya? Au hiyo dunia hautushangai tukinunua ndege kipindi hiki cha Corona?
Mkuu vurumai la mchakato wa katiba unalijua, huwezi kufananisha na kwenda kununua ndege
 
CCM si mliendelea na Bunge la Katiba mpya na mkapigisha kura Hadi watu waliokuwa mahututi huko India Ili column ienee!
Na tukabiwa Katiba pendekezwa imepitishwa na kilichobaki ni kupeleka Kwa wananchi ikapigiwe kura!!!

Sasa swali:Kushupaza shingo kulizuia Nini CCM/Serikali kuipeleka Katiba pendekezwa Kwa wananchi ikapigiwe kura???

Acheni ujinga!
Jpm hakuipa priority, hiyo haindoi ukweli kuwa rasimu bado ipo na imebakiza kupigiwa kura ya maoni,
Wazo lenu la kuanza mchakato mpya kwa kupitisha rasimu ya warioba ndo iwe katiba,, SAHAUNI..
 
Kwa nini mnapenda kupinga, kukashfu na kubeza kila kitu, as long as kinatoka upande ambao hamkubaliani nao? Kwa style hii itachukua muda mrefu sana wapinzani kutoboa
Hawa lao ndio liwe, sasa watu wa namna hii ni hatari maana wanataka yao tuu.
 
Tukipata Tume HURU hata tunaweza kuifanyia marekebisho Katiba hihii hii halafu tukaingia kwenye Uchaguzi mkuu.

Huko mbele ndio tutaibadilisha Katiba.
Sawa, lakini swali,, unafanyia marekebisho katiba ukiwa wapi? Si lazima bunge liwepo kupitisha, au?
 
Lakini sisi Wapinzani tukishapata Tume HURU ya Uchaguzi tukaingiza Wabunge wengi baadae tutakuwa na ubavu wa kubadili Katiba.
Sure,, ishu hapa ni kupata wabunge wengi,, bila hivyo hakuna namna mtaweza pitisha katiba mnayoitaka,, hizi mambo hazihitaji nguvu, majority ndio KEY WORD
 
Back
Top Bottom