Mizengo Pinda: Tuanze mchakato wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi
kwani yeye anaongelea tume ipi? ya CCM au tume ya Taifa ya uchaguzi? sasa kama tume ikiwa huru manake yuko tayari kuongozwa na wa upinzani kama hiyo tume ikimtangaza? wamejifunza zambia na kenya kwamba hakuna vita iliyotokea kama walivyokua wanatuaminisha hapo zamani?
 
Misimamo iliyopitiliza kwenye dunia ya sasa ndiyo mambo ya "Kilongi" chief, siku hizi issues zinaisha kwa mazungumzo na "compromises", Ni mwendo wa kula na kuliwa, wewe ukitaka kula tu basi dunia ya sasa inakutema! Mambo ya akina Fidel castro, Che Guavara, Mugabe hayana nafasi kwenye ulimwengu wa sasa

Mbona hujamtaja PUTIN na yule KIM wa NORTH KOREA? Au wao hawako ulimwengu wa sasa?
 
Mbona hujamtaja PUTIN na yule KIM wa NORTH KOREA? Au wao hawako ulimwengu wa sasa?
Putin ndani ya wiki hii kafanya mazungumzo ya muda mrefu sana na Biden and Boris kwa njia ya mtandao, ni maadui wa muda mrefu lakini wanazungumza! Kim alikutana na Trump mara mbili kabla haya mambo ya Covid hayajaibuka, na walikuwa na mwendelezo wa vikao vya muda mrefu! Taliban (Na ubishi wao wote) wamekaa chini na US, na vikao vingine vitafuata, na ni Taliban hao ndio wanaforce hivyo vikao, walijipeleka hadi UN kwa nguvu japo hawakutambuliwa, hiyo yote ni kutafuta muafaka kwa mazungumzo! Dunia ya sasa haina nafasi kwa washupaza shingo
 
Nikikumbuka ya mzee wa msoga kuanzisha ule mchakato then mwishon akabadili gia angani cna hamu kabsa
Hakubadili gia, tatizo lilikuja pale UKAWA walipotaka matakwa yao yote yaingizwe kwenye katiba, likiwemo la serikali tatu ambalo JK alilipinga, UKAWA wakaamua kujitoa and CCM nao wakapata kisingizio cha kutupilia mbali mchakato wote
 
Sawa....Mbowe kidogo ni diplomatic

Ila,in this deal kama wanataka turekebishe katiba twende nayo,then ningekua Mbowe ningewaambia wanipe haya:

1)mikutano ya hadhara bila compromise
2)wafungwa wote wa kisiasa waachiwe bila compromise
3)tume huru ya uchaguzi bila compromise

Katiba tunaweza ipooza mpaka hiyo 2025.

Bila hayo I cant take any other deal.....

Naona wameongelea kupooza katiba tu,sijaona mikutano ya hadhara,wanachosema eti isifanyike kwanza eti warekebishe sheria ya mikutano ya hadhara maana yake itakua haipo,hilo ni changa la macho.

Halafu eti ACT ndio wameweka matako hapo wanakubali hilo deal la hovyo kabisa,hawa jamaa ni bure kabisa yaani!
Hayo yote uliyozungumza yanapatikana kwa mazungumzo, na mazungumzo haina maana kuonana na Samia tu, hata waziri mkuu mnaweza mkakaa naye, mkafikisha mahitaji yenu na yakashughulikiwa! Hii ishu ya CDM kutaka kuonana na Samia tu sidhani kama ina afya sana
 
"Kuna mambo ambayo sisi CCM kama chama tawala lazima tubebe dhima. Tutoe uongozi. Kwa, mfano hili la Tume Huru ya Uchaguzi kizuizi ni nini? Hili ni jambo ambalo lazima tukubaliane na wenzetu wa upinzani na tuanze mchakato wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi" Mzee Mizengo Pinda
View attachment 2047141
Msajili wa vyama na IGP hawawezi kukubali hili.Pinda atapuuzwa
 
Putin ndani ya wiki hii kafanya mazungumzo ya muda mrefu sana na Biden and Boris kwa njia ya mtandao, ni maadui wa muda mrefu lakini wanazungumza! Kim alikutana na Trump mara mbili kabla haya mambo ya Covid hayajaibuka, na walikuwa na mwendelezo wa vikao vya muda mrefu! Taliban (Na ubishi wao wote) wamekaa chini na US, na vikao vingine vitafuata, na ni Taliban hao ndio wanaforce hivyo vikao, walijipeleka hadi UN kwa nguvu japo hawakutambuliwa, hiyo yote ni kutafuta muafaka kwa mazungumzo! Dunia ya sasa haina nafasi kwa washupaza shingo

Mazungumzo ya KIM na TRUMP na pia TRUP na PUTIN yalizaa matunda gani? Badala yake yakamletea uadui na wapiga kura wake wakamtosa kwani waliona kama anawaabudu DICTATORS [ Bending to Dictators] kama ilivyokuwa hulka yake!!! Marekani hawakutoka Afghanistan kwa mazungumzo bali kwa kipigo cha mbwa koko ikabidi wasalimu amri!!!
 
Kwa nini mnapenda kupinga, kukashfu na kubeza kila kitu, as long as kinatoka upande ambao hamkubaliani nao? Kwa style hii itachukua muda mrefu sana wapinzani kutoboa
Ukitaka kuona wapinzani watatoboaje, ruhusu time huru, heshimu sanduku la kura, TISS na Polisi waangalie usalama tu, halafu jibu la watatoboaje utalipata mapema asubuhi.
 
Kwa nini mnapenda kupinga, kukashfu na kubeza kila kitu, as long as kinatoka upande ambao hamkubaliani nao? Kwa style hii itachukua muda mrefu sana wapinzani kutoboa
Haya maneno ya Pinda yamesemwa na Mkapa kwenye kitabu chake, sio mapya.
 
"Kuna mambo ambayo sisi CCM kama chama tawala lazima tubebe dhima. Tutoe uongozi. Kwa, mfano hili la Tume Huru ya Uchaguzi kizuizi ni nini? Hili ni jambo ambalo lazima tukubaliane na wenzetu wa upinzani na tuanze mchakato wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi" Mzee Mizengo Pinda

View attachment 2047118

Hii inatoka moyoni akimaanisha tume huru kweli kweli?! Au ni chezo CCM wanataka kutufanya mazuzu tuingie kwenye 18?

Tumeshuhudia mahakama ikijidhirisha kutokuwa huru, tumeona tume huru ya Jecha wa Jecha ilichofanya kule Zanzibar.

Tumuunge mkono Pinda kwa tahadhari kubwa sana, atazamwe kwa jicho la tatu.
Katiba mpya ni sasa ,may ccm bado wanachukulia biashara as usual,

Mnanunua Ndege kesh, tunashindwa vipi kuwa na kamati shirikishi ndogo na washauri wachache wa Mambo ya kokatiba kutoka nje ya chi,waka kaa na rasm ya warioba na kuja na katiba mpya

Mh Mizengo pinda nakueshim Sana ,ila tulipofika viraka ndani ya katiba hatutaki

Ccm mnawaonaje wenyenchi
 
"Kuna mambo ambayo sisi CCM kama chama tawala lazima tubebe dhima. Tutoe uongozi. Kwa, mfano hili la Tume Huru ya Uchaguzi kizuizi ni nini? Hili ni jambo ambalo lazima tukubaliane na wenzetu wa upinzani na tuanze mchakato wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi" Mzee Mizengo Pinda

View attachment 2047118

Hii inatoka moyoni akimaanisha tume huru kweli kweli?! Au ni chezo CCM wanataka kutufanya mazuzu tuingie kwenye 18?

Tumeshuhudia mahakama ikijidhirisha kutokuwa huru, tumeona tume huru ya Jecha wa Jecha ilichofanya kule Zanzibar.

Tumuunge mkono Pinda kwa tahadhari kubwa sana, atazamwe kwa jicho la tatu.
Hana moral authority ya kuomba Tume huru wakati huu, hata yeye alikuwa PM na alikuwepo wakati tunahangaika na mabadiliko ya Katiba haya yote yangekuwa yalishapita Leo anakuja kuongea kama hajui nini kilitokea mpaka CCM wakahakikisha ule mchakato unaishia njiani???

Pia, ukiweka Tume huru Ina maana CCM wanapigwa mapema sana maana chaguzi zote especially wa kuanzia 2010 CCM walikuwa wanapigwa wazi ukiacha wa 2020 ambao Magufuli aliamua kuwa dikteta wazi kabisa kuhakikisha hakuna mpinzani anapita kwa kutumia mabavu.

Pinda haaminiki nachojua ametumwa wawazubaishe watu, wale pesa za vikao na mtaona kama hayo maazimio yatafanyika.

Wakubaliane tuendelee na mchakato wa Tume ya Warioba kwanza hatutaki Tume huru hiyo ipo kwenye Katiba, the whole point ni kubadili Katiba nzima tuchukue rasimu ya mapendekezo ya Warioba ambayo ilipigiwa kura nchi nzima hiyo ndio tuendelee nayo maana Katiba ya kwelikweli hutoka kwa wananchi wenyewe.
 
Jpm hakuipa priority, hiyo haindoi ukweli kuwa rasimu bado ipo na imebakiza kupigiwa kura ya maoni,
Wazo lenu la kuanza mchakato mpya kwa kupitisha rasimu ya warioba ndo iwe katiba,, SAHAUNI..
Haiitwi Rasimu tena bali katiba pendekezwa!
Sasa hiyo Katiba pendekezwa ni galasa tu,ndio maana mmeogopa kuileta Kwa wananchi maana ingeangukia pua!
 
Back
Top Bottom