Mizengo Pinda: Tuanze mchakato wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi
Kwanza KATIBA MPYA alafu hayo mengine yatafanyiwa reformation na takwa kuu la katiba mpya.

Mawili haya hayahusiani.

Inahitajika tume huru kuipitisha katiba mpya kwa uhuru. Lakini kushughulikia tume huru haisimamishi kushughulikia pia katiba mpya.
 
Kama mzee Pinda anaongea kutoka moyoni na nia ya dhati kwa maslahi mapana ya nchi, namuunga mkono. Ikipatikana tume huru ya uchaguzi na kipengere Cha kuhoji matokeo ya urais jumlisha na mahakama huru, katiba mpya itapatikana.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kama mzee Pinda anaongea kutoka moyoni na nia ya dhati kwa maslahi mapana ya nchi, namuunga mkono. Ikipatikana tume huru ya uchaguzi na kipengere Cha kuhoji matokeo ya urais jumlisha na mahakama huru, katiba mpya itapatikana.
Kwanini huamini anaongea ukweli? Hata kama huamini basi muunge mkono ili umlazimishe ku carry on na kauli yake hii!
 
Historia inaonyesha kuwa watawala hulazumika kwenda kwenye meza ya mazungumzo serious, sizungumzii mazungumzo ya kuzuga ya funika kombe mwanaharamu apite baada ya maafa makubwa, mfano Kenya, Zanzibar, Ethiopia/Eritrea, Sudan, Congo, Burundi etc.

Maswali langu ni je Tanzania ya kisiwa cha amani inashindwaje kumaliza changamoto hizi bila kulazimika kufikia kwenye maafa makubwa? Kwanisni bado kuna janja janja nyingi katika ku handle issues serious? Tunajua ni lini chuki na hasira zilizojaa vifuani mwa watu zitalipuka na kuzaa maafa?
 
Tume huru ya uchaguzi lazima ianze na katiba, uwezi kutunga Sheria iliyo kinyume cha katiba. Mzee Pinda atusaidie yeye hiyo tume huru inaundwaje endapo katiba inabaki ileile?

Je hiyo tume itatokana na wananchi au itatokana na wanasiasa? Nadhani kujadili kuwa na tume huru ni makosa na nimchongo wa TCD kupunguza Kasi ya mambo yanayoendelea Sasa. Tumekwama na tumekuwa watu wakulumbana Kwa miaka Sasa, malumbano yalianza baina ya viongozi lakini Sasa yamekwenda Hadi Kwa wananchi wa chini, hakuna mwenye Imani na mfumo wa kisiasa na hata waliopitishwa na mfumo uliopo wa siasa hakuna mwenye uwezo wakusimama mbele ya wananchi kusema walimchagua.

Hoja ibaki moja TU ya katiba mpya, ndani ya katiba mpya mengine yote yatapata ufumbuzi. TCD waache agenda za michongo, wasimame kuhesabiwa kwa kudai Kati mpya SIYO kuitia Katiba viraka.

Mwisho, wanapojadili Tum huru wajiulize bunge lakupitisha hiyo sheria ya kuunda tume huru ni lipi? Bing la Sasa linaweza kupitisha sheria ya Tume huru? Bunge la chama kimoja lipitishe sheria ya kuunda tume huru.....labda wapewe maelekezo.

Tukitaka tume huru tutengeneze bunge jipya la katiba , la sivyo hata bunge la kubadili sheria Kwa sasa halikidhi vigezo vya mabunge ya kidemokrasia
WAKORA sana Mama.
Lakini hata Bunge la katiba latakiwa NALO lije kuwa huru. BUNGE la katiba latakiwa kuja kuundwa na wajumbe huru watakaotokana na makundi ya kijamii, kiuzalishaji na sio kutujazia TENA 'wawakilishi' wao kutokea Bungezuzu kama ilivyokuwa safari iliyopita.
Ndivyo wenzetu wa Ghana mwishoni mwa miaka ya 90, walivyofanikiwa kupata KATIBA BORA na kuanza upya safari ya kweli ya TAIFA LAO lililokuwa limepotea njia.
 
Tume huru ya Uchaguzi sio kitisho sana kwa CCM

Kama Ccm inaweza kuwa na Wazalendo hadi ndani ya vyama vikuu vyenyewe vya Upinzani ndio itakosa 'Wazalendo' kwny hiyo Tume huru

“Wazalendo”? Wa kazi gani? Tume inanunuliwa tu huku polisi na watendaji wakiendelea kufanya yao kama zamani kwa peanuts.

Bila suala la katiba kuwa resolved hasa kuhusu mamlaka ya Rais na mgawanyo wa madaraka ya mihimili na taasisi, hakuna cha maana.
 
Hatutaki Tume huru bila Katiba mpya

Wengi wanaikosa hii point. Tatizo kubwa kuliko yote ni mamlaka makubwa kupita kiasi ya Rais. Hata kukiwa na “tume huru”, huku kauli ya Rais ndiyo sheria ya nchi ni sawa sawa na bure tu. Bunge, mahakama, vyombo vya dola vyote viko chini ya amri yake.

Rais ana namna ya kuamrisha taasisi zote hata hiyo “tume huru” ifanye anavyotaka. Anaweza hata kutoa maagizo ya kiutendaji au hata kushughulikia baadhi ya member wa hiyo tume kwa visingizio kadhaa. Anaweza kutumia polisi, TISS, Uhamiaji, wakuu wa mikoa, wilaya kubana shughuli za vyama kiasi cha kufifisha advantage ya kuwepo tume huru. Achilia mbali kuwanunua wajumbe. Mshiko wote wa Taifa ni wake. Si bunge wala CAG wanaweza kuhusika na matumizi yake.
 
Watu wanaongea kinaa kutafuta umaarufu miaka yoote serikalini hukuona hilo?
Halafu mbona enzi za maguvanga hamkusema mlimwachia warioba?
saivi ndomnabidua midomo Kuwashwawashwa kumeanza!
 
Back
Top Bottom