Mjadala huru: Kwanini vifo vya Mkapa na Magufuli vilifuatana?

Mjadala huru: Kwanini vifo vya Mkapa na Magufuli vilifuatana?

Wacha weee..kwahiyo mahiga, kijazi, mfugale, kuandikwa nao ni gonjwa hilohilo? Na gonjwa lilipomalizana na hao tu likaisha na kuondoka Tanzania kabisa? Basi gonjwa hatari sana hili doh!
Sasa wewe unataka kusema kitu gani, umesahau kwamba tulikuwa katikati ya janga la COVID-19?

Au kwa vile akili zenu zilipumbazwa na kudhani hilo gonjwa halikuwa hatari sana?

Nenda katafute vipimo vya kitaalam vya hao watu kama hawakuzuia visifanyike uone kama UVIKO haukuhusika katika vifo vyao.

Ninamsikitikia sana Mkapa, lakini asingefanya lolote kuepuka dhahma lililompata. Nampongeza sana Mzee Ruhsa, yeye kwa kudra za Mungu kasavaivu!
 
Kifo humpasa mwanadamu kumfika hilo halina ubishi.

Lakini kwa nini kifo cha Mkapa na Magufuli vilifuatana?!
Ukiua kwa upanga lazima ufe kwa upanga. Magufuli ana mkono kwenye kifo cha Mkapa. Naye akapata dozi yake. Tayari Mkapa alikwisha toa msimamo wake kuzuia kubadili ukomo wa kipindi cha Urais cha vipindi 2 vya miaka mitani mitano. Aliandika kitabu na alinukuliwa mara kwa mara akipinga uchafu wa Magufuli. Hivyo Magu akamtanguliza Ben
 
Ukiua kwa upanga lazima ufe kwa upanga. Magufuli ana mkono kwenye kifo cha Mkapa. Naye akapata dozi yake. Tayari Mkapa alikwisha toa msimamo wake kuzuia maguguli kubadili ukomo wa kipindi cha Urais cha vipindi 2 vya miaka mitani mitano. Aliandika kitabu na alinukuliwa mara kwa mara akipinga uchafu wa Magufuli. Hivyo Magu akamtanguliza Ben
Ooh okeee! Kwahiyo na huyu Magufuli katangulizwa na nani sasa mtaalamu wa mambo?
 
Wacha weee..kwahiyo mahiga, kijazi, mfugale, kuandikwa nao ni gonjwa hilohilo? Na gonjwa lilipomalizana na hao tu likaisha na kuondoka Tanzania kabisa? Basi gonjwa hatari sana hili doh!
Mkuu 'BakiliMuluzi'' hapana shaka yoyote juu ya Mahiga, Kijakazi, Mfugale, na hata huyo Kwandikwa kwamba ni gonjwa hilo hilo.
Unachopaswa kujuwa ni kwamba si COVID-19 inayohusika na watu kufaa ila 'complications' zinazoambatana na magonjwa mengine waliyokuwa nayo hao watu kabla ya kuipata COVID-19.
COVID-19 ni kama inakuja kumalizia kwenye matatizo waliyokuwa nayo mwanzo hao watu.
Nikupe mfano: Philip Mpango asingepona kama angekuwa na gonjwa jingine wakati COVID-19 ilipomshambulia ile mbaya.
Pia fahamu kwamba hao watu wote walikuwa wanakutana kwa ukaribu kabisa bila ya kuchukua tahadhari zozote za kinga kwa sababu tu za ujinga wa Magufuli na waliokuwa wakimshauri juu ya gonjwa hilo.

Mwisho, kama unaouwezo wa kumshawishi Samia, jaribu kufuatilia vipimo vya hao marehemu wote kama hawakuwa na tatizo lolote kiafya na wakati wanakufa hawakuwa na COVID-19. Hizi ni taratibu za kawaida kitaaluma mtu anapoaga dunia, sababu husika iliyosababisha kifo huchunguzwa. Sababu zilizotajwa kwa hawa ni mbali na COVID-19, lakini ni lazima watakuwa wamechunguzwa kama walikuwa na COVID-19 walipoaga dunia kwa sababu hizo zilizotajwa.
 
Deep state ilikuwa inaporwa toka upande huu kwenda kwa wale kule.. Short and Clear.. Ila sijui kama walifanikiwa..??
 
Kifo humpasa mwanadamu kumfika hilo halina ubishi.

Lakini kwa nini kifo cha Mkapa na Magufuli vilifuatana?!
Mungu alipanga hivyo. Kwamba Mkapa aishi miaka 82 na JPM aishi miaka 61 na miezi kama mitano hivi.

Hayo mengine yote ni zile zile imani potofu za kiafrika kwamba kila kifo kina mkono wa mtu.

Ni ushirikina fulani hivi, kama ukifikiria kwa kina.
 
Mkakati ulikuwa ukipangwa kwa mda mrefu jinsi ya kumuondoa kwa kuwa aliingilia viongozi wengi mali zao walizoiba kwenye chama..na serikalini..Lakini pia alitaka wqlioe kodi kwenye biashara zao..Hili liliwauma sana..Ndo maana kila alipotoa maelekezo,,walioelekezwa walifanya mambo ya ovyo ili kumchonganisha na wananchi..mafno mauaji mbalimbali..kwqni haya yalifqnyikq bilq maelekezo yake bali alishitua limetokea.Bqada ya kumchonganisha na wanachi wake,,wakaonq njiq bora ya kumuondoa ilikuwa kiwqondoa watu wake wa karibu..ndo wakaanza na mkapa, wakafuata watu wa karibu yake kama maalimu ..kijazi nk..Baada ya vifo vingi yeye alikaa mda mrefu chato hadi waziri wa nje wa China na Rais wa msumbiji akaja chato.Wakati huo aliishapata taarifa za mipango ya mauaji yake...akatumia watu anao waamini kwenye systwm wakamuaminishq kuwa sasaa kila kitu kikopoa..ndo akarudi..harafu wapangaji wakampangia ziara za morogoro..na dar ili kwenye msafara wamalize kazi na divyo walivyomumaliza..ila nia kagenge kadogo sana akiwemo kiainaainq,ikweta,,manyuzi..etc
Delusional mind from a typical Tanzanian. Kumbuka kuwa JPM na hao wengine walikufa wakati Covid 19 ikiwa imepamba moto.
 
Mkuu 'BakiliMuluzi'' hapana shaka yoyote juu ya Mahiga, Kijakazi, Mfugale, na hata huyo Kwandikwa kwamba ni gonjwa hilo hilo.
Unachopaswa kujuwa ni kwamba si COVID-19 inayohusika na watu kufaa ila 'complications' zinazoambatana na magonjwa mengine waliyokuwa nayo hao watu kabla ya kuipata COVID-19.
COVID-19 ni kama inakuja kumalizia kwenye matatizo waliyokuwa nayo mwanzo hao watu.
Nikupe mfano: Philip Mpango asingepona kama angekuwa na gonjwa jingine wakati COVID-19 ilipomshambulia ile mbaya.
Pia fahamu kwamba hao watu wote walikuwa wanakutana kwa ukaribu kabisa bila ya kuchukua tahadhari zozote za kinga kwa sababu tu za ujinga wa Magufuli na waliokuwa wakimshauri juu ya gonjwa hilo.

Mwisho, kama unaouwezo wa kumshawishi Samia, jaribu kufuatilia vipimo vya hao marehemu wote kama hawakuwa na tatizo lolote kiafya na wakati wanakufa hawakuwa na COVID-19. Hizi ni taratibu za kawaida kitaaluma mtu anapoaga dunia, sababu husika iliyosababisha kifo huchunguzwa. Sababu zilizotajwa kwa hawa ni mbali na COVID-19, lakini ni lazima watakuwa wamechunguzwa kama walikuwa na COVID-19 walipoaga dunia kwa sababu hizo zilizotajwa.
Hata wewe unafahamu moyoni mwako kua ulichoandika hapo ni propaganda tu.
 
Hata wewe unafahamu moyoni mwako kua ulichoandika hapo ni propaganda tu.
Dah!
Sibahatishi mkuu, haya siyo mambo ya kupigia porojo tu bila ya kuwa na uelewa wa hayo mambo.

Kama wewe unataka iwe "porojo" kwa kutokuwa na ufahamu wake, hilo ni swala linalokuhusu wewe, siyo mimi.

Sina sababu yoyote, na wala sifaidiki na kupiga 'propaganda' kama unavyoziita wewe.
 
Nakwambia hivi, kama ulikua hujui ulichoandika ni propaganda ndio mimi nakujulisha sasa. Hiyo corona iue viongozi selectively, tena inner circle tu halafu ipotee ghafla! Mbona wanafamilia wa hawa viongozi waliofariki wasife nao kwa kuambukizwa hiyo corona? Wake zao, watoto zao na ndugu wa karibu ambao ndio wanawauguza kwa karibu iweje wasipate hiyo corona na wao wafe? Unaweza ukaandika propaganda unavyotaka lakini ukweli utakua wazi tu, and very soon.
 
Mbona hunielewi mkuu wangu 'BakiliMuluzi', unataka nieleze vipi ndipo unielewe?

COVID-19 lilikuwa ni gonjwa la mlipuko kwa muda huo lilipoingia, likasambaa kati ya watu na nchi kwa haraka sana.

Wewe hukusikia lilivyosumbua kule ulaya, Marekani na kwingineko na watu maelfu kwa maelfu wakapoteza maisha?
Kwani bado unasikia taarifa za vifo vingi kama ilivyokuwa huko mwanzo gonjwa lilipoingia?

Hili gonjwa lilikuwa gonjwa jipya, halijulikani na wala halikuwa na tiba. Linaenea kwa kasi ya ajabu katika jamii, sisi tukajifanya wajuaji, tukalidharau na kulipa jina la mafua. Tukadharau hata kuchukua tahadhari za kinga lisienee katika jamii kwa kasi.

Sasa unakakazania, mbona sasa halisababishi matatizo kama hapo mwanzo! Ni tabia ya magonjwa ya milipuko, ndivyo yalivyo, na kama ungeelewa kidogo maana ya 'mlipuko' ungeelewa ninachozungumzia hapa. Nikupe mfano wa Cholera; kwani huwa siku zote gonjwa hilo linanguvu wakati wote?

Ni jambo rahisi tu, kama unataka kujuwa hao waliokufa ni nini hasa kilisababisha au kilichangia, uliza kunakohusika kama wakati hao watu wanakufa walikuwa na tatizo la UVIKO. Najuwa hutapewa jibu, lakini jibu lipo.

Siyo kila aliyeugua na gonjwa hilo alikufa. VP yupo hapo anaendelea kudunda, pamoja na kwamba yeye hali ilimuwia mbaya sana kuliko wengi wengine waliowahi kuugua hilo gonjwa. Hao wake au watu wa karibu yao unajuwaje kuwa hawakuuguwa, au ulitaka mpaka walazwe ndipo ujue?
 
Back
Top Bottom