Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Nimeupenda ujumbe wako mkuu. Hata mm msimamo wangu kama wako tu ila harusi za ndugu huwa nachangia kwakweli ila kitchen party sichangi wala send off hata kama ni ndugu
 
Kama nawaona vile walikushambulia kama nyuki
 
Bado hujawekwa ktk loud speaker unaulizwa pledge yako"tuko kikaoni hapa tumekuweka ktk loud speaker, enhe unapledge ngapi"
 
Michango ya Harusi:

jambo hili linachosha sana mathalan kwa miezi hii baada ya Easter unakuta mtu una card zaidi ya tano (mimi binafsi nnazo saba) ,minimum mchango ni TZS 50,000 na unatakiwa kwenda kwenye wedding utatumia extra cost minimum TZS 40,000
 
Mimi hilo jambo ni raisi sana. Nawaambia sina bajeti hiyo kwa sasa, nina majukumu ambayo ni kipaumbele kwangu. Nami nimeshajipanga kisaikologia sitakuja kuomba michango kwa mambo ya sherehe labda kwa familia yangu.
 
KWELI MDAU TUNAPASWATUAMKE TOKA USINGIZINI TUBADILIKE TUEPUKANE KUSHIBISHA FUNZA CHOONI BALI TUANGALIE MABADILIKO YATAKAYO LETA TIJA KWA JAMII SASA NA SIKU ZIJAZO.
 
Ndoa za mwendokasi zimekuwa ni nyingi sana skuizi, vijana wamekuwa wanamuamko wa ajabu kuowa bila kujiandaa mwishowe wanakuja kusumbua watu, Alafu unapewa kadi ya mchango yenye kiwango cha mwisho kabisa cha mchango yaani unaambiwa usitoe chini ya 100,000.

Nimeshawachangia mabest zangu wengi nilisoma nao miaka ya nyuma, nakumbuka nishawachangia mabest zangu kama 40 hivi na kati ya hao 15 ndoa zao zimeshavunjika tena ndani ya mda mfupi tu tokea wafunge ndoa

Na wengine wamekuwa ni matapeli kama yule mzee Kokobanga wa kule Instagram, wanaomba michango ukishawachangia wanaingia mitini na ndoa hamna hela wanakula, ifike mahali sasa kila mtu apambane na hali yake, ukitaka kuowa nenda kanisani au msikitini na mpenzi wako kimya kimya fungeni ndoa yenu na maisha yaendelee, mambo ya michango michango yamekuwa mengi alafu ndoa zenyewe hazidumu mnachezea hela za watu tu
 

Umegonga ikulu mkuu....michango inasumbua sana.....me huwa nikiona hizo text za michango napiga kimya tu maisha yenyewe yako wapi
 

starehe yake yeye sie ndio tugharamikie....upuuzi mtupu. tena anaweka na kiwango kabisa. ukiomba mchango wa ada za shule wanasema oh mbona ulizaa kama ulikuwa hujajiandaa...basi kama nawe unaoa jiandae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…