Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Kuchangia harusi raha lakini, ni kama umbeya flani.
Na kawaida ya waTZ wanapenda umbeya
 
sijatoa hata moja, uwezo wangu ni 50,000 tu, nimpe nani nimwache nani......yangu macho.....

Loh. . .
Nilidhani umeshajitoa 300, 000 kwa hiari alafu unaona uchungu. Wangekua hawawekagi viwango ungewagawia hiyo 50, ila sababu sivyo chagua uliye nae karibu zaidi au uwapotezee wote.
 
Moja ya mambo siyapendi ni harusi.Kwanini iwe hivi?Huu ni uendawazimu!
 
Dah! At last mtu kaileta hii mada, Big up mkuu!
Yani mtu hata hamjuani vizuri anataka mchango- Full kutesana kila mwisho wa mwezi una harusi ya kuchangia. Hata mambo ya maendeleo yanazorota...Yani mi nimeshaamua sichangii hovyohovyo tena
Kwanza harusi zenyewe tunachangia keshokutwa watu wanataka devorce yani kama maigizo vile..
Mtu akiambiwa aolewe ye anawaza harusi tu, ikishapita anaanza kujuta!
 
Huwa tumezoea kuwekeza kwenye matumizi badala ya uwekezaji,
angalia hata Serekali yetu matumizi ya magari na manununzi yake yanashinda
fedha za miradi "tuache kuwekeza kwenye matumizi tuwekeze kwenye uwekezaji"
 
wani ni lazima kuchanga? Mi nachojua kwa upande wangu harusi huchangiwa na watu wa karibu na muoaji for me there is no point ya kuletewa kadi ya kaka mtu tunaefanyanae kazi eti namchangia mdogo wake ambae harusi itafanyikia Katavi wakati mimi naishi Dar. Hata kama tutakuwa tumeshibana vipi nikiamua kutoa natoa kiasi kwa sbb kwanza harusi yenyewe sitahudhuria na pia mimi huyo mtu simfahamu nafahamiana na ndugu yake. Watu wanaochangisha kwa ajili ya ndugu zao mimi nilishaset kiwango si zaidi ya elfu 20
 
mabadiliko yanaanzia na wewe...anza kubadilika wewe wengine watafuata.. hii hali imetokana na mabadiliko ya mila na desturi zetu ila hatujachelewa, mimi wewe na yule tunaweza kuitokomeza tabia hii kwa kuwaelimisha wengine na kukataa kuchangia michango ya mambo ya starehe (wataarifu kabisa watu wako wa karibu ili wasikuletee kadi) na kuwachangia wengine katika mambo yeye maendeleo mfano, kulipia ada ya shule, kjunga nyumba, kuanzisha biashara nk...(wenzetu wakenya wameweza)
 
habari tanzania....huwa najiuliza bila majibu ya uhakika,kuna umuhimu gani wa mtu anaogopa kufunga harusi kisa sherehe ambayo hata ukichangiwa bado inatumika yote kwenye sherehe?nafikiri we have to change tuwe tunachangishana kwenye mambo ya dharura na siyo harusi ambayo unaweza enda kwa kanisa au shekhe na kumaliza hiyo shughuli bila ya kuleta usumbufu kwa watu.nawasilisha

ni kweli
 
dah......
Umenitonesha kidonda.....
Mfanyakazi mwenzangu kaka yake anaoa..50,000
mfanyakazi mwenzangu anaolewa 50,000
kuna harusi 2 kwenye kikundi chetu 100,000
binamu zangu 2 wanaoa na kuolewa 100,000

khaaaaa......!!!!!

Ukijumlisha huo mpango unapata mtaji wa duka....
 
sijatoa hata moja, uwezo wangu ni 50,000 tu, nimpe nani nimwache nani......yangu macho.....

Heri lawama kuliko fedheha! Ukatoe 300,000 ubaki unapiga miayo? Huo mshahara unalipwa sh.ngapi?
Siku hizi hata kamati watu wamezishtukia, hapa mbeya kima cha chini mwanakamati 50,000 hadi kufikia 100,000! Wengine,wanakuwa katika zaidi ya moja. Huko si ni kutafuta sifa kama mshumaa? Unamulikia wengine, lakini hatima ya huo mshumaa ni nini?
 
habari tanzania....huwa najiuliza bila majibu ya uhakika,kuna umuhimu gani wa mtu anaogopa kufunga harusi kisa sherehe ambayo hata ukichangiwa bado inatumika yote kwenye sherehe?nafikiri we have to change tuwe tunachangishana kwenye mambo ya dharura na siyo harusi ambayo unaweza enda kwa kanisa au shekhe na kumaliza hiyo shughuli bila ya kuleta usumbufu kwa watu.nawasilisha

HAO WAKINA DADA NDIO TATIZO BILA HARUSI PANAKUA HAPATOSI KISA ANATAKA AMZIDI MWENZAKE !!! YAN WAMEKAA KIMASHINDANO TU...
sIKU HIZI MICHANGO IMEKUA KERO YAN TUNALAZIMISHANA NA USIPOTOA NI UGOMVI.
SERIKALI HAINA KIPAUMBELE NAA RAIA PIA HAWANA KIPAAUMBELE KAMA TUTAENDELEA KUENDEKEZA MICHANGO YA KIPUUZI.
 
Heri lawama kuliko fedheha! Ukatoe 300,000 ubaki unapiga miayo? Huo mshahara unalipwa sh.ngapi?
Siku hizi hata kamati watu wamezishtukia, hapa mbeya kima cha chini mwanakamati 50,000 hadi kufikia 100,000! Wengine,wanakuwa katika zaidi ya moja. Huko si ni kutafuta sifa kama mshumaa? Unamulikia wengine, lakini hatima ya huo mshumaa ni nini?

unaungua loh.........
Kwanza hizi kamati hizi kamati hizi........
Muhusika asipokuwa makini tu wanamchakachua hahaah......loh.....
 
unaungua loh.........
Kwanza hizi kamati hizi kamati hizi........
Muhusika asipokuwa makini tu wanamchakachua hahaah......loh.....

Haswaaa! Ndio maana wengine wanazing'ang'ania hata akichanga anawekeza anajua zitarudi na cha juu!
 
Jamani eeh, hivi vitu ni wewe utavyoguswa, uwezo wako, na ukaribu wako na muhusika, sizani kama kuna mtu atakulazimisha kuchanga kama hautaki, muhimu ni kutochangia watu usio wa jua but mtu mlieshibana na washkaji wa ukweli unamchangia hata gharama ya kukodi cleopatra quality centre kama uchumi unakuruhusu, but kama huna unamwambia sina na imani atakuelewa kama mmeshibana na urafiki utaendelea,
 
Back
Top Bottom