Mjadala kuhusu chanzo cha ulimwengu na maisha

Mjadala kuhusu chanzo cha ulimwengu na maisha

Imekuwepo mijadala mingi ya aina hii hapa JF,Kwa hiyo lengo la uzi huu ni kujadili hoja zitakazoletwa bila jazba na hivyo kupanua uwezo wa kujenga hoja.kuna makundi makubwa mawili duniani yaani wanaoamini uwepo wa Mungu(Theism) na imani ya kutokuwepo Mungu au uungu yaani (Atheism) Wote hawa wanakubaliana kuwa ulimwengu upo,hoja ya kwamba ulimwengu una chanzo au hauna umegawanya watu katika makundi matatu makuu hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na David Foster Wallace na ninayaainisha kama ifuatavyo:

1.Kundi la kwanza linaamini ulimwengu umekuwepo na hauna chanzo chake yaani The universe has always existed and it has infinite past.

2.Kundi la pili hapa kuna wanasayansi wengi sana wanaamini kwamba ulimwengu ulitokea kutokana na mlipuko ambao haukusababishwa na kitu chochote yaani The universe was popped into existence from nothing with absolutely no cause rejea bigbang theory

3.Kundi la tatu linaamini kwamba ulimwengu ulisababishwa kuwepo na nguvu au kitu nje yake yaani The universe was caused to exist by something outside it.

Hapa ndio mwanzo wa kila ubishi uliopo kuhusu chanzo hivyo Great thinker unaamini kundi lipi liko sahihi?

Mimi na Theist wote tuko kundi namba tatu ,kundi la kwanza halina mashiko kwa sababu utafiti wa kisayansi uliofanyika mwanzoni mwa miaka ya 1960 ulionyesha kwamba kwa namna yoyote ile ulimwengu una chanzo chake,hivyo hoja kuwa umekuwepo haina mashiko.

Kuhusiana na atheist waliobaki wa kundi namba mbili kiranga sijajua uko 1 au 2 ?Hoja ya kwaamba ulimwengu una chanzo chake nakubaliana nalo lakini hoja kwamba "it popped into existence from nothing with absolutely,no cause"hainiingii akilini,ukiangalia ulimwengu huu ambao unajiendesha kwa namna ya kustaajabisha kuna "costants" nyingi sana na zingine zinazidi kugunduliwa na hazibaliliki hii inadhihirisha kwamba kulikuwa na being that caused that existence hata mtaalamu wa sayansi bwana Albert Einstain aliwahi kusema 'Every scientist becomes convinced that the law of nature manifest the existence ofa spirit.Vastly superior to that of man"
na alipoulizwa kuhusu kuwa atheist Einstein alisema 'I am not atheist and i don't think i can call myself an atheist;

HITIMISHO Hivyo mtu yoyote ana haki ya kuamini anachoona kinamfaa na mnisamehe kwa uandishi na makosa ya kiuandishi na pia kila mtu ajitokeze kutetea anachoamini na kujibiana kiustaarabu inaonyesha jinsi gani tumestaarabika.Naungana na Einstein na viongozi wa dini kuwa kundi la tatu.


Hiyo nguvu ya nje ilitoka wapi kaka ? Na kipi kimejulisha kulikuwepo na nguvu ya nje ?
 
Chukulia Dunia ndio jf, kisa wengine hatumfahamu Mr Melo ndio tuseme ilijiunda??? No. Dunia imeumbwa na Mjuuzi aliyeumba ujuuzi kwa ujuuzi wenye ujuuzi katika ujuuzi wote wenye ujuuzi wa hali isiyo na kikomo.
 
Mungu awepo au hasiwepo... tatizo linabaki kuwa moja tu.

Kusema kwamba Mungu huyo katutaka tufanye mambo kadhaa.... na hapa ndio kwenye shida na utata. Ukichunguza kwa kina utaona mambo hayo ni yenye kupingana, dini zimekuwa nyingi....

Ukitaka kuona ukakasi wa kundi la 3 ni kwamba lina watu wenye mitazamo tofauti kumuhusu huyo Mungu...lina watu wa makundi mbali mbali wenye maarifa ya hali ya juu na wasio na maarifa kabisa.

Hivi wakristo na wenye imani nyingine mnajua kwamba Mungu wa waislamu hawatambui.... na kishasema anaenda kuwachoma moto kwa kukufuru kwenu......

Waislamu mnajua kwamba bila kupitia kwa Yesu hamtamuona baba yake.....?????

Kinachotakiwa kujadiliwa sio Mungu yupo au hayupo bali ni huyo Mungu anataka tufanye nini baada ya kuamini yupo..... je, tunajifanyia tu au tunafuata mwongozo wa nani?????

Changamoto iliyopo ni kwamba tufuate mwongozo wa nani hautokani na how intelligent we are.... kwasababu pande zote zina watu wabobezi.

Hivyo huwa inanifanya nifikie conclusion kwamba hata kama Mungu yupo basi hausiani na vitendo vyetu..... its nature that decides our destiny... (nature inajumlisha na matendo yetu)....

Mwizi anapokuibia kwako is bad, kwake is good..... so tuendelee kupamabana ili ku-survive.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The universe popped into existance from nothing (big bang theory ) very funny !! May be the term nothing is the supreme being .. What is nothing of nothingness ? There must be the first cause ! May be after death the soul will be able to see . Don't struggle for the first cause while you are still alive ! Just study what you are able to see and touch

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi wengine tunaamini katika chanzo fulanj(Muumba)

Na hicho kitabu hatukubaliani nacho kuwa ni cha Muumba

Na sio hicho tu na vyenzake vyote vilivyotangulia

Ila tunakubali kuwa ni cha miungu

Na kina kila sababu yakuwa kitabu cha Alien wanaotaka kutuingiza chaka

Na kinawafanya watu kuwa kondoo na wao kuwa wachungaji

kinatoa majibu Mepesiiiii..kwa maswali magumuuu

kwa shutuma hizi na zenginezo naomba usitumie nukuu zake huku

utachenji gia ya mjadala Angani sasa hivi
Tutumie nukuu ya kitabu au vitabu vipi basi ili tuwe ndani ya mada husika?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitendo hiki cha akili ya mwanadamu kusumbuliwa na mawazo na uwepo wa MUNGU ni.ushuuda tosha kuwa MUNGU yupo..
Kwa hali ya kawaida akili ya mwanadamu haiwezi kusumbuka kuwaza au kutafuta majibu ya kitu ambacho hakipo..
 
Kama kila kitu kimetokea kwa bahati mbaya/accidentally/Nature kama wanavyoita wao . THEN MBONA HAIKOKEI SIMBA.Tembo. Twiga au ngamia wakachati kwa kutumia smart phone kama binadamu..

Nini kimetokea hadi hiyo Nature akabagua viumbe wengine wote na kumpatia ufahamu binadamu kuendesha hii Dunia..
Kama ni hivyo basi hii Nature inaubaguzi sana kudharau viumbe wengine wote na kumpenda zaidi binadamu..
Na kama nature inaubaguzi kiasi hiki nani kaifundisha hiyo sellection ya kuacha Fisi na mamba asiwape.akili kama binadamu..

Mbona Ngamia hajui kusoma na kuandika ..

Nani kampendelea binadamu kujua yote hayo na viumbe wengine wasijue..
 
Siku ikitokea Sokwe na.Nyati wakatengeza TV zao ndio nitaamini Nature is everything otherwise kuna Nguvu inapanga haya maisha yote na nguvu hiyo ni MUNGU tu
 
Tuanzie hapa kwenye "logic"

We we unataka logic ya namna gani.au mpakaa mpate maneno ya watu weupe ndy mnayaamini Unajua msipinge tu vitabu vingine bila kuchunguza kwa undani..


Lazma uzame ndani ya hivyo vitabu uchimbue ujue kinachosemwa sio kukurupuka tu na kutoa hitimisho.
Hicho ktabu kimeja uongo mwingi... Vry shame kuktumia kama rejea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana mimi nimesema kwa mtazamo wangu tu. Wapo wengine watakuja kwa mitazamo yao na Mimi siwezi kuwaingilia sababu ni misimamo yao tayari.

Masala haya huwa hayalazimishwi ni kitendo cha kumfikishia mtu mwenyewe akiona ni sawa basi na afuate. Kinachomata ni je? Kile kilicho Elezwa ni sahihi kusudio ni kuwa kina make sense. Je? Kinapimika na kipo logic ?

Sio mtu unakuja na ushahidi ambao ukiuangalia ata wewe mwenyewe utakuta kuna mapungufu. Swala sio Ku judge kitabu Bali ni Ku judge kile kilichoandikwa ndani. Apo ndiyo utajua kuwa ni sahihi au sio sahihi in hayo tu mkuu.
Sawa ngoja tuheshimu mtazamo wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Allah ndio kila kitu
Mlokore nae atakuambia yehova ndiye alie juu ya vyote.
yaan kila dini ina mungu wake.Huyo allah kashindwa kuthibiti mauaji ya vitoto vichanga uku syria,somalia na kule burma..
antbaraka wanaua waislam kule afrka ya kat, kule misri nako wakristo wanachinjwa kama kuku alaf uniambie kuna mungu mweza wa yote?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom