y
oote uliyosema ni ukweli,lakini tatizo wanawake wa leowanataka wawapande waume zao kichwani!!!!,,,,,dunia ya leo sio ya jana!!!!!,,,wewe unaenda kazini na mkeo anaenda kazini watoto wanalelewa na house girl sasa ndoa ya nini,manake mama akae na watoto mwanzo mwisho asimamie mifugo ya familia na miradi ya familia iliyo karibu na nyumbani au hapo nyumbani{wachagga wanatumia sana huu mfumo] sasa wewe unaenda job,nae anajipodoa anaenda kazini kwake nahuko anakutana na wajanja wanamyandua mpaka akili ichanganyikiwa na kumwona mumewe boya na hapo tatizo linaanza
 
Habari wakuu

Jambo lolote zuri hupambaniwa(earned)...kuna sadaka kulipata.Watu wanaoshindwa kutoa sadaka kupata jambo zuri,huwa na tabia ya kuwaaminisha kuwa jambo hilo ni gumu haliwezekani na kubaki katika Hali ya kushindwa ndio mazingira sahihi...utawasikia watu wenye ufukara wa kujitakia wakisema ...uwe na Mali usiwe nayo utakufa tuu...au hakuna utajiri halali na blah blah

Wakati mwingine wale walioshindwa masomo ya sayansi au hisabati nao wangekuja na hoja zao ooh kwanza siasa ndo kila kitu nk

Nirudi katika ndoa...ndoa msingi wake ni jambo linalohitaji uadilifu wa half ya juu na kuaminiana,hali hii inahitaji kumshirikisha Mungu kwa sababu yote haya kuwezekana inahitajika IMANI...mfano unajua A Ana mapungufu haya lakini B nitadumu nae kama mume /mke baba/mama wa watoto wangu

Wengi hasa vijana hawawezi kujidhibiti miili kwa tamaa mbaya,starehe na anasa...anataka alale na kila mtu...ale hovyo hovyo na kunywa kwa sababu tuu Ana pesa,anajiona yuko huru lakini kwa kweli hayuko huru,ndio maana baadae hali kama addiction zinatuumbua...mfano wa mtu alie huru...akikuta hot pot limejaa nyama akiambiwa ajipakulie,atachukua finyango chache tuu!sio kwa sababu nyama ni tamu basi apakue zote

Silika hiyo ndio inatutofautisha na wanyama...mnyama akishikwa na ashki,anampanda yeyote na popote....anaweza mpanda hata mama yake au dada yake...ndio sifa ya kijana ambaye hawezi kuhimili hisia na mwenendo wake,ni kama mnyama ...huyu hafai wala ndoa haiwezi...atafanya harusi baadae atakwambia ndoa haifai

Msichana au dada anaeingia kwenye ndoa kama fursa ya kutoboa maisha,akikutana na changamoto ndogo ndogo za maisha ,atakwambia hayo hayo

Watu hawa kwa sababu wanadaiwa uadilifu,kumcha Mungu ...mambo ambayo sio rahisi yanahitaji kujisadaka mpaka kuyazoea kama mfumo wa maisha wa kawaida wa mtu...nao hawako tayari kuyafanya...mfano...kwenda kanisani/msikitini,kufunga kwaresma au Ramadan nk...kusaidia wengine...watakwambia ndoa ni ngumu

Hii haindoi ukweli kuwa wakati mwingine watu wamejikuta katika matatizo makubwa kwenye ndoa,lakini ni mara chache sana,ndio kusema gari kwa sababu zinapata ajali kila siku na kugharimu maisha ya watu...ndio tufanye safari zetu kwa mguu...kutoka Dar es Salaam hadi Njombe....au Kigoma?

Msingi wa jamii yoyote njema ni familia ya baba na mama,ndoa ndio taasisi bora kutupa haya...NDOA NI JAMBO JEMA LIMETOKA KWA MUNGU MWENYEWE NA LIHESHIMIWE NA KILA MTU
 
Kweli ndoa ni jambo jema, ila kwa kizazi hiki tunachoishi sasa Mungu aturehemu tu.
 
Ndoa na mahusiano ya kimapenzi ya muda mrefu ni maigizo tu.
 
Reactions: M45
Wale vijana waliozaliwa na michepuko a.k.a wale wa kataa ndoa watakuja muda sio mrefu kukukashifu.
 
Ndoa ni jambo jema sana, wanadamu kusaidiana ... Inshallah Mungu atuwezeshe tupate wenza maana umri umeenda sana.
 
Tatizo la ndoa lilianzia pale mkutano wa beiging ulipofanyika haki sawa ...zikimpendelea mwanamke..mf kugawqna Mali linapotokea mmeachana hata akisababisha yeye mgawane..upendo kugeuka fedha na maisha Bora...wimbi la wanawake kutegemea mwenza badala ya kijishughulisha...wanawake kutegemea child support ...mkiachana anapewa jukumu la kibali na watoto...wanawake wanainchi kwenye ndoa wakifocus kuwa mwanaume atakufa mapema na la sivyo wanafocus kwenye retirement plan akiona Ana watoto na wewe huna Cha kumuachia au faidi kumshinda anakuacha na kuondoka na watoto inabaki mpweke na kujifia...ndoa NI nzuri ukibahatisha NI swa na bet ukila unaisifu Ila wengi wanatumia umizwa ..asilimia kubwa ndoa zinawaumiza lakini wamo tu...
 
Mna miaka mingapi ya ndoa na shemeji/wifi yetu?
 
Mwanamke kama utii na heshima kwako ni msamiati sababu ya malezi usiingie kwenye ndoa
 
Kweli ndoa ni jambo jema, ila kwa kizazi hiki tunachoishi sasa Mungu aturehemu tu.
Kila kizazi huwa na changamoto...lakini familia ndio sehemu sahihi ya kuzishinda changamoto...pamoja na kubebeana mapungufu ya kibinadamu,tunaunganisha nguvu kushinda changamoto...NDOA ni msingi wa familia thabiti
 
Mungu ni mwema atusaidie
Biblia yenyewe inasema bora usioe/kuolewa ila sababu ya tamaa za ngono uwe na mke/mume wako mwenyewe
ni kana kwamba ndoa sio jambo zuri ni vile tu kuna genye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…