Hahaa mkuu naona umetapika ile mbaya. Umezungumza vema sana. Mwenye masikio na asikie.

Nashukuru kwa mchango huu maridhawa kabisa.
 
Ibrahimu na Suleiman waliyafanya hayo sana still Mungu aliwapenda
 
Ibrahimu na Suleiman waliyafanya hayo sana still Mungu aliwapenda
Siyo kweli. Labda kama una Biblia yako mwenyewe.

Ibrahimu alipata kibali kutoka kwa mke wake kufanya alichokifanya (kuzaa na Hajiri). Lakini pia, hadithi ya Ibrahimu ulikuwa ni mpango wa Mungu.

Suleimani alikufa kifo cha kupotea (yaani hakwenda peponi), soma 1Wafalme sura ya 11 kuanzia mstari wa 1 na kuendelea.
 
Hii ni kama uamuzi wa mtu kuamua ajiunge na chama gani, ccm watapika pilau chadema watasema tuandamane nawe amua vile akili yako itakushauri

Kibali chenye uhalisia ni pale unatupa ndoana yenye chambo akanasa ...hivyo vibali vya kukusanyia sadaka ni uhuni mwingine
 
Sawa.
 

Best comment ever

#YNWA
 
KATAAA NDOA NDOA NI UTAPELI
 
Hii mada ya kuoa na kutooa inatrend sana aseeee πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ikifuatiwa na mada za walimu humu ndani.
Turudi kwenye uhalisia anayeona Ndoa inamfaa aende akafurahie maisha !! Anayekataa pia ana sababu zake !
Zamani mara nyingi tulifanya vitu kwa ushawishi wa watu waliotutangulia (wakubwa) ndo maana kulikua na age fulani msichana au mvulana ukifikisha huna mtoto au hujaolewa ilikua inakutatiza sana !! Kwa hiyo wengi waliingia kwenye ndoa kwa mtego huo !! Kwa sasa vijana wengi wamejikita katika kutafuta pesa sana , na tamaa ya mali inakua kubwa kila kukicha sio kwa wanaume hata wanawake pia vigezo ni vingi ! Pia sherehe kubwa kubwa za kusimamisha mtaa.

Pia msiwalaumu kuna Childhood trauma mtoto aliyezaliwa kwenye familia yenye migogoro ya ndoa anaona mama anavyopigwa ,anasikia habari mtaani kwamba Mama alimuua Baba amiliki vitu , anaona dharau anazofanyiwa Baba na mama huyu mtu Ndoa kwake ni kipengele ni ngumu sana hizi trauma za utoto hawazisemi au hawazitambui ila zinawatafuna watachagua sababu nyingine za kutumia kuikataa ndoa ila ukweli unakua moyoni ,Binti amelelewa bila baba , kijana amelelewa na watu tofauti tofauti leo yuko kwa mjomba kesho kwa Babu keshokutwa yuko kwa jirani humwambii habari za ndoa. Mtoto aliyelelewa na mama wa kambo mkorofi anajua ndoa ni kifungo pia

Mwisho mimi nawasupport wanaokataa ndoa kwa hiyari yao , inasaidia pia walio tayari kupata wenzi sahihi kwa sababu walio wengi hawapendeki utajituma vya kutosha umwoneshe mahaba yote lakini yeye hajali kwa baadhi yao ! Wengi ni Sadist .
Inapunguza na vifo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ No string attached
 
Mkuu ukristo ndivyo unavyo sema hivi ?

Una wafahamu hawa watu katika ukristo ?i, Yesu
ii, Paulo
iii, Padre
iv, Watawa
v, Waseja

Karibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…