Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Kama wewe binafsi umeona CHANGAMOTO ZA NDOA zinakwepwa kwa kutokuoa...basi BAKI HIVYO HIVYO NA UFUSKA WAKO USIOE...

Sio kutwa kushinda kusambaza kampeni ya KISHETANI usioe...eti kisa ndoa ina changamoto nyingi...

Mkimaliza kukimbia changamoto za ndoa kwa wanawake...mtakuja kupiga kampeni juu ya CHANGAMOTO ZA MAMA ZENU...kwa sababu nao ni wanawake...

Kwanza MWANAUME RIJALI KAMILI HAKIMBII CHANGAMOTO...ANAZIKABILI...ANAPAMBANA NAZO...

Isije kuwa nyie mnaopiga kampeni watu wasioe...ni AGENTS WA USHOGA...Kwahiyo kwenye suala la kuoa mnatumia kama njia tu foreplay...ili mfikie malengo yenu ya kusambaza ushoga...

Kwa sababu usipotaka kuishi na mwanamke...basi unataka kuishi na MWANAUME MWENZIO...

Hakuna kuishi mwenyewe...anayeishi mwenyewe ni MAITI TU KABURINI...

MASHEYTWAANI WAKUBWA NINYI...
Hahaa mkuu naona umetapika ile mbaya. Umezungumza vema sana. Mwenye masikio na asikie.

Nashukuru kwa mchango huu maridhawa kabisa.
 
Sikatai kwamba tunaweza tukaziliana bila ndoa, lakini huu ni uzinzi ambao ni dhambi machoni pa Mungu, na watoto ambao ni zao la uzinzi ni chukizo kwa Mungu. Soma 1Wakorintho 7:1-2, neno la Mungu linasema, "...heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwasababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe" (mume au mke anayezungumziwa hapa ni yule wa ndoa).
Ibrahimu na Suleiman waliyafanya hayo sana still Mungu aliwapenda
 
Ibrahimu na Suleiman waliyafanya hayo sana still Mungu aliwapenda
Siyo kweli. Labda kama una Biblia yako mwenyewe.

Ibrahimu alipata kibali kutoka kwa mke wake kufanya alichokifanya (kuzaa na Hajiri). Lakini pia, hadithi ya Ibrahimu ulikuwa ni mpango wa Mungu.

Suleimani alikufa kifo cha kupotea (yaani hakwenda peponi), soma 1Wafalme sura ya 11 kuanzia mstari wa 1 na kuendelea.
 
Ukisoma Mithali 18:22 neno linasema, "Apataye mke apata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Bwana".

Kibali ni nini? Kibali ni hali ya kukubalika katika jambo/kitu fulani. Kumbe ukioa unapata kibali kutoka kwa Mungu, hii ina maana hakuna jambo/kitu ambacho utatia mkono wako kisifanikiwe.
Hii ni kama uamuzi wa mtu kuamua ajiunge na chama gani, ccm watapika pilau chadema watasema tuandamane nawe amua vile akili yako itakushauri

Kibali chenye uhalisia ni pale unatupa ndoana yenye chambo akanasa ...hivyo vibali vya kukusanyia sadaka ni uhuni mwingine
 
Sawa.
 
Hujajibu hoja ZAO!!!

Umetoa maoni!!

Waambie KWANINI ndoa siyo utapeli kea wanaume!!?

Waambie kwanini wasiogope kugeukwa na wake zao wapatapo mali NYINGI!?

Waonyeshe pia na takwimu ya wanawake waliofiwa na waume zao na kuachiwa mali NYINGI na wanamiliki kwamba ni za Uongo na vice versa ni true!

Waambie ili kuwatoa wasiwasi!!

Best comment ever

#YNWA
 
Kama wewe binafsi umeona CHANGAMOTO ZA NDOA zinakwepwa kwa kutokuoa...basi BAKI HIVYO HIVYO NA UFUSKA WAKO USIOE...

Sio kutwa kushinda kusambaza kampeni ya KISHETANI usioe...eti kisa ndoa ina changamoto nyingi...

Mkimaliza kukimbia changamoto za ndoa kwa wanawake...mtakuja kupiga kampeni juu ya CHANGAMOTO ZA MAMA ZENU...kwa sababu nao ni wanawake...

Kwanza MWANAUME RIJALI KAMILI HAKIMBII CHANGAMOTO...ANAZIKABILI...ANAPAMBANA NAZO...

Isije kuwa nyie mnaopiga kampeni watu wasioe...ni AGENTS WA USHOGA...Kwahiyo kwenye suala la kuoa mnatumia kama njia tu foreplay...ili mfikie malengo yenu ya kusambaza ushoga...

Kwa sababu usipotaka kuishi na mwanamke...basi unataka kuishi na MWANAUME MWENZIO...

Hakuna kuishi mwenyewe...anayeishi mwenyewe ni MAITI TU KABURINI...

MASHEYTWAANI WAKUBWA NINYI...
KATAAA NDOA NDOA NI UTAPELI
 
Hii mada ya kuoa na kutooa inatrend sana aseeee 😂😂😂 ikifuatiwa na mada za walimu humu ndani.
Turudi kwenye uhalisia anayeona Ndoa inamfaa aende akafurahie maisha !! Anayekataa pia ana sababu zake !
Zamani mara nyingi tulifanya vitu kwa ushawishi wa watu waliotutangulia (wakubwa) ndo maana kulikua na age fulani msichana au mvulana ukifikisha huna mtoto au hujaolewa ilikua inakutatiza sana !! Kwa hiyo wengi waliingia kwenye ndoa kwa mtego huo !! Kwa sasa vijana wengi wamejikita katika kutafuta pesa sana , na tamaa ya mali inakua kubwa kila kukicha sio kwa wanaume hata wanawake pia vigezo ni vingi ! Pia sherehe kubwa kubwa za kusimamisha mtaa.

Pia msiwalaumu kuna Childhood trauma mtoto aliyezaliwa kwenye familia yenye migogoro ya ndoa anaona mama anavyopigwa ,anasikia habari mtaani kwamba Mama alimuua Baba amiliki vitu , anaona dharau anazofanyiwa Baba na mama huyu mtu Ndoa kwake ni kipengele ni ngumu sana hizi trauma za utoto hawazisemi au hawazitambui ila zinawatafuna watachagua sababu nyingine za kutumia kuikataa ndoa ila ukweli unakua moyoni ,Binti amelelewa bila baba , kijana amelelewa na watu tofauti tofauti leo yuko kwa mjomba kesho kwa Babu keshokutwa yuko kwa jirani humwambii habari za ndoa. Mtoto aliyelelewa na mama wa kambo mkorofi anajua ndoa ni kifungo pia

Mwisho mimi nawasupport wanaokataa ndoa kwa hiyari yao , inasaidia pia walio tayari kupata wenzi sahihi kwa sababu walio wengi hawapendeki utajituma vya kutosha umwoneshe mahaba yote lakini yeye hajali kwa baadhi yao ! Wengi ni Sadist .
Inapunguza na vifo 😂😂😂 No string attached
 
Kwa sisi Wakristo, ukisoma Kitabu cha Mwanzo 1:28 Biblia inasema, "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha;...".

Sikatai kwamba tunaweza tukaziliana bila ndoa, lakini huu ni uzinzi ambao ni dhambi machoni pa Mungu, na watoto ambao ni zao la uzinzi ni chukizo kwa Mungu. Soma 1Wakorintho 7:1-2, neno la Mungu linasema, "...heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwasababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe" (mume au mke anayezungumziwa hapa ni yule wa ndoa).

Ukisoma Mithali 18:22 neno linasema, "Apataye mke apata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Bwana".

Kibali ni nini? Kibali ni hali ya kukubalika katika jambo/kitu fulani. Kumbe ukioa unapata kibali kutoka kwa Mungu, hii ina maana hakuna jambo/kitu ambacho utatia mkono wako kisifanikiwe.

Kwanini vijana tunadanganyana kwamba tusioe?

Shida ni moja tu, mifarakano kwenye Taasisi ya ndoa ndiyo imesababisha kampeni hii huku wanaume tukiwatupia lawama wanawake kwamba wao ndiyo chanzo cha mifarakano hii, jambo ambalo si kweli.

Ukisoma 1Petro 3:7 neno linasema, "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe". Acha kushindana na mwanamke, Biblia imeshasema kwamba mwanamke ni chombo kisicho na nguvu, usishindane naye.

Sasa ni wanaume wangapi wanakaa na wake zao kwa akili? Wangapi wanawapa wake zao heshima kama neno linavyotufundisha? Wangapi hawashindani nao? Interesting part ya andiko hilo hapo juu ni kwamba ukilitii au ukilitimiza basi KUOMBA KWAKO HAKUTAZUILIWA, yani hakuna kitu utaomba kwa Mungu kisitimie, hapa najifunza kwamba wake zetu wanabeba mafanikio yetu endapo tukiwaheshimu na kuishi nao kwa akili.

Aidha, ukisoma 1Petro 3:1, wanawake wanaaswa KUTUTII WAUME ZAO. Sasa ni wanawake wangapi wanawatii waume zao? Lakini pia ukisoma Mithali 14:1 Biblia inasema "Mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake, bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe". Je, ni wanawake wangapi wenye hekima za kujenga nyumba zao kwa kutofuata ushauri mbaya wanaoshauriwa na marafiki zao ambao pengine wao hawajaolewa?

Hapa najifunza kwamba kila upande (ME na KE) unapaswa kuishi kwenye misingi yake ili Taasisi ya ndoa ilete tija iliyokusudiwa. Shida haiko kwa wanaume au wanawake tu; ingawa kuna upande unaweza ukawa una matatizo zaidi.

Niwe mkweli tu, upande wenye matatizo zaidi ni upande wetu wa ME. Mwanamke ukimpenda, ukimthamini, ukimtunza kwa kadiri ya kipato chako, ukimheshimu, NAKUHAKIKISHIA kwamba mwanamke huyu hawezi kukukosea heshima. Ukiona mwanamke amekengeuka ujue kuna shida mahali, na kwa kawaida mwanamke huwa anapenda mara moja tu, akichoka amechoka, huwa harudi nyuma.

Ni rai yangu kwa wanaume wenzangu kwamba tusiogope kuoa. Na unapomtafuta mwenza nakusihi usitumie macho na hekima ya kibinadamu bali umtangulize Mungu mbele. Usioe makalio, sura n.k. Sura siyo roho; kwamba akiwa na sura nzuri basi ana roho nzuri.

Mimi sijaoa ila I am on the way. Niko single but seriously searching. Mungu atusaidie vijana wote wenye dhamira ya dhati ya kuoa. Muwe na week end njema.
Mkuu ukristo ndivyo unavyo sema hivi ?

Una wafahamu hawa watu katika ukristo ?i, Yesu
ii, Paulo
iii, Padre
iv, Watawa
v, Waseja

Karibu.
 
Back
Top Bottom