Kataa ndoa wewe acha ulofa
Kampeni zinazohamasisha watu kukataa ndoa zisipewe nafasi Kwa kuwa hazina Nia njema ya kujenga jamii ,kinyume chake zinaharibu maadili yetu kama watanzania,wewe unayeshawishi watu wasioa umelelewa kwenye ndoa halafu unapotosha wengine wasioe .
 
Cha ajabu wanaoumia na kampeni ya KATAA NDOA ni walio kwenye ndoa, Sasa utajiuliza kama ndoa ni tamu wanateseka na nini?,Kila mtu aishi atakavyo. Wasiotaka ndoa waeleweke pia.
Mkuu, ndoa ni gereza, haswa kama wewe ni wale ambao mkifunga ndoa mpaka kifo kiwatenganishe ndo utajua hujui

Mimi ninaweza nikaoa muda wowote na nikatoa talaka muda wowote kulingana na imani yangu

Hao wanaochukizwa na kampeni za KATAA NDOA Wanajua yanayoendelea sio mazuri yangekuwa mazuri wasingechukizwa na hizi kampeni zinazoendelea badala yake wangeongeza wake maana vijana wa sasa wengi hawataki kuoa

Kwa kuongezea tu, tafuta uzi wa Mshana Jr unaoitwa "Mada maalumu kwa wanandoa"

Kule nimefunguka yaliyonisibu mpaka sasa linapokuja swala la kuoa najiuliza mara mbili mbili

Ninaye binti mzuri tu ana kila sifa ya kuwa mke lakini bado nahofia naweza kukutana nayo kama ya mwanzo japo mwenyewe anajitahidi kufanya kila awezalo ili nimuoe

Ila binafsi bado nikikumbuka yaliyonikuta naghairi
 
Kuna watu wametoka kufunga ndoa hata miezi 4 hawajafika,timbwili tayari

Ova
Ndoa sio sherehe ya kula na kunywa

Ndoa sio hitimisho la ngono ya masaa kadhaa pekee

Ndoa sio hitimisho au kifungo kwa umpendae

Ndoa sio utumwa kwa mwanamke Wala mwanaume

Ndoa bora haifungamani moja kwa moja na matamanio ya mwili na hisia pekee.



Haijalishi itakuwaje Mwanaume atabaki kuwa kiongozi wa familia unless you fail to select a partner...... OVER

(UTAPATA WA KUFANANA NAE)
 
Uliangalia vigezo Gani ? Ulipotaka kuoa.

1. Umri wa kuoa ulifika?
2. Ulimpenda ?
3. Alikupenda ?
4. Mzuri ?
5. Unamjua jina na sura ?
6. Ukamilifu wa tabia ? (Malaika)
7. Mengineyo (TAJA....)
 
Wajibiwe kwa hoja mbona wataacha kupiga ban ni kuukimbia ukweli.
Akileta hizo hoja nishtue ili twende sawa

Wanawake wenyewe wa kuoa ndo hawa wanaotaka 50 kwa 50?
Yaani wanasema haki sawa wakati huo huo wanakwambia pesa ya mwanamke ni yake peke yake ila ya mwanaume ni ya wote

Yaani kama wote tunafanya kazi na yeye anaingiza pesa ndefu kuliko mimi, lakini bado hiyo pesa ni yake peke yake (hii ni tabia ya ubinafsi walionayo wanawake na hapa ndipo tunaposema ndoa ni kwa ajili ya kumfaidisha mwanamke na kumrudisha nyuma kiuchumi mwanaume hapo utakuta mwanamke pesa yake anajengea kwao wakati mwanaume wazazi wake wanaishi kwenye nyumba ya miti)

NASUBIRI ALETE HOJA HAPA
 
Your browser is not able to display this video.

NDOA NI MRADI WAKUMNYONG'ONYEZA ME KIUCHUMI
 
Uliangalia vigezo Gani ? Ulipotaka kuoa.

1. Umri wa kuoa ulifika?
2. Ulimpenda ?
3. Alikupenda ?
4. Mzuri ?
5. Unamjua jina na sura ?
6. Ukamilifu wa tabia ? (Malaika)
7. Mengineyo (TAJA....)
Mkuu lete hoja na sio maswali, mpaka sasa nna 36+ nilioa nikiwa na 29+
Lete hoja za kuwashawishi vijana waoe na sio kuhoji ili kuonekana walikosea kuoa wakati kila mmoja ana mapungufu yake
 
Unayoyasema hapa sio kama hayawatokei au labda hawayajui

Wanayajua sana na ni kero kwao ila wanachodai busara ni kuvumilia
 
anaetaka 50/50 ni Demu wako sio wa wengine. Msipite kama hamuoni hoja na maswali yetu

NB. UTAPATA WA KUFANANA NAE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…