Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Nautafuta ule uzi kisha nakutagi mkuu hakikisha unapitia comment za kila mdau kuna kitu utajifunza

Kule wapo watu wanandoa zenye miaka 50+ nao wameelezea changamoto zao, yupo mama terry kule nae kachangia ule uzi

Hivyo nikikutag kule utajifunza zaidi maana uzi ni mrefu na kuna nondo haswa ambazo hata ukitaka kuingia kwenye ndoa unakuwa umeshajiandaa kisaikolojia

Yaani ni Jando tosha
Nikasome story zao kwenye comment ama ? Usinitag ww niambie ni madhara yapi nitayapata nikioa ? Mfano labda 1. Nikioa nitakufa mapema 2. Nikioa nitafilisika 3. Nikioa Demu wangu watamgonga n.k....... hata huko kwenye huo Uzi pitia alafu rejesha madini ya huko kwa ufupi hapa .
 
Jana buana, kuna mazaaa alikuwa amemkimbia mume wake miaka mitano, mume wake akamove on na maisha yake. Leo hii mwanamke amerudi analeta fujo anataka wagawane mali. Hii ni mojawapo ya fact kwamba ndoa ni kimbembe. Sema at the end, kuwa na mtu sahihi, ndoa ni kitu kizuri, campaign hii ikienda ikiwa inakemea mambo ambayo ni hasi kuhusu ndoa yanayoweza kurekebishika italeta ufahamu wa nini kirekebishwe ili ndoa iwe na matunda mazuri
Case closed [emoji359]
 
Ugomvi wenu wa kitoto sana.
Ugomvi wa kitoto sawa

Ujue mpaka nimejikuta namwacha yule mwanamke nimeshapitia taratibu zote

Mwisho wa siku mzee mwenye hekima na busara zake aliniita pembeni na kuniambia, "kama unaona habadiliki achana nae maana mnapoelekea ni kubaya"

Mimi mwenyewe nikafikiria nikaona ni kweli ninachoambiwa maana ilifika hatua chakula nikawa nakula na watoto (najua kama kaweka sumu au vitu vibaya hawezi kukubali watoto wadhurike)

Na hapo mwanamke ndo nilikuwa najitahidi mutimiza mahitaji yake lakini ndo kwanza akawa anaona kanikamata na sifurukuti

Ila cha ajabu sa hv anajidai kuniomba msamaha eti turudiane

Nimemjibu tu, "Hakuna nilichosahau kwako"
 
Pole sana.
 
Sasa mambo si hayo.

Ulikosea mwanzo . Ila una nafasi ya kufanya vyema mbeleni

NB. USIRUDIE MATAPISHI
 
If possible. Lakini kwann ukosee kuchagua ? Ww ni dhaifu kiasi Gani ukadanganywa
Unawezaje kujua tabia ya mtu katika kipindi cha uchumba?

Uchumba ni zone ambayo watu huficha madhaifu yao (fake life) au tabia zao na ndio maana mahusiano ya kiuchumba yanaweza fika hata miaka 10 mkawa mnapendana bila kuhitilafiana
 
Hakuna haja. Kampeni yao haiwezi fanikiwa. Jamii bado itakuwa na waoaji na waolewaji.
 
Wee huniambii kitu nikakuelewa,

Ningekuwa sijawahi kuoa hapo sawa,

Mimi nilifunga ndoa kabisa ya kiislamu ila mwanamke alipoanza kunipangia ratiba ya kwichi kwichi (na mimi hii ndo starehe yangu kubwa), baadae akaanza kuniambia nitaondoka mimi yeye nimuachie nyumba akae na watoto (wakati nyumba yenyewe ya kupanga), ikafika kipindi nikawa hata kurudi nyumbani nachukia nikajikuta nafanya kazi masaa kumi na sita,
Mwanamke unaacha kila kitu ndani lakini hapiki badala yake anaenda kununua chipsi anakula na watoto (huyo alikuwa mama wa nyumbani) nilikuwa nampatia kila anachohitaji mwisho wa siku akawa anajisifu kwa watoto wa dada yangu kwa kuwaambia,
"huyo mjomba wenu mwenyewe nampelekesha"

Siku anaamua kuondoka nyumbani yeye mwenyewe akachukua kila kitu na bado narudi kazini nakuta barua kutoka chang'ombe polisi kanifungulia kesi kwamba nimemfukuza, nimemtolea vyombo nje (ninachoshukuru wale kina dada/mama walikuwa ni waelewa) na walijua kwamba yeye ndo mwenye matatizo hivyo walimuuliza tu, "kwa hiyo wewe unatakaje?"

Akajibu, "nahitaji kila mwezi anipe pesa kwa ajili ya watoto" (kimoyo moyo nikajisemea huyu kumbe anataka kuwatumia watoto kama kitega uchumi chake)
Maana kabla hatujaachana nilishawahi kumwambia, "nakupa miezi mitatu fikiria ni biashara gani utakayoweza kufanya ambayo itakuwezesha kuhudumia watoto hata ikitokea siku nimekufa" huwezi amini ilipita miezi mitatu nakuja kumuuliza umefikia wapi, ananijibu l, "sijaona biashara ya kufanya", shiiit

Kifupi huyu mwanamke kuna kipindi nilikuwa naishi nae kwa tahadhari, maana nilikuwa naona kabisa tunapoelekea kuna siku mmoja atamuua mwenzie

Kisha mnajaribu kutushawishi tuoe, aaah weeee... tena kwa sasa hivi wapo na msimamo wao wa 50 kwa 50

Nakwambia, "Niache kidogo"
Pole mkuu,kwa watu waliopitia changamoto kama zako ni ngumu kumshawishi
Ila sasa yawezekana makosa yalikuwa yako maybe hukuwa makini kwenye kuchagua mwenza mfano mazingira aliyopo na wazazi wake pia
Ko nadhani kuna haja ya kujaribu tena,wanawake wazuri wapo sana
 
Sasa mambo si hayo.

Ulikosea mwanzo . Ila una nafasi ya kufanya vyema mbeleni

NB. USIRUDIE MATAPISHI
Pamoja mkuu

Nilikosea mwanzo, na ili umpate mwanamke sahihi inabidi uwe makini haswa

Maana wanawake kwa kuigiza hatuwawezi anaweza akakuigizia tabia zote nzuri unazihitaji ila siku ukimuoa sasa anaanza kuziachia
 
Cha ajabu wanaoumia na kampeni ya KATAA NDOA ni walio kwenye ndoa, Sasa utajiuliza kama ndoa ni tamu wanateseka na nini?,Kila mtu aishi atakavyo. Wasiotaka ndoa waeleweke pia.
Wanaoumia ni wale wenye vijana wao wa kike na wa kiume ambao hawatamani wazaane hovyo bila utaratibu wa ndoa na wanajua kwa dunia ya teknolojia watapita kusoma hizi mada nyakati fulani katika maisha yao. Inapendeza kuwa kuna watu wengi wanaelewa kwann katika nyakati fulani huko nyuma binadamu walikuja na mfumo wa ndoa badala ya kupandana kama ng'ombe. Hakuna jipya chini ya jua. Kuna sababu kwann binadamu alifikia uamuzi wa kuweka utaratibu wa ndoa.
 
Pole mkuu,kwa watu waliopitia changamoto kama zako ni ngumu kumshawishi
Ila sasa yawezekana makosa yalikuwa yako maybe hukuwa makini kwenye kuchagua mwenza mfano mazingira aliyopo na wazazi wake pia
Ko nadhani kuna haja ya kujaribu tena,wanawake wazuri wapo sana
Ahsante mkuu
 
Mnapiga kelele alafu mnata mjibiwe kwa hoja ?

Leteni hoja .

Ndoa ni utumwa kivipi? (how).
Kataa Ndoa kwann ? (Why)

Otherwise nyie ni waropokaji msiokuwa na hoja .

HOJA HOJA HOJA.
Sipo kwenye hiyo kampeni ya kataa ndoa ila kiuhalisia asilimia 90 ya ndoa zinapumulia mashine, waathirika wakubwa wa mazila ya ndoa ni wanaume.

Hichi kizazi Cha 50/50 ni tatizo kubwa mno, hizi sheria za ndoa na ustawi wa jamii zinamkandamiza mwanaume, nitarudi kuelezea visa vitatu hapa na changu kikiwepo
 
Back
Top Bottom