Demi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 40,466
- 88,695
Naolewa keshoBado hujaolewa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naolewa keshoBado hujaolewa?
Hakuna anayetishika, visa haviwezi kufanana kuna ambao wanaishi vizuri hawana tatizoAhsante mkuu
Tukirudi kwenye hizi kampeni zinazoendelea
Hawa wapiga kampeni (na mimi mmoja wapo) wakimpata mwanamke sahihi kwao wanaoa hivyo zisiwatishe mlio kwenye ndoa
Maana bado inatumika kauli, "zakuambiwa changanya na zako".
Utafiti usio rasmi.Sipo kwenye hiyo kampeni ya kataa ndoa ila kiuhalisia asilimia 90 ya ndoa zinapumulia mashine, waathirika wakubwa wa mazila ya ndoa ni wanaume.
Hichi kizazi Cha 50/50 ni tatizo kubwa mno, hizi sheria za ndoa na ustawi wa jamii zinamkandamiza mwanaume, nitarudi kuelezea visa vitatu hapa na changu kikiwepo
Ni kweli mkuu na ni kwa sababu kila mmoja kampata mtu sahihi kwakeHakuna anayetishika, visa haviwezi kufanana kuna ambao wanaishi vizuri hawana tatizo
We umeolewaNasisitiza kama hutai kuoa bhas jua utaolewa tu one day
Ndugu yangu ni kuvumilia mengi. Ndoa kudumu inabidi ujitoe muhanga ni kufa wewe au yeye. Kuna wakati kabisa unahisi kapigwa nje ila unakausha. Inauma ujue.Dah kweli ila kunA wengne wameoa na wanaishi vzuri tu au ndo wanatuektia
Wewe ulikosea kuoa,hapo tatizo sio ndoa bali uliingia ndoa kwa mguu wa kushoto.Wee huniambii kitu nikakuelewa,
Ningekuwa sijawahi kuoa hapo sawa,
Mimi nilifunga ndoa kabisa ya kiislamu ila mwanamke alipoanza kunipangia ratiba ya kwichi kwichi (na mimi hii ndo starehe yangu kubwa), baadae akaanza kuniambia nitaondoka mimi yeye nimuachie nyumba akae na watoto (wakati nyumba yenyewe ya kupanga), ikafika kipindi nikawa hata kurudi nyumbani nachukia nikajikuta nafanya kazi masaa kumi na sita,
Mwanamke unaacha kila kitu ndani lakini hapiki badala yake anaenda kununua chipsi anakula na watoto (huyo alikuwa mama wa nyumbani) nilikuwa nampatia kila anachohitaji mwisho wa siku akawa anajisifu kwa watoto wa dada yangu kwa kuwaambia,
"huyo mjomba wenu mwenyewe nampelekesha"
Siku anaamua kuondoka nyumbani yeye mwenyewe akachukua kila kitu na bado narudi kazini nakuta barua kutoka chang'ombe polisi kanifungulia kesi kwamba nimemfukuza, nimemtolea vyombo nje (ninachoshukuru wale kina dada/mama walikuwa ni waelewa) na walijua kwamba yeye ndo mwenye matatizo hivyo walimuuliza tu, "kwa hiyo wewe unatakaje?"
Akajibu, "nahitaji kila mwezi anipe pesa kwa ajili ya watoto" (kimoyo moyo nikajisemea huyu kumbe anataka kuwatumia watoto kama kitega uchumi chake)
Maana kabla hatujaachana nilishawahi kumwambia, "nakupa miezi mitatu fikiria ni biashara gani utakayoweza kufanya ambayo itakuwezesha kuhudumia watoto hata ikitokea siku nimekufa" huwezi amini ilipita miezi mitatu nakuja kumuuliza umefikia wapi, ananijibu l, "sijaona biashara ya kufanya", shiiit
Kifupi huyu mwanamke kuna kipindi nilikuwa naishi nae kwa tahadhari, maana nilikuwa naona kabisa tunapoelekea kuna siku mmoja atamuua mwenzie
Kisha mnajaribu kutushawishi tuoe, aaah weeee... tena kwa sasa hivi wapo na msimamo wao wa 50 kwa 50
Nakwambia, "Niache kidogo"
Kuwa nje ya mfumo wa maadiliUtamu wa ndoa ni upi zaid ,tofauti na wasio na ndoa wana wanawake na mbususu wanaoga nazo na watoto wanao?
Leteni hoja ?Naunga mkono hoja. hatuwezi kuwa na jamii inayotaka kufanya tendo la ndoa bila ndoa
Kuna mkuu nimeenda nae sawa na nimemuelewa na yeye kanielewa ninachomaanishaWewe ulikosea kuoa,hapo tatizo sio ndoa bali uliingia ndoa kwa mguu wa kushoto.
Ulichunguza asili yao.
Ulichunguza hali yake ya kiroho ipoje au ulitazama nje.
Unaweza ukaoa shetani akatutenda ukachukia wanawake wote.
Wapo wanawake wanaojua nini maana ya mume.
Dah kweLi mliooa ou walioolewa wanaptua changamoto sanaNdugu yangu ni kuvumilia mengi. Ndoa kudumu inabidi ujitoe muhanga ni kufa wewe au yeye. Kuna wakati kabisa unahisi kapigwa nje ila unakausha. Inauma ujue.
Sio wote mkuu, ukioa/kuolewa na mtu sahihi mtaishi vizuri, tatizo kuigiziana wakati wa uchumba afu baadae mkija kuingia kwenye ndoa kila mmoja anaanza kuonyesha tabia zake halisi na kujikuta mnatofautianaDah kweLi mliooa ou walioolewa wanaptua changamoto sana
Sasa hayo si mambo yako binafsi? Yaani kuchapiwa kwako na kuachwa na mkeo ndio utuhusishe na sisi? Eti nimuache mama manka wangu kisa mpuuzi mmoja anaendesha kampeni mtandaoni kwa fake I'd kisa kaachwa na mkewe?Mimi nillioa nikaachaa kwa TALAKA, Bado nasisitiza, KATAA NDOA, NDOA NI UTUMWA, NDOA NI KWA AJILI YA KUMFAIDISHA MWANAMKE, NDOA NI KWA AJILI YA KUMKANDAMIZA MWANAUME,
KATAA NDOA
KATAA NDOA
KATAA NDOA
Liverpool VPN njoo huku