Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Ahsante mkuu

Tukirudi kwenye hizi kampeni zinazoendelea

Hawa wapiga kampeni (na mimi mmoja wapo) wakimpata mwanamke sahihi kwao wanaoa hivyo zisiwatishe mlio kwenye ndoa

Maana bado inatumika kauli, "zakuambiwa changanya na zako".
Hakuna anayetishika, visa haviwezi kufanana kuna ambao wanaishi vizuri hawana tatizo
 
Sipo kwenye hiyo kampeni ya kataa ndoa ila kiuhalisia asilimia 90 ya ndoa zinapumulia mashine, waathirika wakubwa wa mazila ya ndoa ni wanaume.

Hichi kizazi Cha 50/50 ni tatizo kubwa mno, hizi sheria za ndoa na ustawi wa jamii zinamkandamiza mwanaume, nitarudi kuelezea visa vitatu hapa na changu kikiwepo
Utafiti usio rasmi.

Na hata ikiwa hivo , fahamu wao sio ww, na ww sio wao .

Asilimia 90% ya watanzania ni masikini

haimaanishi Mo Dewji, Rostam Aziz, Bakhresa, Diamond, Alikiba, Marioo, MillardAyo, na Laizer mmasai wa mgodini sio watanzania.

If possible be 10% remain.
 
Wee huniambii kitu nikakuelewa,

Ningekuwa sijawahi kuoa hapo sawa,

Mimi nilifunga ndoa kabisa ya kiislamu ila mwanamke alipoanza kunipangia ratiba ya kwichi kwichi (na mimi hii ndo starehe yangu kubwa), baadae akaanza kuniambia nitaondoka mimi yeye nimuachie nyumba akae na watoto (wakati nyumba yenyewe ya kupanga), ikafika kipindi nikawa hata kurudi nyumbani nachukia nikajikuta nafanya kazi masaa kumi na sita,
Mwanamke unaacha kila kitu ndani lakini hapiki badala yake anaenda kununua chipsi anakula na watoto (huyo alikuwa mama wa nyumbani) nilikuwa nampatia kila anachohitaji mwisho wa siku akawa anajisifu kwa watoto wa dada yangu kwa kuwaambia,
"huyo mjomba wenu mwenyewe nampelekesha"

Siku anaamua kuondoka nyumbani yeye mwenyewe akachukua kila kitu na bado narudi kazini nakuta barua kutoka chang'ombe polisi kanifungulia kesi kwamba nimemfukuza, nimemtolea vyombo nje (ninachoshukuru wale kina dada/mama walikuwa ni waelewa) na walijua kwamba yeye ndo mwenye matatizo hivyo walimuuliza tu, "kwa hiyo wewe unatakaje?"

Akajibu, "nahitaji kila mwezi anipe pesa kwa ajili ya watoto" (kimoyo moyo nikajisemea huyu kumbe anataka kuwatumia watoto kama kitega uchumi chake)
Maana kabla hatujaachana nilishawahi kumwambia, "nakupa miezi mitatu fikiria ni biashara gani utakayoweza kufanya ambayo itakuwezesha kuhudumia watoto hata ikitokea siku nimekufa" huwezi amini ilipita miezi mitatu nakuja kumuuliza umefikia wapi, ananijibu l, "sijaona biashara ya kufanya", shiiit


Kifupi huyu mwanamke kuna kipindi nilikuwa naishi nae kwa tahadhari, maana nilikuwa naona kabisa tunapoelekea kuna siku mmoja atamuua mwenzie


Kisha mnajaribu kutushawishi tuoe, aaah weeee... tena kwa sasa hivi wapo na msimamo wao wa 50 kwa 50

Nakwambia, "Niache kidogo"
Wewe ulikosea kuoa,hapo tatizo sio ndoa bali uliingia ndoa kwa mguu wa kushoto.
Ulichunguza asili yao.
Ulichunguza hali yake ya kiroho ipoje au ulitazama nje.
Unaweza ukaoa shetani akatutenda ukachukia wanawake wote.
Wapo wanawake wanaojua nini maana ya mume.
 
Wewe ulikosea kuoa,hapo tatizo sio ndoa bali uliingia ndoa kwa mguu wa kushoto.
Ulichunguza asili yao.
Ulichunguza hali yake ya kiroho ipoje au ulitazama nje.
Unaweza ukaoa shetani akatutenda ukachukia wanawake wote.
Wapo wanawake wanaojua nini maana ya mume.
Kuna mkuu nimeenda nae sawa na nimemuelewa na yeye kanielewa ninachomaanisha

Ila fuatilia kwanza comment zote utanielewa

Binafsi huwa nimeanzisha tabia ya kutomjibu mtu mpaka nisome comment zote kisha ndo baadae namjibu

Tafuta na uzi wenye jina hili, "

Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena​


Huu wa mkuu DeepPond kuna vya kujifunza pia

Nyuzi zipo nyingi tu na zote zinaletwa na sisi wanaume tukiwalalamikia wanawake
 
Ndugu yangu ni kuvumilia mengi. Ndoa kudumu inabidi ujitoe muhanga ni kufa wewe au yeye. Kuna wakati kabisa unahisi kapigwa nje ila unakausha. Inauma ujue.
Dah kweLi mliooa ou walioolewa wanaptua changamoto sana
 
Dah kweLi mliooa ou walioolewa wanaptua changamoto sana
Sio wote mkuu, ukioa/kuolewa na mtu sahihi mtaishi vizuri, tatizo kuigiziana wakati wa uchumba afu baadae mkija kuingia kwenye ndoa kila mmoja anaanza kuonyesha tabia zake halisi na kujikuta mnatofautiana

Hapo ndipo ndoa inapokuwa ndoana

Kuna mdau kwenye ule uzi wa "Mada maalumu kwa wanandoa" wa Mshana Jr alisema, "UNAPOOA KAA UKIJUA UNAMMILIKI MTU MWENYE AKILI ZAKE TIMAMU"
 
Mimi nillioa nikaachaa kwa TALAKA, Bado nasisitiza, KATAA NDOA, NDOA NI UTUMWA, NDOA NI KWA AJILI YA KUMFAIDISHA MWANAMKE, NDOA NI KWA AJILI YA KUMKANDAMIZA MWANAUME,

KATAA NDOA


KATAA NDOA


KATAA NDOA

Liverpool VPN njoo huku
Sasa hayo si mambo yako binafsi? Yaani kuchapiwa kwako na kuachwa na mkeo ndio utuhusishe na sisi? Eti nimuache mama manka wangu kisa mpuuzi mmoja anaendesha kampeni mtandaoni kwa fake I'd kisa kaachwa na mkewe?
 
Ila kiukweli wake za watu wanabutuliwa sana hapo nje, kuoa sio kubaya lakini sio guarantee life itakuwa nzuri, unaweza kutamani uwe single again, kwa statistics nchi ya Marekani zaidi ya nusu ya ndoa 60% zinaishia na divorce na wengine wengi wanaoendelea kukaa pamoja wanajikuta wapo kwenye sexless life for years, nilikuwa siamini kama inawezekana kukaa na mwanamke bila shughulilakini yaliwahi kunikuta nilikaa na mwanamke nyumba moja na hatukufanya mapenzi for almost 9 months, ilikuwa karibu tuuane huko ndani
 
Ebanaee,kila mtu aishi atakavyo,kupangiana namna ya kuishi sio poa,japo ni kwl ndoa za siku hiz ni lukumba lukumba mwendo wa ngamia!
 
Back
Top Bottom