Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Unasoma lakini wachangiaji wanasema nini?! Ukiona watu wanatoa maoni yao kuhusu jambo lolote usipende kuwaona wanakosea kabla haujawaelewa. Inawezekana hayo maoni yao ni experience binafsi kwenye maisha yao so wanahaki ya kushare.
 
Kampeni zinazohamasisha watu kukataa ndoa zisipewe nafasi Kwa kuwa hazina Nia njema ya kujenga jamii ,kinyume chake zinaharibu maadili yetu kama watanzania,wewe unayeshawishi watu wasioa umelelewa kwenye ndoa halafu unapotosha wengine wasioe .
Hii ni free platform, huwezi piga ban mawazo ya mtu, kama hukubaliani nayo, jifunze programming languages kama html, java na cs kaanzishe platform nyingine.
Hata Mungu sio dikteta ila ni Hakimu.
 
Ila kiukweli wake za watu wanabutuliwa sana hapo nje, kuoa sio kubaya lakini sio guarantee life itakuwa nzuri, unaweza kutamani uwe single again, kwa statistics nchi ya Marekani zaidi ya nusu ya ndoa 60% zinaishia na divorce na wengine wengi wanaoendelea kukaa pamoja wanajikuta wapo kwenye sexless life for years, nilikuwa siamini kama inawezekana kukaa na mwanamke bila shughulilakini yaliwahi kunikuta nilikaa na mwanamke nyumba moja na hatukufanya mapenzi for almost 9 months, ilikuwa karibu tuuane huko ndani
Ilikuwaje mkuu
 
Kampeni zinazohamasisha watu kukataa ndoa zisipewe nafasi Kwa kuwa hazina Nia njema ya kujenga jamii ,kinyume chake zinaharibu maadili yetu kama watanzania,wewe unayeshawishi watu wasioa umelelewa kwenye ndoa halafu unapotosha wengine wasioe .
@moderators
 
Ndoa ni upumbav.... Tena mwanaume kuharakisha kuoa ni kujichimbia kabuli.. ni upuuzi kufunga ndoa... Tafuta mwanaume au mwanamke zaa nae then achana nae fanya maisha yako... Ukitaka kufanikiwa ktk maisha basi epuka ndoa hasa kwa wanawake... Wanawake wengi masikini kwasabab ya kuolewa... Wanaume wengi wanakufa mapema kwasabab ya ndoa
 
Unawezaje kujua tabia ya mtu katika kipindi cha uchumba?

Uchumba ni zone ambayo watu huficha madhaifu yao (fake life) au tabia zao na ndio maana mahusiano ya kiuchumba yanaweza fika hata miaka 10 mkawa mnapendana bila kuhitilafiana
Fact kabisa.
 
Kampeni zinazohamasisha watu kukataa ndoa zisipewe nafasi Kwa kuwa hazina Nia njema ya kujenga jamii, kinyume chake zinaharibu maadili yetu kama watanzania, wewe unayeshawishi watu wasioE umelelewa kwenye ndoa halafu unapotosha wengine wasioe .
Maadili ndiyo nini?
 
Sio wote mkuu, ukioa/kuolewa na mtu sahihi mtaishi vizuri, tatizo kuigiziana wakati wa uchumba afu baadae mkija kuingia kwenye ndoa kila mmoja anaanza kuonyesha tabia zake halisi na kujikuta mnatofautiana

Hapo ndipo ndoa inapokuwa ndoana

Kuna mdau kwenye ule uzi wa "Mada maalumu kwa wanandoa" wa Mshana Jr alisema, "UNAPOOA KAA UKIJUA UNAMMILIKI MTU MWENYE AKILI ZAKE TIMAMU"
Kbsa mkuu
 
Utafiti usio rasmi.

Na hata ikiwa hivo , fahamu wao sio ww, na ww sio wao .

Asilimia 90% ya watanzania ni masikini

haimaanishi Mo Dewji, Rostam Aziz, Bakhresa, Diamond, Alikiba, Marioo, MillardAyo, na Laizer mmasai wa mgodini sio watanzania.

If possible be 10% remain.
Na wewe sio Mimi na Mimi sio wewe so Baki ulivyo na mimi nibaki nilivyo
 
Kampeni zinazohamasisha watu kukataa ndoa zisipewe nafasi Kwa kuwa hazina Nia njema ya kujenga jamii, kinyume chake zinaharibu maadili yetu kama watanzania, wewe unayeshawishi watu wasioE umelelewa kwenye ndoa halafu unapotosha wengine wasioe .
Yaani huwa nashangaa mno kama hutaki kuoa unataka nini!? Kuolewa;?[emoji848][emoji2827]
 
Oa upate stress owa ubebe majukumu ya watu wanaume walio kwenye ndoa wanamsemo wao kwamba mwanaume majukumu bna uku roho zinawauma, owa uishi kwa manung'uniko kila siku.

Kata ndoa uishi kwa amani,
kata ndoa ufurahie maisha
kata ndoa uwe huru .
Kata ndoa usipangiwe cha kufanya
 
Ndoa ni taasisi njema by its foundations. Hivi karibuni kumetokea mabadiliko mengi yaliyopelekea ndoa kuwa na maumivu zaidi ya furaha.

Hakuna mtu amesomea uvumilivu, uvumilivu tunajifunza tu, na wala hakuna guarantee kwamba umejifunza na umefaulu. Kama hukufaulu, ndoa hugeuka na kuwa kitu cha ajabu.

Kizazi cha sasa hakina mfanano sawia na cha zamani kdg na kwa hiyo sitegemei ndoa za sasa ziwe sawa na za wazee wetu. Na huenda tafsiri ya ndoa kitaani ikawa nyingine kabisa. My take: Wanawake wa sasa (sio wote lakini) hupenda kuolewa kwa ajili kutatua matatizo yao yaliyoshindikana kama angeamua kupambana kivyake. Wanaume wa sasa (sio wote) huoa kwanza kwa Tamaa ya mwanamke mzuri pengine, halafu pili Pride ya kuwa mtoto au watoto. Hakuna love hapo.
 
Back
Top Bottom