Nikasome story zao kwenye comment ama ? Usinitag ww niambie ni madhara yapi nitayapata nikioa ? Mfano labda 1. Nikioa nitakufa mapema 2. Nikioa nitafilisika 3. Nikioa Demu wangu watamgonga n.k....... hata huko kwenye huo Uzi pitia alafu rejesha madini ya huko kwa ufupi hapa .
 
Case closed [emoji359]
 
Ugomvi wenu wa kitoto sana.
Ugomvi wa kitoto sawa

Ujue mpaka nimejikuta namwacha yule mwanamke nimeshapitia taratibu zote

Mwisho wa siku mzee mwenye hekima na busara zake aliniita pembeni na kuniambia, "kama unaona habadiliki achana nae maana mnapoelekea ni kubaya"

Mimi mwenyewe nikafikiria nikaona ni kweli ninachoambiwa maana ilifika hatua chakula nikawa nakula na watoto (najua kama kaweka sumu au vitu vibaya hawezi kukubali watoto wadhurike)

Na hapo mwanamke ndo nilikuwa najitahidi mutimiza mahitaji yake lakini ndo kwanza akawa anaona kanikamata na sifurukuti

Ila cha ajabu sa hv anajidai kuniomba msamaha eti turudiane

Nimemjibu tu, "Hakuna nilichosahau kwako"
 
Pole sana.
 
Sasa mambo si hayo.

Ulikosea mwanzo . Ila una nafasi ya kufanya vyema mbeleni

NB. USIRUDIE MATAPISHI
 
If possible. Lakini kwann ukosee kuchagua ? Ww ni dhaifu kiasi Gani ukadanganywa
Unawezaje kujua tabia ya mtu katika kipindi cha uchumba?

Uchumba ni zone ambayo watu huficha madhaifu yao (fake life) au tabia zao na ndio maana mahusiano ya kiuchumba yanaweza fika hata miaka 10 mkawa mnapendana bila kuhitilafiana
 
Hakuna haja. Kampeni yao haiwezi fanikiwa. Jamii bado itakuwa na waoaji na waolewaji.
 
Pole mkuu,kwa watu waliopitia changamoto kama zako ni ngumu kumshawishi
Ila sasa yawezekana makosa yalikuwa yako maybe hukuwa makini kwenye kuchagua mwenza mfano mazingira aliyopo na wazazi wake pia
Ko nadhani kuna haja ya kujaribu tena,wanawake wazuri wapo sana
 
Sasa mambo si hayo.

Ulikosea mwanzo . Ila una nafasi ya kufanya vyema mbeleni

NB. USIRUDIE MATAPISHI
Pamoja mkuu

Nilikosea mwanzo, na ili umpate mwanamke sahihi inabidi uwe makini haswa

Maana wanawake kwa kuigiza hatuwawezi anaweza akakuigizia tabia zote nzuri unazihitaji ila siku ukimuoa sasa anaanza kuziachia
 
Cha ajabu wanaoumia na kampeni ya KATAA NDOA ni walio kwenye ndoa, Sasa utajiuliza kama ndoa ni tamu wanateseka na nini?,Kila mtu aishi atakavyo. Wasiotaka ndoa waeleweke pia.
Wanaoumia ni wale wenye vijana wao wa kike na wa kiume ambao hawatamani wazaane hovyo bila utaratibu wa ndoa na wanajua kwa dunia ya teknolojia watapita kusoma hizi mada nyakati fulani katika maisha yao. Inapendeza kuwa kuna watu wengi wanaelewa kwann katika nyakati fulani huko nyuma binadamu walikuja na mfumo wa ndoa badala ya kupandana kama ng'ombe. Hakuna jipya chini ya jua. Kuna sababu kwann binadamu alifikia uamuzi wa kuweka utaratibu wa ndoa.
 
Ahsante mkuu
 
Mnapiga kelele alafu mnata mjibiwe kwa hoja ?

Leteni hoja .

Ndoa ni utumwa kivipi? (how).
Kataa Ndoa kwann ? (Why)

Otherwise nyie ni waropokaji msiokuwa na hoja .

HOJA HOJA HOJA.
Sipo kwenye hiyo kampeni ya kataa ndoa ila kiuhalisia asilimia 90 ya ndoa zinapumulia mashine, waathirika wakubwa wa mazila ya ndoa ni wanaume.

Hichi kizazi Cha 50/50 ni tatizo kubwa mno, hizi sheria za ndoa na ustawi wa jamii zinamkandamiza mwanaume, nitarudi kuelezea visa vitatu hapa na changu kikiwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…