[emoji23] [emoji1787] Hii kauli nimeikumbuka juzi nimemwambia mama watoto, japo ilikuwa kimasihara, nimepika msosi fresh, kaja mgeni nikaenda kumsikiliza, narudi ndani si namkuta mwenzangu anafakamia msosi.. [emoji23], nikamwambia ndio maana tunakufa mapema..
Jibu lake,
[emoji23], akacheka, "hii sio sababu, sababu ni nyingi, ukiacha maisha na mastress tuliyonayo, pia uzembe wa magonjwa unatumaliza, wanawake wakiumwa kidogo wanatafuta tiba, sisi hatujali afaya tukiumwa kidogo tunavumilia, hata ukienda hospital wanawake wengi na utakuta bado ugonjwa haujawa mkubwa, sogea kwetu wakina baba, ukimkuta mwanaume kama ni kifua kikuu basi kimemtafuna kisawa sawa"
Hiki kitu kimenifikirisha mnoo, kuna kaukweli hapa, mie viugonjwa vingi mnoo navipuuzia.