Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya

Umeanza vizuri ila umemalizia kwa kuchochora.

Wanasheria wote yaani Wanasheria wa Serikali, Mawakili binafsi, Mahakimu na Majaji, hufundishwa vitu vinavyofanana na huhitimu pamoja Shahada ya Sheria.

Kwa hiyo, kama ni mbinu, basi wote wanapewa mbinu sawasawa, yaani hakimu anaweza kuwa wakili, wakili anaweza kwenda upande wa Serikali, na pia wote hawa wanaweza kuwa Majaji.

Kinachotofautisha kazi zao ni uzito wa kesi, na upande waliosimama.

Kwa hiyo huwezi kusema huyu kapewa na yule kanyimwa.
 
mnamuonea wakili. sheria zetu zina loopholes. na kingine tz shida iko kwenye upelelezi. tuna perform sifuri hilo eneo. wanaopindisha kesi ni askari wa upelelezi.
Kumbuka pia mpelelezi anawea akawa mzuri ila mwanasheria akawa vizuri zaidi kwa kuupinga ushahidi wake kwa hoja nzito nzito.
 


Msingi wa kesi yeyote ni ushahidi. Ushahidi ukiwa mzuri na halisi, na jaji akiukubali kisheria basi lazima upate haki.

Kuna watu wanakosa haki zao kwa sababu ya kushindwa namna ya kuidai, wapi pa kwenda na wakati gani aende, na aende na kitu gani na kwa nani.

Wakili ana jukumu la kumuelewesha mteja wake na siyo kukataa maelekezo ya mteja wake.

Mfano, wakili ana jukumu la kumuelewesha mteja njia mbadala wa kupata haki yake, lakini hatakiwi kukataa maelekezo halali ya mteja, mfano kutaka kwenda mahakamani n.k.

Kila kitu sheria imeelekeza!
 
Yaaani sijui kwann hizi mahakama zinakuwa hivi, mtu kakamatwa toka 2016 upelelrzi unakuja kukamilika 2024 na unakutwa hauna hatia asee[emoji849]
 
Katika kesi ya Miriam Mrita ushahidi ulikuwa wa mazingira na siyo wa moja kwa moja, na pia hati ya mashtaka ilikosewa na hivyo kufanya watuhumiwa kukwepa adhabu.
Hii hapa sasa mkuu! hapa ndipo hao wanasheria huwa wanakula mlungula. Kama hati umekosea kwa nini wanasheria wasione mapema mpaka wasubiri mahakamani? Halafu kwenye hizi kesi MAWAKILI wanaowekwa na serikali wanakula sana rushwa! Tulikuwa na kesi moja ya mauaji eti mwanasheria wa kwetu anaenda kuongea na mtuhumiwa kwa kificho hapo hapo mahakamani? Kwenye kuuliza maswali kanauliza maswali ya ngumbaru kanaacha yale maswali ya msingi! Pumbavu kabisa wanasheria wote! Nyie wanasheria nawalaani kuanzia sasa na Mungu awafichie hiyo mbingu msiione!
 

Sijakuelewa.

Ilikuwaje mkawa na mwanasheria wenu kwenye kesi ya jinai?

Iwapo mlikuwa na mwanasheria, je, mtuhumiwa alikuwa ni ndugu yako?
 
Ahsante mkuu Kwa ufafanuzi, of course naelewa hiyo ila nilikuwa nawaza Kwa Sauti Kwa wale wazee wa deal mjini anakupiga na unafungua kesi mnaanza kupelekeshana Kwa vifungu, unajikuta unakataa tamaa kushindwa mahakamani kama kawaida yetu wazee wa "namwachia Mungu"
 
Mawakili wa serikali wana kazi ngumu sana kwa sababu wao ndiyo wanaibeba kesi kwa asilimia 90.
Na ndio maana nikasema ni failures, wameridhika na check number na mishahara inaingia with or without winning. Tofauti na private sector mawakili inabidi wajitume maana the more anashinda kesi ndio more anaongeza wateja/bei.

Kaangalia hata zile Arbitration mawakili wa Tanzania we PhD wanazidiwa na vitoto vya undergraduate hadi aibu. Mpaka kutetea vidhibiti vya upande wa Tanzania wanashindwa!! So issue sio ushahidi ni ubovu wa mawakili wa serikali.

Waambie wenzako wabadilike wanatutia aibu na hasara daily.
 
Hata wakiomba watashindwa tena kesi yenye.miaka 10 wwalishindwa nini kujipanga miaka yote Kumi na wameipoteza?
It depends on judge's reasoning, kama reasoning ni ya hovyo wanaweza kushinda. majaji wenyewe hawa wa kuokoteza..... hawana sifa za majaji wa zamani ........ idogo labda Court of appeal ( ingawa nao wanatokana na hao, ila somehow wanakuwa vey carefylly selected kama hakuna influence ya wana siasa. Lakini kwa huyu Juma, hamna kitu!
 
Ile kesi ilihitaji majaji mahiri kama akina Lugakingira, sio hawa UPE! Kakolaki hawezi ku handle kesi kama hiyo..... tuwekee hapa tuipite tuone reasoning ya Judge!
Umenikumbusha mbali sana kumtaja Lugakingira.
J. Mwalusanya.
R. Kisanga

The best of the best.
 

Mawakili wa pande zote wanaongozwa na Code of Ethics ambazo kimsingi zinamtaka Wakili aisaidie jamii na mahakama katika kutafuta haki na SIYO KUSHINDA KESI.

Kushinda kesi siyo kazi ya wakili popote duniani.

Kazi ya uwakili ni kazi yenye kuhitaji ujasiri na uwazi ndiyo maana wanavaa mavazi ya rangi nyeusi na nyeupe.

Mawakili, Majaji na Mahakimu kwa pamoja ni Maafisa wa Mahakama wenye lengo moja la kutafuta haki na siyo kushinda kesi.

Mtuhumiwa anapoachiwa, ama kufungwa, vyovyote tunasema hiyo ni haki yake na siyo ushindi wake.
 
Kimsingi, tuaamini kwamba Mungu ndiye mtoa haki na hutolea haki Mbinguni.

Hapa duniani kazi ya kutoa haki ni ya Mahakama ( WANASHERIA). Sasa unapokosewa halafu unadai kumwachia Mungu siyo sawa.

Mimi nindhani umuombe Mungu akupe maarifa na siyo kumuachia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…