Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya

Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya

Mawakili wa pande zote wanaongozwa na Code of Ethics ambazo kimsingi zinamtaka Wakili aisaidie jamii na mahakama katika kutafuta haki na SIYO KUSHINDA KESI.

Kushinda kesi siyo kazi ya wakili popote duniani.

Kazi ya uwakili ni kazi yenye kuhitaji ujasiri na uwazi ndiyo maana wanavaa mavazi ya rangi nyeusi na nyeupe.

Mawakili, Majaji na Mahakimu kwa pamoja ni Maafisa wa Mahakama wenye lengo moja la kutafuta haki na siyo kushinda kesi.

Mtuhumiwa anapoachiwa, ama kufungwa, vyovyote tunasema hiyo ni haki yake na siyo ushindi wake.
Shaaban Robert alisema _Uanasheria ni elimu ya kupingana na haki. Was he right?
 
Daah polen sana Auntuja polen sana dada zangu, na wazee wangu. Rafiki yangu Erasto Mungu azid kukupa pumziko la Aman tuonane ile asubuh iliyo njema. that's how life it's. Jambo la muhimu kukumbuka daima ni hili.
Kabla hujaoa piga magoti funga hata mwez tu muombe Mungu akupe mke wa kuwa nae maishan. Mungu sio dhalimu utapata. Unaweza kuoa mtu mmoja akasambaratisha familia nzima. Hiz sura na makalio yasikupofushe hakuna jipya aisee. Mtwisheni Mungu fadhaa zenu mbona liko wazi. Watu wengi wanateseka coz ya kwenye maamuz ya kuoa. Kumbuka wanawake wameamka na wanaume itabid tuwe macho. Kuna maisha baada ya hela ambayo ni mateso matupu.
Nani kakudanganya maombi yanakupa mke mwema unaweza ukamuomba Mungu,shetani akawahi kujibu maombi yako.
Mke ni zaidi ya maombi pili mwanadamu ubadilika
 
'Hiz sura na makalio yasikupofushe hakuna jipya'uko sahihi sana,wengi wameumia hapo.Angalia mfano wakina Diamond,Ali Kiba,Harmonize n.k,wanajitahidi kwa pesa zao kuchukua wanawake walio wazuri ajabu,lakini baada ya muda mfupi unashangaa mahusiano yamevunjika...
Hao achana nao hawaoi hao sababu ya maagano na masharti ikiwemo mikataba waliyoingia na shetani.
Hao sio wa kutolea mfano kuhusu mahusiano.
 
Tukio lote hili limesababishwa na hela. Tangu Msuya kuuawa ni hela hadi huyu mama Miriam Mrita kuachiwa ni hela.

Bora sisi kina kajamba nani, mkono kinywani, ngono, umbea na kurogana.
Msuya ni karma ya damu alizomwaga so katimiza maandiko ukiuwa kwa upanga.Annete kadhulumiwa damu isiyo hatia.
 
Mambo ya Mahakamani mtu kufungwa ni mpaka iwe proven beyond reasonable doubts (kwahio kama ushahidi ulikuwa na mashaka hata kidogo basi mtu atakuwa hana Hatia)

It is better that ten guilty persons escape than one innocent suffer. - Ingawa na huyu kwa kukaa ndani muda wote huu hata kama alikuwa innocent inaonesha walakini katika kushughulikia haya mambo kwa haraka....

Anyway Andhaa Kanoon - Na hii sio Bongo tu bali dunia kwa Ujumla
Ukiwa masikini ushahidi unapatikana haraka sana ufungwe kama mfano WA Sheria zinafanya kazi.
Bongo kesi ni biashara.
Unadhani pale b ngapi zimetembea
 
Acha upumbafu hadhari eti wife kagoma watoto wasisome sheria

Ujinba sna umeleta hapa wife wako ndio anapanga nin mnakula na kusoma hyo familia mam ndio mwenye akili

Kwanza litoto linaweza kusoma hyo sheria na bdo akashindwa kutoboaa law school akaishi kuwa muuza duka la mangi au mtendaji wa kata

Sheria uwendi kilaza

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Vilaza wengi mbona wamejaa huko
 
Wengi walipewa ujaji kwa sababu ya kumfurahisha jiwe kuwafunga wapinzani na sio kwa sababu ya weledi wao kwenye sheria isiwe Hawa ni mmoja wao.
 
Wife wako hakuwa sawa.

Mimi nimesomea sheria na nimegundua mambo kadhaa.

1. Elimu ya Sheria ni fani kama zilivyo fani nyingine.

2. Baada ya udakari, fani ya sheria inafuata kwa umuhimu wake kwa jamii.

3. Kesi za jinai ni aina ya kesi ambazo mtuhumiwa ana uwezekano mkubwa kushinda.

4. Jamuhuri ndiyo huchukua jukumu la kufungua kesi za jinai dhidi ya mtuhumiwa/watuhumiwa.

5. Jamhuri ndiyo yenye mzigo mzito wa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mtuhumiwa/watuhumiwa.

6. Mtuhumiwa anatakiwa kuonyesha shaka kwenye ushahidi wa jamuhuri na siyo kupinga.

7. Kwenye jinai, chembe kidogo ya shaka, hata kama ni tofauti ya tarehe, itamfanya mtuhumiwa kuachiwa.

8. Katika kesi ya Miriam Mrita ushahidi ulikuwa wa mazingira na siyo wa moja kwa moja, na pia hati ya mashtaka ilikosewa na hivyo kufanya watuhumiwa kukwepa adhabu.
2. Baada ya udakari, fani ya sheria inafuata kwa umuhimu wake kwa jamii

Mkuu kwamba hizo fani ndiyo za muhimu kuliko fani yoyote Duniani????

Kwahiyo UALIMU si lolote???

Fani ya ualimu ni mama na baba wa fani zote. Hizo nyingine ndizo hufuata. Hii ni kwa maoni yangu.
 
Yaani bure kabisa! Kijana wangu aligoma kusoma hgl ili kwamba wakasome sheria pamoja na mabembelezo ya mwalimu wake akaweka wazi kabisa "mimi siwezi hizo dhulma!"
Siku ukipata janga linalohitaji Mwanasheria utajua umuhimu wa sheria.
 
Unaendaje jela wakati una hela kwa nchi ya kitu kidogo kama Tzedi?😂
Yaani yule maźa hakuwa na wacwac kabisa siku ya hukumu. Mimi nasemaje Annete huko uliko watokee wauwaji wako mpaka waende polisi wenyewe, kujisema. Sisi tulimuuwa anatutokea tunaomba tujisamishe.
 
Mawakili wa serikali hamna kitu kabisa, kesi ilikua wazi kabisa ila wanashindwa kuwa serious. Sijui nini ambacho wanaweza hawa watu!! Na hata wangeshinda kesi wangeenda kubwagwa kwenye rufaa.
Mkuu, kipi usichokielewa hapo? Mawakili wa Serikali ni aina ya watu waliojibwetesha sana. Mimi Wakili wa kujitegemea namtoza hela ndefu mteja wangu, hela hiyo ndefu ni pamoja na charges nitakazowalipaMawakili wa Serikali pindi nitakapikuwa nawapa maagizo ya watumie ushahidi upi, wauondoe upi, au waongee na kujibu nini.
Mawakili wa serikali huwa wanakuwa kwenye payrolls za watu.
Mfano ile kesi ya Mbowe unaona kabisa kuwa kilichokuwa kinapelekea Mbowe kuendelea kukaa ndani ni serikali kuamua ku deal na Majaji, kwamba inyeshe mvua au liwake jua, hakuna kumuachia. Sababu upande wa mawakili wa serikali wali flop vibaya mno, hakuna cha maana walichokuwa wakifanya.
 
Shida sio kakolaki.

Kakolaki ni mzoefu kwenye kesi za jinai kafanya miaka mingi tangia akiwa wakili aa serikali , kapitia pia tume ya kupambana na madawa ya kulevya, huko ndiko anakopajua.

Tatizo lipo kwenye upepelezi, haufanyiki vizuri, niliwahi kushauri hapa na pia tume ya haki iliyoundwa na kumpa ripoti Rais Samia ilikuja na maoni kama hayo kuwa iundwe taasisi maalum ya upelelezi wa makosa ya jinai.

Bila kufanya hivyo tutarudi hapa kulaumiana kila siku.
Kwahiyo Makonda yupo sahihi !.
 
Mkuu, kipi usichokielewa hapo? Mawakili wa Serikali ni aina ya watu waliojibwetesha sana. Mimi Wakili wa kujitegemea namtoza hela ndefu mteja wangu, hela hiyo ndefu ni pamoja na charges nitakazowalipaMawakili wa Serikali pindi nitakapikuwa nawapa maagizo ya watumie ushahidi upi, wauondoe upi, au waongee na kujibu nini.
Mawakili wa serikali huwa wanakuwa kwenye payrolls za watu.
Mfano ile kesi ya Mbowe unaona kabisa kuwa kilichokuwa kinapelekea Mbowe kuendelea kukaa ndani ni serikali kuamua ku deal na Majaji, kwamba inyeshe mvua au liwake jua, hakuna kumuachia. Sababu upande wa mawakili wa serikali wali flop vibaya mno, hakuna cha maana walichokuwa wakifanya.
Kwa hio Serekali haina mawakili bali Ina magalasa ukianza na bwana Felesi Mwanasheria Mkuu wa Serekali?
 
kwa vipi? Mbon Mungu anawaumba masikini na tajiri ie anawapa watu vipaji tofauti wengine masikini, wengine matajiri. Wengine vilema etc etc (maana tunaambiwa kla kitu kimeumbwa na Mungu). Anawaacha waovu wanatawala dunia kama hangaya and team? Hakimu wa kweli yuko wapi
Siku ya kiama kila mtu atahukumiwa sawasawa na hesabu zake

Pia Mungu anahukumu kwa kutoa laana ya vizazi na vizazi

Usishangae analipiza kwa watoto wako na wajukuu zako

Kwa hiyo do right things bila kumuonea mtu
 
Back
Top Bottom