Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya

Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia ya mauaji ya Aneth Msuya

Kwa hio wameroga?
Siwezi sema moja kwa moja wameroga au hawajaroga ila chochote kinaweza tokea Ndio! Wapo watu watasema imani potofu ndio! Kwa sisi ambao tumeshakumbana na mambo ya kesi tunajua jinsi nguvu za giza zinavyoweza badilisha matokeo na hutaamini hata kama ushaidi upo wazi.

Ni ngumu kuelewa hizo mambo unless umekumbwa na changamoto za mambo ya kesi.
Wapo humu watu JF wanajua jinsi mambo yanavoweza kwenda na jinsi ushirikina unavotumika kwenye hizi mambo za kesi.
 
Bei ya Kibatala kuwa juu au chini ya mawakili wengine haina maana kwamba Advocate Remunaration Rules hazijaweka viwango vya tozo.
Ndugu yangu ingia ngomani ujue inavyochezwa. Mwanasheria mzuri ni mtu asiye na utu hata kidogo. Ili ushinde kesi mtuhumiwa anatakiwa akuambie ukweli asilimia 100. Ili ujue unamteteaje. Nimeshuhudia kesi zaidi ya tatu nikaja kujua kuwa ili uwe mwanasheria mwenye mafanikio inabidi utu ukae pembeni. Sifa ya kuwaokoa waovu ni nzuri kuliko kutetea wenye haki. Siwapondi wala kuwachukia maana wana familia pia na watoto inabidi wale.
 
Ndugu yangu ingia ngomani ujue inavyochezwa. Mwanasheria mzuri ni mtu asiye na utu hata kidogo. Ili ushinde kesi mtuhumiwa anatakiwa akuambie ukweli asilimia 100. Ili ujue unamteteaje. Nimeshuhudia kesi zaidi ya tatu nikaja kujua kuwa ili uwe mwanasheria mwenye mafanikio inabidi utu ukae pembeni. Sifa ya kuwaokoa waovu ni nzuri kuliko kutetea wenye haki. Siwapondi wala kuwachukia maana wana familia pia na watoto inabidi wale.

Sasa wewe hoja yako ni nini?

Hata sikuelewi maana sheria hujui na practice pia huna.
 
Sasa wewe hoja yako ni nini?

Hata sikuelewi maana sheria hujui na practice pia huna.
Hoja yangu ni kuwa Kibatala amefanya kazi yake. Na amefanya kazi kwa faida yake ni si kwa haki. Na hatakiwi kulaumiwa maana ana watoto na familia. Na namalizia kwa amepiga hela ndefu kwenye kesi.
 
Nimeshangaa eti dna haionyeshi damu ni ya nani ,tuko serious kweli unachukua damu kwenye kisu na sehemu ya tukio unashindwa kuchukua damu kwenye mwili wa marehemu ufanye comparison ,au ndugu yake basi .Huu ni UHUNI
 
Hoja yangu ni kuwa Kibatala amefanya kazi yake. Na amefanya kazi kwa faida yake ni si kwa haki. Na hatakiwi kulaumiwa maana ana watoto na familia. Na namalizia kwa amepiga hela ndefu kwenye kesi.
Hiyo bado ni dhahania isiyo na uthibitisho. Wivu na husda umekujaa!
 
Hiyo bado ni dhahania isiyo na uthibitisho. Wivu na husda umekujaa!
Mimi sina wivu wala husda nimefanya kazi na mawakili wengi.Wengi wao ni marafiki zangu. Kila mtu ana majukumu na majukumu ni pesa. Simlaumu wala simchukii Kibatala maana alisoma ili awe na uwezo wa kuihudumia familia yake.
 
Kiba kavuta SI chini ya b 2 hapo kuubadilisha ukweli kuwa uwongo.
-kazi ya kiba ulikuwa ni hii kwenye ile kesi ya R vs Miriam Mrita na revocatus muyella,
(I) kwanza alipinga utaratibu uliotumika kufanya gwaride la utambuzi kwamba ulikosewa.
(II) Alionyesha kwamba First Crime Report ilimtaja mtuhumiwa mwingine tofauti na Miriam Mrita na Muyyela
(III) alipinga kwamba gari lililotumika kutenda kosa kuwa halikuhusika kwa sababu tarehe ya kosa Hilo gari lilikuwa gereji ya general Motors
(Iv) kwamba ushahidi ulichukuliwa kwa kipigo na vitisho hivyo haupokelewi mahakamani
(V)
 
Sheria fani ya uongo uongo..
Kesi moja akikutetea wakili X unaenda jela..
Lakini kesi hiyo hiyo akikutetea wakili Y unatoboa..
Kwamba wakili Y alielewa zaidi darasani.
Unajua maana ya competence?
Sheria ndio taaluma pekee ambayo watu wanabishana kwa rejea ya vifungu via sheria hata Sisi CPA tunatumia sheria zile za Tax
 
mbona hizo huku machimboni watu wanazo tena mwingine hana hata gari wala nyumba
Issue ni kwamba huna hata idea ya bei za huduma za sheria tanzania ,case kuonekana kwenye tv haimaanishi ndio umelipwa hela nyingi, kuna wanasheria huwaoni kwenye case za tv ila kazi zao za documents tu ils zinalipa sana kuliko haya ma kesi ya mauaji
 
Nani kakudanganya maombi yanakupa mke mwema unaweza ukamuomba Mungu,shetani akawahi kujibu maombi yako.
Mke ni zaidi ya maombi pili mwanadamu ubadilika
Maombi yanakupa mke mwema chief trust me. Usichanganye maombi na uovu. Maana Mungu hakai sehem chafu so kama umeamua funga omba utapewa. Kanuni ni moja tu.
Ombeni mtapewa, tafuten mtapata na bisheni mtafunguliwa. Hayo yote yanawezekana kwa aliyedhamiria sio unaomba then unaenda kununua malaya wa kugonga. Kwa asili sisi shetan hawez kutufanya chochote kama umesurender mwili na akili yako kwa Mungu. "Nasimama mlango nabisha yeyote akinifungulia mlango nitakaa kwake na nitakula nae" anitafutae kwa bidii ataniona. Chochote ukikitafuta kwa bidii unapata iwe mke mbingu utajiri nk.
 
rufaa ni haki yenu, ila hukuna ushahidi mpya,
Sawa haku na ushahidi mpya, but kuna Wrong apprehension of evidence by the Judge!
c&P: A judgment must convey some indication the judge or magistrate has applied his mind to the evidence on the record. Though it may be reduced to a minimum/it must show that no material portion of the evidence before the court has been ignored...sasa inaweza ikatokea Judge hakufanya hivyo. Hivyo anything can come out of Rufaa!
 
Bila eyewitness kesi za mauaji watu wengi sana wanashinda na unakuta ameua kweli, ndo maana serial killers wanapotekeleza mauaji huwa hawataki mtu mwingine aone na ukimuona ujue umeingia kwenye batch ya kifo na pia hawaachi ushashidi wowote kifaa anachoulia anaondoka nacho ukiona kaacha silaha aliyotumia kuulia ujue huyo siyo muuaji mzoefu
 
Back
Top Bottom