Nitoe ushuhuda wangu,
Hii kazi ya kukodisha vifaa vya ujenzi Eg, mbao za lenta, mirunda, fox, nguzo za chuma, majukwaa nk. Ni nzuri kwakuwa nami naifanya japo changamoto zipo ndogo ndogo
Eg, mbao kukatwa na mafundi, mteja kuchelewa kurudisha vifaa kama mlivyo kubaliana nk.
Hata hivyo pamoja na changamoto hizo bado inalipa. Binafsi nina miaka3 tangu nianzishe biashara hii, nakumbuka nilianza na mbao20 ila kwa sasa zimefika mbao 600 na nimefungua branch office
Lakini sikuishia hapo nilianzisha na biashara ya kuuza vifaa vya ujenzi kwakuwa ni biashara zinazoendana.
Kwa sasa namshukuru Mungu kile kilio cha ajira kwangu kimeisha kwa sasa naagalia namna gani ya kutanua biashara yangu
Haikuwa rahisi kiivyo kupiga hatua but kujituma na kuwa na nidhamu ya pesa ndio mambo muhimu.
Vijana wenzangu tupambanie ndoto zetu coz wazee wameishamaliza majukumu yao kutuleta duniani. Asanteni wote