Katika ujenzi ili kupunguza gharama ya kununua mbao mpya ambazo ni ghaliMbao za
unazitumia kufanya nini
Je kama ntaziitaji nizitumie kama kuni baadae..!?Ni hivi kuna hatua ya ujenzi(beam ya zege) inahitaji mbao ili kutengeneza shape ya hio beam sasa mbao hizi unaweza kujikuta unatumia hata 200,000 kununua na ukimaliza kazi hii hutazihitaji sasa badala ya kununua unazikodi kwa hela ndogo kama 30,000 tu. Inapunguza gharama za ujenzi.
Thank you very much Sir.Nitoe ushuhuda wangu,
Hii kazi ya kukodisha vifaa vya ujenzi Eg, mbao za lenta, mirunda, fox, nguzo za chuma, majukwaa nk. Ni nzuri kwakuwa nami naifanya japo changamoto zipo ndogo ndogo
Eg, mbao kukatwa na mafundi, mteja kuchelewa kurudisha vifaa kama mlivyo kubaliana nk.
Hata hivyo pamoja na changamoto hizo bado inalipa. Binafsi nina miaka3 tangu nianzishe biashara hii, nakumbuka nilianza na mbao20 ila kwa sasa zimefika mbao 600 na nimefungua branch office
Lakini sikuishia hapo nilianzisha na biashara ya kuuza vifaa vya ujenzi kwakuwa ni biashara zinazoendana.
Kwa sasa namshukuru Mungu kile kilio cha ajira kwangu kimeisha kwa sasa naagalia namna gani ya kutanua biashara yangu
Haikuwa rahisi kiivyo kupiga hatua but kujituma na kuwa na nidhamu ya pesa ndio mambo muhimu.
Vijana wenzangu tupambanie ndoto zetu coz wazee wameishamaliza majukumu yao kutuleta duniani. Asanteni wote
Kwenye ghorofa umekwenda mbali mno,kama una uwezo wa ghorofa huwezi kukodi mbao.hizo za kukodi mara nyingi huwa kwa kazi ya lenta,au kufunika shimo la maji taka,ni zile kazi ambazo leo umekodi ..fundi seremala anafunga leo na kumwaga zege..kesho zege unaiacha itulie,keshokuwa unafungua mbao unarudisha kwa mwenyewe.sasa zikivunjika km 6 hivi au cement iking'ang'ania huoni ni bora ungenunua zako, maana ni lazima tena utakaa nazo miezi 6 mpaka ghorofa hilo likauke la sivyo Mhandisi hatakubali
na 30,000 ni kwa siku moja au mpaka umalize ujenzi
Huna sababu ya kwenda kukodi , hapo kanunue zako tu hardware ukoke upate moto. Maana hizo za kukodi utalipishwa bei ya mbao mpyaJe kama ntaziitaji nizitumie kama kuni baadae..!?
Kwa kweliHiyo ndo mipango yenyewe ya mjini!
Hadi mtu awe na hiyo iPhone aje afanye biashara ya kukodisha mbao😂😂 bongo bhana....Sio wote wana eneo la kuhifadhi hizo mbao. Wewe unaizungumzia tu hela ya iPhone inayonunua mbao lkn husemi kiwanja hicho ambacho jamaa kajenga na kaweka hizo mbao
Yale Yale ya kilimo cha nyanya kinalipa ingia sasa shambanibiashara ya kuhadisiwa inalipa sana
Ulimkata vibao ama[emoji23][emoji23][emoji23]maana majamaa wanakera kwa kiwango cha juu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mi Ndo maana fundi alinikimbia
Kuna watu hawapendi kubaki na makorokoro ya ujenzi akishamaliza.Unapima risk wewe mwenyewe. Kwangu ni nafuu kukodi. Kuvunjika sio rahisi sema fundi azikate na mara nyingi mafundi wanajua masharti ya mbao za kukodi.
Kuna wakati unatakiwa kusimama kama mwanaume.Basi fundi wangu aliniibia
Nikamwambia tuchukue za jamaa yangu akasema hazifai tununue mpya
Inawezekana alienda kuchukua kwa mtu wake tu zilizotumika, maana sikuziona kama mpya sana
Watu wanaweza kuona mtu yupo tu kumbe ana mazaga yake anayakodi kimya kimya.Fursa za aina hii hazionekani kirahisi na watu.
Mwaka wa pili sasa nakodisha tablets, voice recorders, gps devices kwa ajili ya wale wanaoenda mikoani kukusanya data.
Tablet 1 ananilipa 5000 kwa siku. Na huwa wanachukua minimum siku 10 na wanachukua arround tablets 10.
Kukiwa na survey hata 3 kwa mwezi sikosi 1M. Ukipoteza unalipa mpya.
Hapo sijaongelea voice recorders na gps.
Mzee wangu ana duka lake la ujenzi.Kiwanja cha nini?
Mimi nilipokodi ametengeneza kama kichanja
Mbao zinapangwa kwenda juu
Mbao moja 1000 ukikata au kupasua unalipa na kuna kipande kukata hakuepukiki
Naishi mbali kidogo na eneo husika, sasa hapo site kuna jamaa yangu pia amejenga akaniambia tuchukue kwake, ili kuokoa muda nikamtuma fundi akaziangalie kama zinafaa akasema hazifai kabisaKuna wakati unatakiwa kusimama kama mwanaume.
Unapofanya maamuzi, fundi anatakiwa akae kimya na kutekeleza.
Wewe umemwambia akodi anataka kununua, nani bosi hapo? Kazi hake ni ufundi na sio kukuambia jinsi ya kutumia pesa zako.
Wewe ungeenda kukodi na kumletea hapo site na kumwambia afanye kazi iliyomleta hapo.