Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Mifumo ya kiuongozi ndio ipo hivyo ukileta ujuaji unabemendwa hakuna jipya hapo
 
Logical non sequitur fallacy.

Hataishi milele ila Magufuli katangulia kufa kamuacha afande analifaidi jua bado.

Magufuli na mabobish yake yote ya "Naweza kukuvua manyota" hayakumsaidia kukishinda kifo.

Cheo ni dhamana, usikitumie kujimwambafy na kutishia watu.

Duniani wote tunapita tu.
Kutangulia kufa si ushindi kwa upande wa pili,

Kinacho matter ni quality ya life uliyoiishi kwenye mapito yako je umeacha alama gani itayokufanya uwe na amani huko uendako.
 
Hoja imetoka kwa mtoa hoja we una Tatizo la Akili kama uamini nenda hospitali kapime alafu lete hapa majibu.

Wewe hujui tofauti ua "uamini" na "huamini".

Huwa siwaamini watu wasiojua kuweka h kwenye sehemu inayotakiwa katika Kiswahili.

Pamoja na wanaochanganya l na r.

Huna hata lugha ya kuweza kufanya mjadala na mimi.

Hawa watu wengi ni Walugaluga wasiojua hata Kiswahili, siwezi kufanya nao mjadala wa kimantiki.
 
Kutangulia kufa si ushindi kwa upande wa pili,

Kinacho matter ni quality ya life uliyoiishi kwenye mapito yako je umeacha alama gani itayokufanya uwe na amani huko uendako.
Ukishakufa umekufa hakuna kuwa na amani huko uendako, labda useme kuacha amani hapa duniani.

Magufuli kaacha majanga hapa duniani, hajaacha amani.
 
Ukishakufa umekufa hakuna kuwa na amani huko uendako, labda useme kuacha amani hapa duniani.

Magufuli kaacha majanga hapa duniani, hajaacha amani.
Kuacha amani duniani YES NDIO POINT.

Kupata habari za mtu siku zote huwa zina pande mbili sasa inategemea umechagua upande gani kuusikiliza. Na upo sahihi kulingana na upande uliouchagua kuusikiliza.
 
Kuacha amani duniani YES NDIO POINT.

Kupata habari za mtu siku zote huwa zina pande mbili sasa inategemea umechagua upande gani kuusikiliza. Na upo sahihi kulingana na upande uliouchagua kuusikiliza.
Pande zinaweza kuzidi kuwa hata zaidi ya mbili.

Lakini tunaweka pande zote kwenye mizani halafu tunapima upande gani umezidi.

Na Magufuli ukimpima objectively, utaona kaharibu sehemu nyingi kuliko alivyotengeneza.

Lakini, watu wengi hawapendi kupima vitu objectively, wanapenda kwenda kwa hisia kumpaisha Mzee wa Show za Kibabe.

Wanapenda kwenda kwa hisia zaidi, kama mwamba wao. Ndiyo maana wanamkubali sana tu.
 
Yule mfungwa akaendelea kusema..Ni kwambie UKWEL DR.MAGUFURI UKIONDOKA HAPA UONDOKE NA MIMI MAANA NTAUWAWA....NIKWAMBIE DR. MAGUFURI HAWA WANA MBINU NYINGI WATATUMIA HATA MA DACTARI WAKUUE KWA SINDANO YA SUMU
Watu wanaomuliza raisi maswali ya papo lwa papo au kuibua kero za eneo husika wote wanakuwa wamepangwa kabla. Raisi haulizwi swali na yeyote popote pale.
Haijawahi kutokea na haitatokea raisi kufanya ziara ya kustukiza lazima iandqliwe.
So jamaa alikuwa target na yule mfungwa yawezekana ni wa MAKUMBUSHO Alipelekwa pale kwa kazi maalumu
 
Pande zinaweza kuzidi kuwa hata zaidi ya mbili.

Lakini tunaweka pande zote kwenye mizani halafu tunapima upande gani umezidi.

Na Magufuli ukimpima objectively, utaona kaharibu sehemu nyingi kuliko alivyotengeneza.

Lakini, watu wengi hawapendi kupima vitu objectively, wanapenda kwenda kwa hisia kumpaisha Mzee wa Show za Kibabe.

Wanapenda kwenda kwa hisia zaidi, kama mwamba wao. Ndiyo maana wanamkubali sana tu.
Naona unakomaa kupambana na hayati.
 
Kuna uonevu wa kiaina ulifanywa mwingi sana,tatizo tukimpenda hata marehemu,hatupendi aambiwe ukweli,au akosolewe.Kuna doctor pale Tabora alishughukiwa kisa alienda hospital binafsi kufuata maslah kwa ajili ya maisha yake.Baba akasahau aliacha ualimu akaingia kwenye siasa.Tuamini ya Mungu ni mengi
Mkuu unapotetea vitu angalia na upande wa pili , ebu fikiriq huyo mfungwa kaamua kujitoa muhanga unahisi kapitia mangap aliyoshindwa kuyameza moyon , ukute ata wanafir@ wafungwq , rudi Kwa daktari wako , kwenda private sio shida ila shida ni kuiba wagonjwa serikalini kupeleka private , kuharibu mashine za serikalin ili private zenu zifanye , mm nmekaa kwenye kada ya afya Kwa muda mrefu nimeiona sio kuhadithiwa , ukitaka Haki na ww tenda Haki

Marehem alifanya Kaz yake bila UNAFIKI , shukuruni hizo pesa za dhuruma mlizipata Kwa wiz kabla ya marehem , maana marehem alifuata Sheria na sio hisia kama mnavyotaka nyiny , UONEWE HURUMA KISA UNATAAFUTA KIPATO CHA ZIADA KWA NJIA HARAM ILA UKISIKIA MWIZ UNAMCHOMA MOTO INGAWAJ NA YEYE ANATAFUTA PESA KWA NJIA HARAM
 
Wewe hujui tofauti ua "uamini" na "huamini".

Huwa siwaamini watu wasiojua kuweka h kwenye sehemu inayotakiwa katika Kiswahili.

Pamoja na wanaochanganya l na r.

Huna hata lugha ya kuweza kufanya mjadala na mimi.

Hawa watu wengi ni Walugaluga wasiojua hata Kiswahili, siwezi kufanya nao mjadala wa kimantiki.
Hapo kwa "watoto" wenye lugha za "kikuda" sijui mara apo kwenye hapo ,uamini badala ya huamini nimekuunga mkono,japo kwenye matumizi ya neno walugaluga ndio nimekuona "umepuyanga" ,lugha nyingine ni za "kimajinuni", Walugaluga ni Askari shupavu wa kukodiwa wa utawala wa kichifu wa unyanyembe enzi hizo,Sasa sijajua kwanini "wafuata upepo" wawahusishe na watu wa hovyo
 
Mkuu unapotetea vitu angalia na upande wa pili , ebu fikiriq huyo mfungwa kaamua kujitoa muhanga unahisi kapitia mangap aliyoshindwa kuyameza moyon , ukute ata wanafir@ wafungwq , rudi Kwa daktari wako , kwenda private sio shida ila shida ni kuiba wagonjwa serikalini kupeleka private , kuharibu mashine za serikalin ili private zenu zifanye , mm nmekaa kwenye kada ya afya Kwa muda mrefu nimeiona sio kuhadithiwa , ukitaka Haki na ww tenda Haki

Marehem alifanya Kaz yake bila UNAFIKI , shukuruni hizo pesa za dhuruma mlizipata Kwa wiz kabla ya marehem , maana marehem alifuata Sheria na sio hisia kama mnavyotaka nyiny , UONEWE HURUMA KISA UNATAAFUTA KIPATO CHA ZIADA KWA NJIA HARAM ILA UKISIKIA MWIZ UNAMCHOMA MOTO INGAWAJ NA YEYE ANATAFUTA PESA KWA NJIA HARAM
Wacha uwongo dogo!! Magufuli alikuwa mtu wa dhuluma tu. Hajawahi kufuata sheria yeyote
 
Hapo kwa "watoto" wenye lugha za "kikuda" sijui mara apo kwenye hapo ,uamini badala ya huamini nimekuunga mkono,japo kwenye matumizi ya neno walugaluga ndio nimekuona "umepuyanga" ,lugha nyingine ni za "kimajinuni", Walugaluga ni Askari shupavu wa kukodiwa wa utawala wa kichifu wa unyanyembe enzi hizo,Sasa sijajua kwanini "wafuata upepo" wawahusishe na watu wa hovyo
Walugaluga ni watu wa makabila tofauti waliofikia sehemu fulani, hawajui hata lugha ya pale vizuri, ndiyo maana wanaitwa "walugaluga".

Hao Walugaluga original walichukuliwa jeshi la Wanyamwezi kutoka makabila tofauti kama Wakonongo, Wanubi etc wakalowea kwa Wanyamwezi.

Sasa hawa walugaluga wa siku hizi nao hawajui Kiswahili wanatuharibia lugha yetu.
 
Back
Top Bottom