UPDATE: FRIDAY 21ST OCTOBER 2022
MAELEZO YA NYONGEZA KUHUSIANA NA BINTI ALIYEONEKANA KANISANI J2 ILIYOPITA; AMBAYE ALIWAHI KUISHI KWA MAMA WA KIROHO WA MHUSIKA ANAYEISHI (MAMA WA KIROHO ) JIRANI NA MHUSIKA
Rasmi mhusika na binti huyu walifahamiana mwaka 2008, kipindi ambacho mhusika alikuwa ametembelewa na wageni wawili; ambao walikuwa ni mama yake mzazi na mdogo wake (mhusika)
Wageni hawa wawili hawakuwa wamemtembelea mhusika isipokuwa mama mzazi wa mhusika alikuwa amemleta mdogo wa mhusika (RIP) kwa ajili ya tiba; mtu huyu alikuwa na tatizo la kiafya; alikuwa ameambukizwa TB
KWA KUKUMBUSHIA TU BAADHI YA MAMBO MUHIMU AMBAYO MHUSIKA TAYARI ALISHAWAHI KUYALETA HUMU JUKWAANI
Baada ya wageni hawa kuwasili nyumbani kwa mhusika mnamo August 2008, mhusika aliamua kuchukua likizo
- Kipindi hicho mhusika alikuwa anaishi peke yake nyumbani kwake na baada ya wageni kuwasili, nyumbani kwa mhusika kukawa na watu watatu
- Pale mwanzoni mwa likizo hiyo, mhusika akaunganishiwa “dili” la kazi ya kwenda kufanya mikoani, nje ya Dar es Salaam, ambayo details zake alishawahi kuzileta humu kupitia baadhi ya maelezo yaliyopo kwenye post hii hapa #113
- Kwenye post hiyo, mtu aliyemuunganishia kazi hiyo anam-refer kama MR T, staff-mate wa mhusika; ofisi tofauti, jengo moja la ofisi
Pasipo mhusika kuwa anajua chochote kile kwa wakati huo, anachokijua na alicho na uhakika nacho muda huu ni kwamba MR T (aliyemuunganishia kazi mhusika) na MAMA WA KIROHO WA MHUSIKA (tumwite MKM) walikuwa na mawasiliano
Mhusika akiwa yupo likizo nyumbani kwake pamoja na wageni wake wawili, MR T (
staff-mate) alimuunganishia kazi mhusika ambayo ilikuwa na sifa hizi zifuatazo
- Ilikuwa inafanyikia mkoani
- Usafiri wa kwenda na kurudi ulikuwa ni wa ndege
- Mwenye kazi alionekana kuwa ni mgeni ambaye hakuwa mTanzania;
- Na kama alikuwa ni mTanzania, basi atakuwa alizaliwa hapa na wazazi ambao hawakuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa; waliozaliwa nje ya Afrika
- Siku mhusika ameenda kunaonana na mwenye kazi ofisini baada ya kuwa amepewa appointment ya kufanya hivyo, baadhi ya wafanyakazi wake waliokuwepo maeneo yale ofisini walimjulisha mhusika kuwa tiketi ya usafiri wake wa ndege ilikuwepo tayari
Wakati wanaachana na mwenye kazi, siku mhusika alipokwenda kupewa details za kazi, mwenye kazi alimpa mhusika kitabu cha mambo ya OCEANOGRAPHY, ambacho author ni yeye mwenyewe (tumwite AUTHROR).
Miezi kadhaa mbele, kitabu hiki kilikuja kupelekea mhusika kufahamu kuwa AUTHOR na MKM walikuwa wanafahamiana
“PLOT” YA NAMNA YA SAFARI HIYO YA KIKAZI (HAIKUFANYIKA) ILIVYOTAKIWA KUWA
Mhusika hakufanikiwa kuifanya safari hii kutokana na sababu kadhaa zifuatazo
Ilionekana alitakiwa au alitarajiwa angesafiri bila kuaga ofisini kazini kwake kisa tu alikuwa yuko likizo, kitu ambacho hakuwa tayari kukifanya
Na kama angesafiri kwa kuondoka tu bila kuaga kazini kwa sababu alikuwa yupo likizo,
Chochote kile ambacho kingeweza kumtokea akiwa yuko huko kwenye kazi hiyo, mamlaka za ofisini kwake zisingehusika kwa sababu ukiachilia mbali kuwa alikuwa yuko likizo, mamlaka hizo zisingekuwa na taarifa za kazi hiyo
Mbali na hilo, baadhi ya watu ikiwa ni pamoja na majirani, wasingejua kama mhusika amesafiri kwa sababu kadhaa kama ifuatavyo
- Wangeendelea kuliona gari lake lipo nje likiwa limepaki
- Wangeendelea kuona taa za nyumbani kwake zikiwashwa na kuzimwa usiku unapoingia
Na kwa sababu watu wote wanaomfahamu walikuwa wanajua kuwa mhusika huwa anaishi peke yake, basi kwa dalili hizo wangejua kuwa mhusika yupo nyumbani kwake, na ndiye huwa anazima na kuwasha taa usiku unapokuwa umeingia!
Kumbe wakati huo mhusika angekuwa amesafiri kwa ndege kuelekea mkoani, nyumbani kwake akiwa amewaacha wageni, na ofisini akiwa hajaaga
Hiki ndicho kilichopelekea mhusika asiende kufanya kazi hiyo; AUTHOR alishindwa kumpa kazi mhusika baada ya kuona kuwa mhusika alitaka aondoke akiwa ameaga ofisini
Baada ya kunyimwa kazi hiyo miezi kadhaa mbele (wageni wakiwa tayari walishaondoka), mhusika alikuja kupata taarifa za mambo mawili muhimu ambayo hapo kabla, hakuwahi kuwa na taarifa zake
TAARIFA MUHIMU YA KWANZA
Ni kwamba mtu huyu ambaye mhusika mpaka huu mhusika anadhani kuwa hakuwa raia na ambaye ailitaka kumpa kazi (mhusika), yaani AUTHOR; mtu huyu alikuwa anafahamiana na mama wa kiroho wa mhusika (MKM)
- Taarifa hizi mhusika alizipata kutoka kwa MKM mwenyewe, siku moja majira ya baada ya saa moja usiku, baada ya MKM kutembelea kwa dharula nyumbani kwa mhusika
- Siku hiyo usiku huo, ilikuwa ni mara ya pili kwa MKM kufika nyumbani kwa mhusika, na mara ya kwanza MKM aliwahi kufika pale ilikuwa ni miaka kadhaa na kwa APPOINTMENT; alikuja kusalimia mgeni
Safari hii ya pili MKM hakufanya appointment na hivyo ilikuwa ni dharula kidogo, ukiangalia pia muda ambao aliuona kuwa ni muafaka kufika nyumbani kwa mhusika
TAARIFA MUHIMU YA PILI
Binti aliyeonekana kwa muda tu Kanisani J2 iliyopita na hatimaye kutoweka tena (tumwite BNT), yeye kwa wakati huo, alikuwa anafika mara kwa mara nyumbani kwa mhusika katika kipindi chote cha miezi mitatu ambayo wageni wa mhusika walikuwepo nyumbani. Hata hivyo, mhusika hakuwahi kulijua hilo isipokuwa baadaye muda mrefu uliwa umeshapita huku wageni wakiwa tayari walishaondoka. Kwa hiyo katika kipindi chote hicho, BNT na mhusika hawakuwahi kukutana nyumbani kwa mhusika
- Hata hivyo, kwenye mazingira ya nje, mhusika na BNT walikuwa wanaonana mara kwa mara, ila BNT hata siku moja hakuwahi kumweleza mhusika kuwa wakati mwingine huwa anafika nyumbani kwake (mhusika) kwa ajili ya kumsalimia mgonjwa
- Kwa hali hiyo katika kipindi chote cha miezi mitatu, mhusika hakuwahi kujua kabisa kama BNT aliwahi kukanyaga nyumbani kwake hata mara moja, wala BNT naye hakuwahi kumweleza mhusika chochote kuhusiana na hilo
Kwa hiyo mpaka hapa mtu anawexa kuona kuwa angalau kulikuwa na usiri fulani wa namna BNT alivyokuwa anafika nyumbani kwa mhusika
MKM na mhusika ni majirani wanaoishi Ma-block tofauti, isipokuwa kwenye lile block la mhusika, kulikuwa pia na jirani mwingine, aliyekuwa anaishi kwenye nyumba iliyo juu ya ile ya mhusika, na ambaye baadaye ilikuja kusemekana kuwa alikuwa ni ndugu wa damu wa BNT japo BNT alikuwa hakai kwa huyo ndugu yake; alikuwa anakaa kwa MKM
- Kutokana na hali hiyo BNT alikuwa akifanya visits za mara kwa mara sana kwenye block la mhusika kutokana na ukweli kuwa kwenye block hilo kulikuwa pia na ndugu yake wa damu
- Kwa hiyo possibly kwa majirani walio wengi walikuwa wakimuona BNT akielekea kwenye block la mhusika na kujua kuwa alikuwa anaelekea kwa ndugu zake; kumbe wakati mwingine alikua anaelekea nyumbani kwa mhusika kwenda kumsalimia mgonjwa
Mgonnjwa alikuwa na TB ambayo baada ya miezi mitatu, alipona na kurudi nyumbani kwake akiwa salama, na tiba yake ilikuwa ni ya bure kupitia Kituo cha Afya cha Taasisi anayofanyia kazi mhusika
Taarifa hizi kuhusiana na ugeni wa BNT nyumbani kwa mhusika, mhusika alikuja kuzipata baadaye kutoka kwa (aliyekuwa) mgonjwa mwenyewe ambaye alikuwa anatembelewa na BNT; kipindi kirefu baadaye mgonjwa akiwa tayari alisharejea mwakwao mwanza
Mpaka hapa inaonyesha wazi kabisa kuwa katika kipindi chote cha miezi mitatu, BNT alikuwa yuko
somehow programmed katika namna ambayo alikuwa anafika nyumbani kwa mhusika katika muda ule tu ambao alikuwa anakuwa ana uhakika kuwa mhusika hayupo nyumani.
……………………….inaendelea