Hivi yule jamaa alikua anaitwa Chizi Maarifa aliendaga wapi? Kuna kipindi story za namna hii msimuliaji anasimulia na hamalizi story yake anasuasua kwa kuleta vipande vifupi vifupi, utamsikia chizi maarifa amemtag msimuliaji na kumwandikia ujumbe kwa maandishi ya herufi kubwa
"NIMELETEWA MALALAMIKO NA WASOMAJI WA HADITHI ZAKO, WANADAI UNASUSUA KUMALIZIA HADITHI UNAYOWASIMULIA. IKIFIKA LEO JIONI SAA KUMI NA MBILI KAMILI UMALIZIE HADITHI YAKO YOTE... SITEGEMEI KULETEWA MALALAMIKO TENA. USIPOFANYA HIVYO NITAKUCHUKULIA HATUA KALI SANA"
Ilifikia kipindi waleta story wengine walikua wanazira kabisa kumalizi story zao kutokana na maneno ya shombo kutoka kwa Chizi Maarifa, so ilikua inafikia stage wasomaji wanamwomba mwandishi aendelee kusimulia hadithi huku wakimwomba Chizi Maarifa akae kimya asiwaharibie story yao π
π€£π
Kipindi story zinaletwa hapa jukwaani Chizi Maarifa alikua anakula ban sana kutokana na hizo issue.