Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Jamani nina swali tuu. Kwani hizo hospitali wanatibiwa watu wa kanisa tu? Ni watu wa imani moja tuu ndiyo wanatibiwa hapo?

Tukienda mfano Bugando, KCMC na nyinginezo pale mbona watu wengi tu wanatibiwa pale. Na hospitali hizi zimekuwa msaada kwa watu wengi tena wa aina zote za kiimani. Hivyo sioni shida kuchangia huduma za kiafya, vinginevyo kama alivyosema mdau mmoja hapo juu basi serikali iboreshe huduma zake za afya badala ya kutegemea sekta binafsi. Ni maoni🙏🏾.
 
Mkataba wa bandari nao unahudumia kama hivyo na hautoishia kuhudumia watanzania tu bali nchi zote za kusini na kati ya Afrika.Jambo zuri zaidi ni kuwa kuna fedha nyingi kuliko vyanzo vyote vya kipato zitakuwa zinaingia serikalini.
Kinyume na huo mkataba wa kanisa kumbe wanachukua peke yao tu
 
Nakuelewa sanaa. Kikubwa tu yale mapungufu ambayo yanapigiwa kelele ndiyo yarekebishwe. Uwekezaji mzuri una faida hilo linajulikana. Serikali isipuuze maoni ya watu mbalimbali wanayotoa kutokana na mkataba huu wa bandari.
 
Na kwa mujibu wa JPM, hospitali za wilaya alikuwa anajenga kwa Tshs. 1.5 Bilioni. Kwa hiyo shilingi bilioni 30 ni karibu kujenga hospitali 20 hivi kwa mwaka, mwaka unaofuata unanunua vifaa tiba, na kuajiri wahudumu. Aisee, hii mikataba ya ajabu sana
 
 

Attachments

  • B2AD51DB-AAC3-479B-A81F-810AAD713CBD.jpeg
    54 KB · Views: 4
Mikataba iliyopitishwa wakati wa JK hii hapa na madhara yake haya hapa
 

Attachments

  • 24C68573-5083-449C-AEF7-9AB80D1FBBEC.jpeg
    47.7 KB · Views: 4
Wanatibiwa watu wote ila bei zake ni za juu sana. Hata wakristo wanaumizwa na hizo hospital.

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Sjaona dini ya kishamba kama hii hivi unasemaje mkataba wa kunyonya nchi wakati serikali inatoa pesa ili wananchi wapate huduma. Alafu mlishukuru sana kanisa katoliki mzungu hakua tayari kumpa nchi muislamu. Kama historia ilikupita watafute wazee wakupe ukweli
 
Mm nilifikiri kwamba na nyie mmejenga hospitali za rufaa then serikali ikakataa kuwapa hyo Mou mnayo imba kila siku. Kumbe ni maneno maneno maneno tu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…