Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Uko sahihi hata Mimi hiyo MoU Nataka mara moja isitishwe.Hili siyo ombi bali ni tamko kuelekezwa serikali ya Tanzania kuhusu MoU ya serikali na kanisa.
Tunaitaka serikali ifute MoU hiyo na fedha zinazopelekwa kanisani zielekezwe kwengine.
Kwa sasa Tanzania ilipofikia hakuna sababu ya kubaki na kutimiza yaliyomo kwenye MoU hiyo. Ikiwa huduma za afya, hakuna hospitali isiyotoza pesa kwa huduma hizo. Kwa hiyo serikali haina tena sababu ya kuelekeza pesa hospitali za kanisani.
Ikiwa ni elimu, Tanzania imetangaza elimu bure kwa wote mpakamwanafunzi anapofikia kiwango cha elimu kwa kukopeshwa. Na hapa hakuna tena sababu ya serikali kuelekeza pesa kwa watoa elimu wa kanisa.
Soma zaidi:
- MoU kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini
- Kweli huo mkataba kati ya serikali na mashirika ya dini hauna ukomo wakati wenyewe wanatoza pesa raia kwenye hizo hospitali na shule zao?
Lakini pia Chuo cha Tanesco Morogoro kirudishwe serikalini mara moja maana kimejengwa Kwa Kodi za watu wa dini zote.