Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Tatizo ambalo tumeliona kwenye historia ya "Tanganyika" tunaliona kwenye hili vile vile. Kuna mambo ambayo hayana utata kwamba yametokea. Yapo kadhaa ambayo hayana ubishi:

1. Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya makubaliano na taasisi za kidini kwa ajili ya huduma za kijamii.

- Mwaka 1991 Julai - Serikali iliingia makubaliano na taasisi ya kidini ya Aga Khan katika kile ambacho kiliitwa "Accord of Cooperation". Mkataba huu uliboreshwa zaidi na Mkapa mwaka 2001 ambapo taasisi ya Aga Khan ilipewa hadhi ya kidiplomasia. Na katika shughuli zake kama zilivyo za Kanisa hailipi kodi. Makubaliano haya ndio yaliifungua Aga Khan kwa namna ya pekee kuweza kuingia nchini na kujishughuliisha na shughuli mbalimbai - za faida na zisizo na faida (na kwa uelewa wangu katika zote hailipi kodi - niko tayari kusahihishwa). Aga Khan ni taasisi ya dini ya Kiislamu inayoongozwa na Imam Aga Khan mkuu wa madhehebu ya Ismailiya. Kwa Tanzania ni Aga Khan ndiye aliyekuwa muasisi wa taasisi ya East African Muslim Welfare Society ambayo imekuwa ikitajwa mara kwa mara. Kwa hiyo. Mkataba wa 1991 uliingiwa chini ya Rais Muislamu mzee Mwinyi na uliboreshwa mwaka August 2001 chini ya Mkapa Rais Mkatoliki. Wote wawili hawakuona tatizo la serikali kuingia ushirikiano na taasisi ya kidini. Ikumbukwe katika maboresho ya 2001 yaliwapa kinga watendaji mbalimbali wa Aga Khan nchini kama mabalozi (though limited immunity).

Mwaka 1992 - serikali hiyo hiyo ikaingia mkataba na makanisa ambao umejadiliwa hapa. Ikumbukwe wakati Serikali ya Mwinyi inaingia mkataba na Makanisa kuhusiana na huduma za kijamii tayari ilikuwa imeshaingia mkataba na Taasisi ya Kiislamu kwa ajili ya suala la huduma za kijamii vile vile. MoU hautoki kinga yoyote ya kidplomasia kwa watendaji wa makanisa kama ilivyo kwa Aga Khan.

Mwaka 2004 - SErikali ya Benjamin Mkapa (Mkatoliki) iliikabidhi rasmi majengo ya serikali ya kule Morogoro kwa taasisi binafsi ya Muslim Development Trust ambayo yamegeuzwa kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu. Majengo ya serikali kupewa bure taasisi moja ya kidini lingeweza kusababisha mgogoro kwenye nchi nyingine lakini katika Tanzania hakukuwa na tatizo kwani ilijulikana chuo hicho kitawafaa Watanzania wote. Wanafunzi wanaosoma shahada ya Ualimu hapo MUM wanalipiwa na serikali na kwa kadiri ninavyojua - nitasahihishwa - kiasi kikubwa cha kuweza kuendesha Chuo hicho Kikuu kinatokana na wao kupokea wanafunzi wa Ualimu ambao wanalipiwa na serikali.

Haya yote yanatuambia nini?
 

Mfumokristo at work........!
 

Tabu yako ukibanwa kwa hoja huwa unakimbilia matusi, huko hunipati ng'o???? Endelea kubwabwaja humu JF na data za kupika na kufikirika!! Ila kumbuka ukibandika uongo tu records will always be set straight. Na nikikusoma btn the lines wewe si mlipa kodi hahaha ahahaha ahahahah!!!!!! Hiyo PAYE niliyokutolea mfano ya wafanyakazi wa Barrick unaita hearsay kwa sababu huipendi au? Halafu kumbuka hao samaki mifupa wanapatikana feri sio viwanjani mkuu tehetehetehe!!!!!!
 

MS

Mbona unaongea pumba shekhe???Mbona unapotosha watu pasi na sababu?Mbona Waislamu mnapenda kulialia na kulalamika kuwa mnaonewa kwenye nchi hii wakti siyo kweli. Unaposema nchi hii inaongozwa na mfumoKristo ati kuwa Kanisa Katoliki ndilo linaendesha nchi hii ni maneno ya KIZUSHI,KINAFIKI,KIPUUZI na yasiyo na MANTIKI!

Leo hii Tanzania@50 MARAIS wote na MAKAMU wake ni WAISLAMU, hapa namaanisha kwa TZ-BARA(Tanganyika) na TZ-VISIWANI(Zanzibar)! To be honest ukija kwenye ORODHA ya Mawaziri,M/Waziri,Makatibu Wakuu,Wakuu wa Mikoa/Wilaya,Wakuu wa Vyuo Vikuu,Vyuo Kati na Sekondari kwa sasa utagundua kuwa the majority of them are MUSLIM! Sasa haya malalamishi ya MFUMOKRISTO yanatoka wapi???? Hapa kiukweli hakuna nguvu ya hoja badala yake kuna hoja ya nguvu!

Unasema hakuna hoja ambayo WAISLAMU wanaweza kuileta mbele ya Serikali ikaakaa na kuijadili! Ebo,hivi HIKI KINACHOENDELEA SASA KUHUSU MAHAKAMA YA KADHI ni propaganda au nini? JK kesha wapa go ahead kuendelea na hoja yenu ya KADHI.Sasa manataka nini zaidi Waislamu wa Tanzania???Mimi huwa siwaelewi enyi watu! Hivi Waislamu mna matatizo gani hasa kwenye bongo zenu na Imani yenu??? Tuambieni tuwasaidie. Maana hizi kelele mwisho wake sana sana ni kuishia na KUJIUNGA na AL-SHAABAB na AL-QAEDA!! Ndiyo. Huko ndiko mnakotaka kutupeleka! hizi kelele si bure kuna kitu nyuma yake!!!

Marehemu Dikteta Muamar Ghaddafi katoa michango chungu mbovu kwa Tanzania ikiwemo kujenga MISIKITI mikubwa kuko DODOMA na DAR. Wewe unalalamika kuwa miaka ya 1990s Daruliman wa SAUDIA ARABIA alitaka kujenga shule ya Kiislamu akakataliwa na kuishia kufunga ofisi zake Dar. Swali ni je tangu hiyo miaka ya 1990s mpaka leo hii 2011 kuna shule ngapi za Kiislamu zimejengwa na ngapi zimekataliwa. Je,kuna Vyuo Vikuu vingapi vya Kiisalmu vimejengwa na vingapi vimekataliwa????

Madai yako kuwa mwaka 2002 Serikali kupitia Bunge ilipitisha Sheria ya Kupambana na Ughaidi nchini IKIWALENGA WAISLAMU ni uzushi na uongo wa kutaka kuipotosha jamii. Pengine tukuulize wewe mwenyewe kwenye Sheria hiyo wametajwa Waislamu kuwa ndiyo walengwa???Kwanini unajihisi kuwa wewe ni sehemu ya huo ughaidi?????Hapa ndipo kwenye maneno. Kila mtu duniani anajua kabisa mahali popote duniani watu wanaoendesha ughaidi wanakuwa na asili ya Arabuni na wengi wao wana IMANI YA KIISLAMU! Al-qaeda,Al-Shaababi,Hizbollah,Black September na wengineo wana asili ya Arabuni na ni Waislamu! Saadamu Hussein.Osama bin Laden,Muamar Ghadaffi, Mohamed Boudia na wengineo walikuwa ni viongozi wa vikundi vya Ughaidi au Wafadhili wa vikundi hivo. They are Muslim! Kwanini serikali yoyote duniani inapoandaa mkakati wa kupambana na magaidi hawa wasifikirie mara mbili kuhusu IMANI ya watu hawa???

Frankly speaking, IMANI ya KIISLAMU is questionable mahali popote duniani! Kama mtu(muumini wa dini) anafundishwa juu ya KUJIUA na KUUA WENGINE KWA KUJILIPUA NA MABOMU kwa imani kuwa anaenda peponi na akifika huko peponi atakuta WANAWAKE WAZURI 70 BIKIRA WANAMNGOJEA wawe wake ataacha kweli kuwalipua wenzake kwa imani hiyo ya kipuuzi??? Hizi siyo hadithi ni ukweli ambao tunaushuhudia huko IRAQ,AFGHASTAN,PAKISTANI,PALESTINA na nchi nyingine nyingi za Kiislamu!

Napenda nimalize kwa swali moja kwako MS: JIHAD ni nini na nini madhumuni yake kwa Waislamu???

Nitaendelea.
 
Kanisa Katoliki na Taasisi zingine za dini ya Kikristo ziliadhirika sana wakati wa kutaifisha mashule na hospitali bila serikali kulipa fidia yoyote. Wakati huo hapakuwa na MOU kati ya taasisi hizo za kidini na Serikali.

Baada ya serikali kushindwa kuendesha mashule na hospitali kwa ufanisi kama ilivyokuwa kabla ya kutaifishwa na serikali kushindwa kujenga shule na hospitali ili kukidhi mahitaji, serikali ikaomba taasisi za kidini kushiriki katika kutoa huduma za elimu na afya.

Katika hali hii, taasisi makini lazima zikae na serikali na kuona jinsi zitakavyoshiriki katika kutoa huma za elimu na afya na hiki ndio chanzo cha MOU hii. Ifahamike kwamba taasisi za dini ya kikristo zimewekeza sana katika elimu na afya na inawezekana kabisa hapo baadaye ikawekeza zaidi kuliko serikali kama bado haijakuwa hivyo.

Ili kulinda masilahi yao katika uwekezaji huu lazima kuwe na makubalioano na serikali katika hili ambalo ni jukumu la serikali na sio la dini ya Kikristo. Kwa maoni yangu hili ni jambo la kwaida kabisa kwa nchi ambazo serikali zao hazina dini na zenye mchanganyiko wa dini mbalimbali kama Tanzania.

Naamini serikali haijafunga milango kwa dini ya Kiislamu kuhusu maslahi yake katika uwekezaji katika elimu an afya hivi sasa na hapo baadaye.
 
Shehe Mohamad na wote wenye mtizamo unaofanana wa wako, tafadhali soma Gazeti la Mwanahalisi la leo tarehe 2/11/2011 namba ISSN: 1821-5432 toleo namba 266 ukurasa wa 3 Kichwa cha Habari: Majeraha ya udini yataangamiza taifa
 
Tujiulize kwanza mou iliyosainiwa ni kwa manufaa ya nani?
Mleta maada atujuze hapo ndipo tutachangia.
 
Kuna ombi lilitolewa kuhusu kuattach document yote, je limefikia wapi mleta hoja?
 

Umenibana wapi? record ipi ya uongo? Kwani uongo turnover ya bakhressa sio $300 Milion hebu kanusha basi? Na hao wafanyakazi wa Barrick PAYE inaweza kuwa kwavile Barrick hawalipi kodi hivyo wanao uwezo wa kuwalipa mishahara mikubwa unaweza kutuambia Barrick wanalipa kodi kiasi gani? Na nikuulize Barrick ni kampuni ya mtu binafsi kama Bakhressa? Je Barrick ni muislamu kama Bakhressa? Huna cha kujibu hapa hebu nipatie mwangaza uongo wangu uko wapi? Sijakutukana kukote ila nimukuambia tuliza hamaki maana macho yamekutoka kama mtu aliyekabwa na samaki kwa jinsi ulivyoandika post yako. Hebu nifahamishe uongo uko wapi?
 

Mwanakijiji,

Unapindisha ukweli unaweza kutuambia viwanja vya waislamu kabla ya azimio la arusha vilienda wapi? Na wenyewe wamerudishiwa viwanja vyao au serikali imewalipa fidia?

Pia hebu tuambie Mwanakijiji inaelekea una data serikali inawapa kiasi gani Aga Khan kwa shughuli zake? Kama inavyowalipa makanisa billioni 91 kila mwaka?
 

Tshs Bilioni 91 au kabla ya mwaka huu ilikuwa Bilioni 60 ziko hapa hebu soma kipengele hiki:-

"The Government shall provide financial asssistance to Church insituttions and shall seek financial assistance to Church run social services in its bilateral negotiations with foreign governments"

source:The Memorandum of Understanding between the Government of the United Republic of Tanzania and the Tanzania Episcopal Council (TEC) and the Christian Council of Tanzania-page 3

Haya tuambieni mnazitaka kodi zetu za nini? Na pesa tulizokwishawapa mlikuwa mnazitumia kwa kazi gani?
 
Mimi hapa sijui lengo ni nini kwa muda sasa nimekua nikiwashauri rafiki zangu na waafrika wenzangu kuzikana hizi dini zote za kuja, unajua hizi dini kubwa mbili yaani Ukristo na Uislamu zote in za kuja na hazina chimbuko na asili yake hapa..na hizi dini ndio zimekua chanzo kikubwa cha matatizo ya kutugawa na kututenga, mara utasikia mara wakristo wanapendelewa, oh mara waislamu walalamishi...mimi naona tuachane na haya mambo tuangalie mstakabali wa Taifa letu na tuyatatuae mataifa yetu kwa umoja wetu. Kwa ushauri sasa kama MoU, ni ya manufaa kwa watanzania wote basi itumike kwa watanzania wote bila ubaguzi na kama kuna madhehebu mengine yanafikiria kufanya hizi kwa maslai ya watanzania wote wafanye. Na lamwisho ninalo taka kusema ni kuwa, Kama kweli Mkristo atafuata hayo maandiko ya Biblia na vilevile Muislamu atafuata hayao maandiko ya Koran kwa ufasaha mimi sioni kama kweli tutashindwa kuishi kwa upendo na kuvumiliana...Ila mimi ninachokiona hapa nikuwa waumini wanafuata matakwa, hoja na tamaa za wanao waongoza, kama Koran na Biblia hiyo mnayo iamini inawataka kuheshimiana, kupendana na kuishi kwa amani na ninyi mnashindwa nini au mnatudanganya kuwa mnamfuata Mungu wa Neema na baraka kumbe mna waabudu watu??? Mimi nacho kifahamu kama kweli wewe Mkristo na Muislamu unamwabudu na kumpenda Muumba wako hutafanya hayo mabaya unayofanya achilia mbali kuyawazia.
 
Waislam wavivu wakufikiri, wanalaumu kuhusu MoU lakini hawaongelei kuanzisha hospitali na vyuo ili wa[pate na wao Mbona Rais alishasema anzisheni then muombe lakini wamebakia kulalama jama Vyuo vikuu kilekile mlichopewa mpaka leo ebu onyesheni uwezo wenu.
 
Taasisi za kikiristo zinawahudumia waislamu wote bila ubaguzi sasa kunahaja gani yakulalama kama hawabaguliwi? Vyuoni kwa wakristo waislamu wamejaa Hopspitali ndio usiseme.
 
Sisi waislamu tuache kulalama wakristo wakitubagua sisi hatuna kitu wala hatuna shule hatuna vyuo hatuna hospitali hatuna shule nzuri, madamu hawatubagui basi wacha serikali iwape tu.
 
Jamani Aga khani ni taasisi yamtu binafsi sio yawaislamu jamani, Huyu Aga khani ni mfanyabiashara tu Hotel za Serena zote zake East Africa, Bank ya DIAMOND yake na biashara zingine nyingi, sasa ebu twambieni Bakwata ina nini?
 
Yanatuambia kwamba sii kweli kwamba serikali yetu haina dini... serikali ina dini na ushahidi ndio huu...isipokuwa tu sahihisho - Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) sio ya Waislaam ni family business ya AghaKhan..
 
Hivi vyuo na hizo hospitali zinatoa huduma kwa watu wa dini gani?
 
Hivi vyuo na hizo hospitali zinatoa huduma kwa watu wa dini gani?

Kwani vyuo vya private, waislamu na hospitali vinatoa huduma kwa watu wa dini gani?

Kwanini vya wakristo vipewe ruzuku? (udini)
 
Mkandara said:
Yanatuambia kwamba sii kweli kwamba serikali yetu haina dini... serikali ina dini na ushahidi ndio huu.

Mkandara,

..tumeona kwamba mwanzo kulikuwa na MOU kati ya serikali na Agha Khan, ambao ni Ismailia.

..halafu ikaja MOU kati ya serikali na makanisa ya Kikristo, namely Anglican,Catholic,Lutheran.

..mwisho, Muslim Trust Fund nao wakapewa majengo kwa ajili ya chuo kikuu, hapoo napo lazima kulikuwa na mkataba/mou.

..sasa katika mtiririko huo, serikali ina dini gani? Je, ni Ismailia, Kristo, au Islam???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…