Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

LA!!!!! nimekushangaa FF, hivi Mwl. Nyerere kakukosea nini? kakuchukulia mumeo au? mbona unamchukia sana hivyo. Mkataba (MoU) umesainiwa wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi ww lawama unapeleka kwa Mwl.Nyerere (BABA WA TAIFA) du. kweli kufikiri kwakpo kuko ndani ya box ssiku ukitoka humo tutakuona
 

Hapo ndipo unapokosea sana, soma kitabu cha Sivalon, cha Aboud Jumbe cha Hamza Njozi cha Mohamed Said cha Bergen cha Illife na wengineo, utaujuwa huu mfumo kristo umeanzia wapi. Ukisikia watu wanausema usifikiri wanakurupuka.

Nyerere ndio chanzo cha yote au hujui kwanini Rais wa nchi anapewa uwenye "heri'? heri ipi aliyoifanyia hii nchi? Kang'atuka katuwacha Tanzania ni nchi ya mwisho duniani kwa umaskini, kuna heri hapo?

Nadhani unaelewa kisa cha Mwinyi kuzabwa kofi na kijana wa Kiislaam, kwa fikra zako kuongolea kondom tu ndio kulikopelekea kuzabwa Mwinyi kibao? la hasha, ni unafik wake.
 

Sina chuki na ukristo kwasababu ukristo siyo tatizo hilo sina haja ya ku-prove kwako maisha yangu yana prove hivyo kwasababu nimesomesha na ninaishi na wakristo wengi na huu msimamo wangu namwambia mkristo face to face ..tunaendelea na maisha

wewe ndio una chuki na uislamu na waislamu na unaona kupendelewa kanisa ni sawa irrespective kuwa hiyo ni haki au siyo haki pamoja na kwamba kila mwenye akili anaona kabisa hiyo MoU ni uwizi wa mali ya umma lakini wewe na wengine of course motivated by udini ..mnaona ni sawa..

Nina uhakika hakuna taasisi ya kiislamu inayopokea bilions kila mwaka kutoka serikalini NONE?? kungekuwa na kelele ya kufa mtu hapa.. sasa majengo wameshapewa unafanye auditing ya nini?..wakati hujapewa ruzuku ya kufanya repair none..

Mengine unayoyasema unataka ku-divert mada..waarabu na wahindi wanafaidi wengine jasho wengine kwa ufisadi na wanaandikwa sana ..

Wakristo hawafaidi oh yes hawafaidi kwasababu Maaskofu wanakula hizo hela za umma ...without auditing wataendelea kuitafuna taifa hili kupita mikataba ya epa/richmond etc na kwakuwa watu kama nyinyi mmeelemea kutetea kanisa (udini) by any cost..wataendelea kula tu..

Mkuu haturisishani hapa ila tunasimamia ukweli, haki na usawa wa ugawaji wa national cake period..

Sasa kama hiyo ni chuki well let iti be..kama ambavyo tunawachukia mafisadi wengine pia..
 
nadhani alikuwa mhubiri wa dini, hatuna 7bu ya kujua habari zake. Napenda kumsikiliza Prof. Safari hasa ktk maada zake za sheria. Ninyi mnaopinga MoU mnafahamu kuwa taasisi za kanisa zikijitoa kutoa huduma za jamii nchi hii itapata kiharusi?????? Tembea nchi hii uone, wengi mnaopinga ,mambo haya mmekulia DSM ambako karanga zinachumwa kwenye miti, angalieni bw.
 
Hapo kwenye Red, tukio hilo nililiona kwenye TBC 1 nikiwa Arusha, Mwilim wote ulilowa, nafsi yangu ilihuzunika kupita kiasi kwa udhalilishaji ule kwa Rais Mstaafu.Ila nilikuwa sijui kumbe wewe FF ulifurahia tendo lile, La!!!!!!!! anyway yote maisha, umenikumbusha jambo la huzuni sana, Nampenda na kumheshimu Mzee Ruksa kama kiongozi wa Taifa. Hivi ulishangilia sn tendo lile mpaka unalitolea mfano du we mkali, mligngeana hata glass kwa udhalilishaji ule. Mpaka una mwita Mnafiki du, siku ukitoka kwenye box nitakuona
 

Wala si uongo itapata kiharusi, na hicho hakina tatizo ikipata kimsiba ndio ingekuwa tatizo.
 

Usemayo sema wewe, mimi nnasema ni mnafik na ndio maana akazabwa kibao.
 
Nauliza tena hili kama kuna mwawahseria atupe jibu
  • Is a MoU a legal binding document like a contract .?

Na hii tafsiri ya wkipedia kama iko sahihi inaweza kutupa mwanga gani juu ya hii Mou ili ifutiliwe mbali

 

C'moon dude kwa nini unapenda sana dilly dallying? Yaani mabadiliko ya katiba 1984 yalifanywa ili ku - accomodate MoU in 1992, 8 years later? Kumbuka ulichotuhumu kwamba katiba ilibadilishwa ili ku-accomodate MoU kitu ambacho ni uongo, baadae ukaja na act ammendment kama proof nikakwambia kubadilisha act si kubadili katiba. Ukaendelea kukomaa na uongo huo. Sasa umen'gamua kwamba ulikuwa unaongea uongo ambao unataka kuuhalalisha kupitia mabadiliko ya katiba in 1984. Mkuu unafaidika nini na uongo? Kwa nini usijadili hoja kwa facts?

Kwa mtindo huu anaweza akatokea mpumbavu mwingine akasema yeah katiba ilibadilishwa wakati ule kwa maandalizi ya MoU wakati Nyerere akiwa raisi - mkristo, ikaviziwa aje raisi muislam, Mwinyi ili kuipa uhalali zaidi na kuifanya isitiliwe mashaka.

Unachozungumza ni sawa na kusema atokee mwanasiasa mwenye charisma ya hali ya juu, mjenga hoja mzuri na anayependwa sana na watu aamue kugombea uraisi lakini anakumbana na kisiki cha mgombea uraisi lazima awe na digrii. Mwanasiasa wetu huyu anaenda majukwaani na kuwaambia wananchi mnaona hata katiba ilibadilishwa ili mimi nisigombee uraisi.


Naakurudisha tena kwenye maandishi yako.

 
Nyambala,

Nafikiri nimekuachia uprove wrong kama mie nachokisema ni uongo lakini umeshindwa. Umetaka Act iliyolegalise MoU nimekupatia reference ya section 30. Education Act No 25 ya 1978 (Refer to what Sheikh Mohamed Said mentioned in his paper). Ukahamia kuwa kuuliza je Act ndio constitution nikakuambia sheria yeyote nchini haiwezi kubadilishwa bila ya kwanza katiba kubadilishwa au kuangaliwa. Nimekupatia kipengele cha katiba section 11 of the constitution ambayo imefanyiwa amendment mwaka 1984. Vile vile nimekupa Law reform commission recomendations zilizofanyika baada ya tume ya nyalali na vipengele vya elimu vilivyokuwa recommended.

Hebu nikuulize wewe sasa hebu niprove me wrong katika maswali yafuatayo:-

a. Section 30-31 ya Education Act No 25 ya 1978 ilibadilishwa au haikubadilishwa? Je umesoma Education Cap 353 inasemaje section 22 inayozungumzia kuhusu private schools and non-governmental schools? Je vilikuwapo vipengele vile katika Act ya mwaka 1978?

b. Katiba ya Tanzania 1977 inasemaje kuhusu right of education na Katiba ya 1997 pia inazungumzaje kuhusu right of education to citizen?

c. Kwanini MoU iliandaliwa na kusigniwa na Waziri Mkuu and First vice president Edward Lowassa instead of waziri wa afya na waziri wa elimu?

Kama huwezi kuyajibu maswali haya labda nikuulize jengine who is dilly dallying baina yangu mie na wewe? Maana naona hutaki kufahamishwa wewe.
 

Haya mkuu inatosha maana ukiangalia toka mwanzo hujibu maswali yangu, ni kuongeza miparagraph na maswali mengine wakati yale yangu hukujibu sasa mijadala ya namna hii ni kupotezeana muda jibu sswali uliza swali si swali juu ya swali. Na kwa sababu I know who exactly I am talking to wala sishangai.
 
@Mdondoaji
Je hizo act unazorefer za mwaka 1978( zilizoachwa na Nyerere) hazina tatizo? Maana unapoteza consistency. umeshamponda sana za huyu mzee bila hat kuumpa 2% yacredit

kwa hiyo kuwa consistency bora Uponde act ya mwaka 1978 na uponde hata ya mwaka 1995 . Alafu ulete yako.

But atleast nimekusoma kumbe kuwa siyo yote yaliyofanyika chini ya nyerere yalikuwa mabaya kwa "watanzania"na "waislam"
 
Ina maana wewe hutumii condom unapokutana na wanaume?
 

Hadithi nyengine zinafurahisha sana. Kila anapotajwa ''msomi'' wa kiislamu lazima atajwe na Nyerere, kwamba alikuwa akimuogopa sana.
Sijui kama ni kusudi ama ni bahati mbaya mnasahau kwamba Nyerere naye alikuwa msomi, alikuwa na uwezo wa kujenga hoja dhidi ya wasomi na wasio wasomi na akaeleweka vizuri sana.
 

Plus Compounding Interest Rate itafikia zaidi ya 20 Trillion. WOW!!
 
Ulitaka serikali ikawashike mkono waislam na wahindu iwaambie njooni tuweke makubaliano ya maridhiano? Cha msingi hizo taasisi za kikristo hazifunngwi kuingia makubaliano na serikali pia kadhalika hawanyimwi.Na makubaliano sio kurudisha shule maana hata wakristo shule zao nyingi bado hazijarudishwa.

Wakristo wameendelea kuwa agressive kwa kwenda maporini kuchukua maeneo makubwa na kuweka taasisi zao huko.Waislam wanaitaji kuiga hili
 

Crap!!!!
 

Ina maana wewe unakubaliana na wizi huo unafanya na haya makanisa kwa Serikali yenu?
 

Zing,

Nitake radhi baba wa taifa ana mazuri mengi ila sio mkamilifu kama mnavyotaka kumfanya awe. Mazuri ya Nyerere ni mengi siwezi kuyataja yote ila nitakupa list yake:-
a. Ameleta umoja even though with sacrifices but ni umoja uliodumu hadi sasa.

b. Ameleta national identity nayo ni kiswahili.

c. Ameanzisha misingi imara ya uwajibikaji na uadilifu kazini.

d. Ameleta ukakamavu katika taifa

e. Ana mchango mkubwa katika kupatikana kwa uhuru wa nchi hii hata hivyo hayuko peke yake.

Na mengineyo mengi.

Ila kuna mabaya pia anayo ambayo ndio tunayazungumzia.
 
Mdondoaji,

..Mwalimu hakuleta kiswahili nchi hii.

..hata wakati wa harakati za uhuru inasemekana ni mara 2[akiwa mbulu, na mwanza(??)] tu alilazimika kuzungumza kupitia mkalimani.

..kwa upande wangu nadhani ilikuwa ni makosa makubwa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ktk shule za msingi.

..kwa kweli mfumo wetu wa elimu ulivyoparaganyika, na hili zimwi la EAST AFRICA FEDERATION linavyotunyemelea, at least wangetuachia Kiingereza wanetu wangeweza kufurukuta ndani ya federation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…