Mrimi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 1,691
- 640
Mkuu kwa kuwa unaushahidi wa hili (japo hujaweka hapa), ila naomba nikukumbushe japo unalijua hili:
Watu wengi tu kama wewe wanajaribu ku ignore ukweli ulio dhahiri. Jamani, hiki kitu kinachoitwa kanisa/ukristo mara yingi kinachukuliwa kijuu juu tu japo ukweli upo wazi. Hawa watu si wamoja. Wewe ni shahidi no.1 kwa kwamba ukihudhuria ktk mikutano yao au makanisa yao utaliona hilo, halijajificha kabisa.
Angalia, Wasabato kivyao, wakatoliki kivyao, walokole(nao wana varieties zao) kvyao. Kila kikundi kiaangalia maslahi yake kivyake. Kuna wakati wanalalamikiana, kutukanana nahata kutishia kufikishana mahakamani. Hawa watu wanafahamika kwa ubinafsi wao(kiroho) kila kikundi kinajiona ndicho chenye kuhubiri ukristo wa kweli na kwamba vingine ni usanii tu. Hawa wakristo si wamoja jamani, tuwe wakweli kama ulivyosema wewe.
Mimi nilitegemea useme kanisa gani hasa linamwangwangusha mheshimiwa(utoe na ushahidi). Tumekuwa mstari wa mbele kuhubiri udini, hata pale ambapo failure reasons ziko wazi. Najua hoja hii itajadiliwa hapa kwa kuzingatia dini ya kila mtu, lakini pia ningependa nione mmoja wetu akituthibitishia kuwa dini yake inafundisha watu kula rushwa, kupendelea, uzembe na uchafu wote tunaojua kwa maana bila kujali dini ya mtu tunaona waumini wa dini mbalimbali wakituhumiwa kuiba, kufanya zinaa na hata ukiangalia ktk sakata la Dowans wahusika ni waumini wa dini mbalimbali tofauti. Je, tuseme hii nayo ni issue ya kidini? La hasha, dini itabaki kuwa dini na usafi wake kwa kuzingatia nguzo zake. Waumini wanaokengeuka wahukumiwe wao kama wao, sio kujumuisha waumini wote ambao kiukweli wengi wao ni wahanga wa huo uchafu unaofanywa na waumini wanzao.
Mimi nadhani kifike kipindi turuhusu ubongo wetu kutimiza wajibu wake wa kufikiria kiuhalisia. Hebu tuanche uvivu wa kufikiri. Udini sio suluhu ya matatizo ya watanzania, tukatae mpumbavu yeyote anayetaka kutuaminisha kuwa tumefikia hapa tulipo kwa sababu ya udini. Nionavyo mimi ni kuwa, hawa watawala wametafuta kitu ambacho kinagusa hisia za kila mtu wametutupia ili tubaki tukibishana kijinga tu, huku wakituibia na kutufanya wanavyotaka wao. Na sisi kweli kwa ujinga wetu tumebaki tukipiga kelele na kutupiana lawama(kama wakristo wanavyofanya). Ujinga mtupu. Tukumbuke, ubishi wa kidini hata kama ni kijiweni huwa hauna hitimisho. Hivi ni kwanini hatufunguki macho jamani?
Mimi nadhani umefika wakati, watu wazima tuwe wazima kweli, wanasiasa wafanye siasa ya kweli wasomi wawe wasomi kweli na watu wa Mungu wawe wa Mungu kweli. Hii Tanzania ni yetu sote na jambo baya lolote litakaolotokea hapa litatupata sote tana ni zaidi kwetu sisi tuliotupiwa mzoga wa hili dudu linaloitwa udini tumeachiwa tukinyang'anyana na kukimbizana kama manyang'au.
Mungu ibariki Tanzania.