Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Faiza Fox said:
Wanauondoa mjadaala kutoka MoU ya kanisa na Serikali, ambao ni wizi mtupu, kuelekea kwenye usomi wa watu.

Four walls of a class room does not make a person learned, it is rather a solitary confinement of someones greater potentials.

FF,

..wengine tumekuwepo kwenye mada hii kwa muda mrefu. Mdondoaji atanisaidia hapa.

..basically ni kama tume-exhaust kila hoja tuliyonayo na ndiyo maana unaona tunatoka nje ya mada kidogo.

..sasa wakija wachangiaji wapya, wakaleta hoja mpya, bila shaka tutarudi kwenye mstari.
 
Mdondoaji,

..Mwalimu hakuleta kiswahili nchi hii.

..hata wakati wa harakati za uhuru inasemekana ni mara 2[akiwa mbulu, na mwanza(??)] tu alilazimika kuzungumza kupitia mkalimani.

..kwa upande wangu nadhani ilikuwa ni makosa makubwa kukifanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ktk shule za msingi.

..kwa kweli mfumo wetu wa elimu ulivyoparaganyika, na hili zimwi la EAST AFRICA FEDERATION linavyotunyemelea, at least wangetuachia Kiingereza wanetu wangeweza kufurukuta ndani ya federation.
Mkuu hapa unafanya makosa makubwa sana... Kama Nyerere asingekifanya kiswahili kuwa lugha ya Taifa tusingekuwa hapa tulipo leo...Na ni makosa makubwa sana ktk ELIMU kuchukua lugha ya kigeni kufundishia..Hakuna nchi iliyoendelea inayochukua lugha ya kufundishia tofauti na lugha ya Taifa isipokuwa nchi maskini na koloniwa, ndio maana Ujinga hauwezi kwisha..
 
Joka Kuu,

Mwalimu alihamasisha kiswahili kitumike nchi nzima. Kiswahili kimeletwa na waarabu nchini ila kilikuwa kikizungumzwa na watu wa pwani na baadhi ya miji kama kwa wanyamwezi, Ujiji na kwengineko. Hata hivyo Nyerere alihamasisha Kiswahili kitumike nchi nzima na kiwe lugha ya taifa.

Kwanza mie siungi mkono East Africa Federation. Federation kama hizi zina madhara mengi kuliko manufaa na nadhani tungelikuwa tunaungana na majirani zetu kwa vitu vyenye manufaa nasi na sio kila kitu. European Union na matatizo yao ya madeni ni funzo tosha kwetu ila asiyesikia la mkuu huvunjika guu tutakuja kuelezana hapa baada ya federation hasara na matatizo yake.

Mie naunga mkono kufundishwa kiswahili hadi vyuo vikuu kwani vitasaidia kuleta maendeleo kwa kiwango kikubwa. Wachina wameweza kufanikiwa kielimu na kimaendeleo kwasababu ya kichina kinafundishwa hadi vyuo vikuu. India kihindi kinafundishwa hadi vyuo vikuu. Ujerumani kijerumani kinafundishwa hadi vyuo vikuu. Sasa kwanini sisi Tanzania tuache kiswahili chetu na kutukuza kizungu??? Kiswahili ni muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
 
Mdondoaji,

..naungana mkono. hoja kwamba Waislamu hawajasoma ni mufilisi.

..hoja kwamba Waislamu hawawezi kusoma pia ni mufilisi.

..I am one of those who believe kwamba Waislamu wakipewa access to a quality education basi wanaweza ku-achieve mambo makubwa.

..Personally nimesoma na Waislamu, and looking back, manake wakati huo tulikuwa hatuulizani dini, kuna vijana wa Kiislamu who were very smart.

..miongoni mwa wa-Tanganyika watatu wa kwanza kupata shahada ya London University ni Abdulrahman Salim Msangi. Ilibidi DC wa wilaya ya Pare wakati huo apande milima ya Usangi kwenda kumpongeza Mzee Salim Msangi kwa achievement ya mwanawe. Later on Abdulrahman Msangi alikuwa dean wa kwanza mzalendo wa kitivo cha Science UDSM.

..now,Prof.Juma Mikidadi Mtupa anafahamika sana tangu akiwa mbunge toka mkoa wa Lindi.

..baada ya kuondoka bungeni akagombea nafasi ya Mufti wa Bakwata na kushindwa. lakini nadhani huyu angewafaa Waislamu.

NB:

..tatizo ninaloliona mimi ni kwamba Waislamu wenye elimu ya ki-secular hawashiriki/hawashirikishwi ktk uongozi wa Jumuiya za Kiislamu.

..nadhani kukosekana kwa waumini wenye elimu ya ki-secular ktk taasisi za Kiislamu ndiko kunakosababisha viongozi wa taasisi hizo kutumiwa kisiasa na CCM na kupelekea kuviaibisha vyombo hivyo.

Joka Kuu.,
Ni kweli hoja kwamba waislam hawajasoma ni hoja muflisi!
Nilichokuwa nasema mimi ni kuhusu viongozi wao wa dini kwamba wengi wao hawana hiyo elimu ya ki secular. Ndiyo maana priority kubwa unaweza kukuta ni kujenga misikiti tu. Yaani unaweza kukuta katika eneo dogo kuna misikiti mingi hata kama hiyo sehemu kuna waislam wachache.
Kingine kinachowakwaza waislam ni dhambi ya ubaguzi. Siyo tu baadhi yao wanabagua wakristu lakini hata wao wenyewe kwa wenyewe wanabaguana sana. Utashangaa sana ukiona wasomi wakubwa kama akina Issa Shivji wanabezwa na baadhi ya waislam eti kwa sababu tu anayasifia mazuri aliyofanya Nyerere. Tunaona hata hapa jamvini akina Mkandara wanavyoshambuliwa wakijaribu ku acknowledge ‘machache’ mazuri aliyofanya Nyerere. Kwa wao ukimsifia mtu mkatoliki kama Nyerere basi wewe siyo muislam safi.
Kifupi watu kama akina Topical, FaizaFoxy na wengine wengi wanaona matatizo yote ya waislam yamesababishwa na bado yanaendelezwa na kanisa(Mfumo Kristu). Hapa mimi nakubali kuwa wanatafuta tu kizingizio baada ya kuona udhaifu wao na kushindwa kutatua matatizo yao wenyewe.
Huu utitiri wa taasisi za kiislam kuanzia Bakwata na nyinginezo zinawakilisha vikundi gani vya waislam? Sasa kama umoja wenyewe haupo na kuna vikundi tu , hizi kelele za kupinga mfumo kristu/MoU zitafika wapi? Hivi badala ya kwenda Diamond Jubilee na kuzunguka nchi nzima kuhamasisha waislam kupinga mfumo kristu, kwanini waislam wasikae chini kwanza na kuanza mchakato wa kuunda chombo/taasisi moja ambayo itakuwa ndiyo inawakilisha sauti ya waislam wote Tanzania nzima?
Mimi nadhani haya makelele ya uhalali wa MoU na mfumo kristo tungekuwa tunayajadili katika angle tofauti kabisa kama hawa wenzetu wangekuwa na viongozi wa dini wenye uwezo wa kutoka nje ya box!
 
Mkandara said:
Mkuu hapa unafanya makosa makubwa sana... Kama Nyerere asingekifanya kiswahili kuwa lugha ya Taifa tusingekuwa hapa tulipo leo...Na ni makosa makubwa sana ktk ELIMU kuchukua lugha ya kigeni kufundishia..Hakuna nchi iliyoendelea inayochukua lugha ya kufundishia tofauti na lugha ya Taifa isipokuwa nchi maskini na koloniwa, ndio maana Ujinga hauwezi kwisha..

Mkandara,

..una maana gani unaposema "tusingekuwa hapa tulipo"?

..kwanza taaluma nchi hii iko chini, juu ya hilo lugha ya mawasiliano ambayo ni Kiingereza ipo chini vilevile. sasa si bora tungekuwa tunafundisha Kiingereza at least tungekuwa na tatizo moja la taaluma tu.

..hivi unajua ujuzi wa lugha ya Kiingereza umechangia kiasi gani kuifanya India kuwa kati ya mataifa vinara ktk masuala ya Teknolojia?

..kwa taarifa yako KIINGEREZA ndiyo official language ya EAST AFRICA FEDERATION. Bunge la Afrika Mashariki linaendeshwa kwa Kiingereza. Raisi wa Afrika Mashariki atakuwa akiwasiliana na wananchi wake kwa Kiingereza. sasa wa-Tanzania tuna nafasi gani hapo?

..anyway, tusiharibu mada ya MOU.

Zing,

Nitake radhi baba wa taifa ana mazuri mengi ila sio mkamilifu kama mnavyotaka kumfanya awe.
Nani kasema mwalimu Nyerere alikuwa ni Mkamilifu???? Ebu taja tu au onyesha cooment Kule kwenye Mada ya Mohamed said inaonekana Nyerere alikuwa Adui wa usilam. Lakini kwenye Maada hii inaonekana act zilibadilihswa wakati wa mwinyi ndio zilikuwa adui wa uislam na zile za kipindi cha nyerere zilikuwa bora..... Ndio maana tunahitaji consistency

Unajua Kuna mambo tukikubalina hata Njia bora ya kutatu tatizo na inequalities itakuwepo. CCM ya ( Mwinyi, Mkapa kikwete) wanatak takiwmu za afya, na elimu ziwabebe. kanisa liko kwenye position nzuri .kuwsiidia hayo so wameaua kufunga ndoa. Sishabikii hilo ni tatizo

Hii MOu sio Mkataba hata JK naweza kuufuta hata kesho. lakini kwa nini anakuwa mzito.
Ni sababu waziri wa afya na katibu wa fya si waislam au? Au ni sbabu za kichama(CCM) Au JK anaon sio maamuzi sahihi kwa sasa ?

Hapo kuna problem lakini tukiwa mashabiki huwezi kujua real cause of problem ni nini.

Sababu ya kutochambua real casue of problem ndio maana tumefikia hatu tunamu attack Nyerere kutafisha mashule na mahopsitali. Ni kwasabu tu Ni nyerere . Tunafikia kumuttaac mwinyi kuyarudisha mahospitali kwa kanisa . May be jsut bcs wanaorusdishiwa ni makanisa... Tunapoteza consistency...

Tuna muattach Mkapa eg kw Kuwapa waislam chuo na Kikwete kwa kmualika papa au kuteua viongzi fulani waislam.

Sasa inakuwa mbaya pale mimi nikianza kumuattach au kumtetea nyerere sababu tu ya Dini yake . Au nishindwe kumkoosoa Nyerere au Mkapa sababu Ni mkristu mwenzangu. Au mimi kama mristu Nikimkosa Mwinyi, Musilam aone zing anamkosoa muislma na sio sera.

Kuna ambo mengi yansabaish watu tutoke kwneye hoja za msingi badala yake ni kuteaa na kukosa Rashidn na John tu.

Mazuri ya Nyerere ni mengi siwezi kuyataja yote ila nitakupa list yake:

a. Ameleta umoja even though with sacrifices but ni umoja uliodumu hadi sasa.

b. Ameleta national identity nayo ni kiswahili.

c. Ameanzisha misingi imara ya uwajibikaji na uadilifu kazini.

d. Ameleta ukakamavu katika taifa

e. Ana mchango mkubwa katika kupatikana kwa uhuru wa nchi hii hata hivyo hayuko peke yake.

Na mengineyo mengi.

Mondoaji Mimi naweza kuyataja mabaya ya mwalimu kwa mtazamo lakini najua hata hayo amabyo naona ni mabaya basi maamuzi yake nyerere hayukuwa yamefanywa kwa msingi wa dini au kabila. Ndio hicho labda tunapishana. Ndio maana utaona naimekuuliza kam Act za mwaka 1978 hazikuwa n tatizo

Ila kuna mabaya pia anayo ambayo ndio tunayazungumzia.
Hayo mabaya hayakosekani Kwa mtu yeyote lakini tuwe wawazi na wakweli .Tutafute chanzo haiisi na sababu. Mimi na wewe hatuwezi kukataa
Katika zuri la kuleta umoja wa kitaifa kuna hili baya moja

  • Alifuta tawala, mahakam za kichief na mkabila.
Sasa tukiondoa ushabiki itakuwa sahihi tuisema nyerere alikuwa na chuki tawala za kichief au msukumo wake huo ulitaokana na kutka kujenga umoja. Je yalikuwa ni maamuzi sahihi . Nngekuwa mmoja wa familia za kichief naweza kusema lilikuwa Kosa kubwa. Lakinimtu kati "mtanzania" akitoa maoni bila upendeleo atakubali maamuzi hayo hayakuwa na shinikizo la ukabila wala udini

Anyway Hapa tunajadili Mou lakini inaonekana things strted to go from bad to worse after Nyerere era.

Sasa navyoona
ii Mou sio Legal binding Document. Kwa nini CCM ya ilianzia kwa CCm ya mwinyi then ikanedelea na CCM ya mkapa na sasa ya Kikwete.
  • Unaweza kumsamehe Mwinyi serikali yake Labda haikuwa na fedha za kuendesha na kuongeza huduama za afya maye be hakuwa na jinsi. Utajiri ulikuwa mikononi mwa watu sio serikali.
  • Mkapa serikali yake ilifankiwa kukusanya mshiko na kurudisha heshima ya kufanya kazi serikalini. Lakini sijui zaidi ya barabarakam serikali imejenga hospitali yeyote. Sana sana kisiasa hospitli za mkoa zinatwa za rufaa wakati hazina facilities na mazingira sahihihi.
  • Kikwete naye na rafiki lowasa shule kila kata. utendaji wa hizo shule ukoje. Walimu wanagapi wazuri wako tayari kwenda kigoma lindi na mtwara wilayani kufundisha?

aisee ngoja niihsie hapa lakini haya mambo tukiyachmbua basi tunaweza kujua na kuona tatizo ni nini hasa. kama tatizo ni "mfumo kristo" basi tunaweza kukuta huu mfumo kristo ndani yake wapo rashid na Juma na khamis. Tunaweza kugundua kuna hata kina John na James wanaathirwa na huu so called "mfumo kristo". So kwa nini uitwe "mfumo kristo"

So lets talk about the real problem lakini if its from religion point view then.........
 
Joka Kuu.,
Ni kweli hoja kwamba waislam hawajasoma ni hoja muflisi!
Nilichokuwa nasema mimi ni kuhusu viongozi wao wa dini kwamba wengi wao hawana hiyo elimu ya ki secular. Ndiyo maana priority kubwa unaweza kukuta ni kujenga misikiti tu. Yaani unaweza kukuta katika eneo dogo kuna misikiti mingi hata kama hiyo sehemu kuna waislam wachache.
Kingine kinachowakwaza waislam ni dhambi ya ubaguzi. Siyo tu baadhi yao wanabagua wakristu lakini hata wao wenyewe kwa wenyewe wanabaguana sana. Utashangaa sana ukiona wasomi wakubwa kama akina Issa Shivji wanabezwa na baadhi ya waislam eti kwa sababu tu anayasifia mazuri aliyofanya Nyerere. Tunaona hata hapa jamvini akina Mkandara wanavyoshambuliwa wakijaribu ku acknowledge ‘machache' mazuri aliyofanya Nyerere. Kwa wao ukimsifia mtu mkatoliki kama Nyerere basi wewe siyo muislam safi.
Kifupi watu kama akina Topical, FaizaFoxy na wengine wengi wanaona matatizo yote ya waislam yamesababishwa na bado yanaendelezwa na kanisa(Mfumo Kristu). Hapa mimi nakubali kuwa wanatafuta tu kizingizio baada ya kuona udhaifu wao na kushindwa kutatua matatizo yao wenyewe.
Huu utitiri wa taasisi za kiislam kuanzia Bakwata na nyinginezo zinawakilisha vikundi gani vya waislam? Sasa kama umoja wenyewe haupo na kuna vikundi tu , hizi kelele za kupinga mfumo kristu/MoU zitafika wapi? Hivi badala ya kwenda Diamond Jubilee na kuzunguka nchi nzima kuhamasisha waislam kupinga mfumo kristu, kwanini waislam wasikae chini kwanza na kuanza mchakato wa kuunda chombo/taasisi moja ambayo itakuwa ndiyo inawakilisha sauti ya waislam wote Tanzania nzima?
Mimi nadhani haya makelele ya uhalali wa MoU na mfumo kristo tungekuwa tunayajadili katika angle tofauti kabisa kama hawa wenzetu wangekuwa na viongozi wa dini wenye uwezo wa kutoka nje ya box!

We acha hizo...

Kwa hiyo kuwepo kwa misikiti mingi na taasisi nyingi za kiislamu

Ndiyo sababu ya serikali kusaini MoU ya kupeleka pesa za umma kanisani?

Huwezi kuongelea ubaguzi wa waislamu wakati ww si muislam (ya ngoswe mwachie ngoswe)..besides umoja wa kikristo ni upi?

Mkuu MoU ni sawa na epa/richmond/ ni wajanja wachache wanavuta hela za serikali kwa mgongo wa kanisa na biashara

Anayetetea MoU anakosa mora authority kuwaonyeshea mkono epa, richmond etc maana..

Either ni mdini (ukristo) au ni mnafiki wa kutupwa period..
 
..............................

Anayetetea MoU anakosa mora authority kuwaonyeshea mkono epa, richmond etc maana..

Either ni mdini (ukristo) au ni mnafiki wa kutupwa period..

MoU hata kama ina tatizo ni tofauti na EPA na richmond. Unless huelewi mana ya MoU
 
MoU hata kama ina tatizo ni tofauti na EPA na richmond. Unless huelewi mana ya MoU

Then you are either "Mdini (mkristo) kutetea hadi kifo kwasababu inafaidisha miradi ya kanisa au ni mnafiki mkubwa...

Tofauti ipo kwasababu EPA/ Richmond wanatoa services kibiashara wanaibia serikali kibiashara..

MoU inaibia serikali kupitia kanisa (unaudited) bila auditing na viwango ni vilevile spririt ni ileile wahi mapema..
 
Kwa hiyo hata serikali ya KIkwete haifanyi Auditing ya fedha za seriali yake.
.
 
Kwanza mie siungi mkono East Africa Federation. Federation kama hizi zina madhara mengi kuliko manufaa na nadhani tungelikuwa tunaungana na majirani zetu kwa vitu vyenye manufaa nasi na sio kila kitu. European Union na matatizo yao ya madeni ni funzo tosha kwetu ila asiyesikia la mkuu huvunjika guu tutakuja kuelezana hapa baada ya federation hasara na matatizo yake...
Nakubaliana nawe 400%: sio miungano yote na ma federation na ma union yana tija. Sasa hivi wanasema baada ya Greece inakuja Italy, na Italy iki default inadaiwa dunia nzima inaingia great depression. Tunachokosea waswahili tunaishi kwa methali: "Umoja ni nguvu, utengano.." Well, kuna exceptions katika hizi general aphorisms. Again, sio miungano yote ina manufaa.
 
Mkandara,

..una maana gani unaposema "tusingekuwa hapa tulipo"?

..kwanza taaluma nchi hii iko chini, juu ya hilo lugha ya mawasiliano ambayo ni Kiingereza ipo chini vilevile. sasa si bora tungekuwa tunafundisha Kiingereza at least tungekuwa na tatizo moja la taaluma tu.

..hivi unajua ujuzi wa lugha ya Kiingereza umechangia kiasi gani kuifanya India kuwa kati ya mataifa vinara ktk masuala ya Teknolojia?

..kwa taarifa yako KIINGEREZA ndiyo official language ya EAST AFRICA FEDERATION. Bunge la Afrika Mashariki linaendeshwa kwa Kiingereza. Raisi wa Afrika Mashariki atakuwa akiwasiliana na wananchi wake kwa Kiingereza. sasa wa-Tanzania tuna nafasi gani hapo?

..anyway, tusiharibu mada ya MOU.

1. Nina maana kwamba kabla kiswahili hakijawa lugha ya taifa mikoa mingi sana ya bara tulikuwa tukitumia lugha zetu ktk mawasiliano. Nakumbuka vizuri udogo wangu nilikuwa nazungumza kijita na kikerewe zaidi nikiwa nje na marafiki zaidi ya kiswahili ambacho tukizungumza nyumbani tena tukiitwa Waswahili na tulionekana watu tofauti. Wakati huo mikoani asilimia kubwa ya Waislaam ndio walizungumza kiswahili kuliko Wakristu na Wapagan hivyo kama kiswahili kisingekuwa lugha ya Taifa tusinge kuwa hapa kwa maana ya kwamba Umoja wetu ungekuwa kwa Utaifa tu lakini Ukabila usingeweza kuondoka...

2. Makosa unayoyafanya ni kufikiria kwamba TAALUMA inaweza kuwa juu kwa kutumia LUGHA ambayo iko chini kama ulivyoandika hapo juu. Kwanza lugha ndio hufundishia taaluma yaani unamfundisha mtu kitu kwa lugha anayoifahamu ili apate kuelimika. Maadam umekiri mwenyewe lugha ya mawasilino ya kiingereza iko chini kwa nini unataka kuwafundisha wananchi taaluma yoyote wakati hawaelewi, unategemea wataelimika vipi kama sii kukariri na kuhifadhi elimu pasipo kujua maana yake. Kisha mnashangaa matokeo ya mitihani kwa watoto wetu miaka hii ni mabaya kuliko wakati wowote ule.

3. India wanafundisha kiingereza kama lugha kwanza yaani somo la lugha wakati huo huo wakiwafundisha watoto wao 1+1 kwa kihindi na nakuhakikishia asilimia 100 ya wahindi wote walosoma wanaweza kuongea na kuandika kihindi lakini ni wachache walosoma elimu ya juu ndio wanaweza kuongea na kuandika kiingereza..Kwa maana kiingereza kwao kimetumika baada ya kujifunza Lugha ya mawasiliano na kuzungumza vitu anavyovifahamu hata akizungumza kwa kihindi, Kiswahili au Kichina...Mtanzania ambaye leo amechukua kiingereza kama lugha ya kufundishia hawezi kuandika kiingereza na hawezi pia kuandika kiswahili hivyo ndio maana elimu yetu iko chini...

4. Najua sana kwamba Kiingereza ndio lugha official ya EAC lakini sii ndio ktk kundi la wale wale wasiokuwa na elimu duniani? maanake Kenya hawana tofauti na sisi wala Uganda, Rwanda na kadhalika. Sisi wote tupo dunia ya tatu na nchi ambazo taaluma ni mtihani mkubwa. Mtu unasoma ili upate taaluma na sii kuzungumza lugha ya kigeni kama unataka kuzungumza lugha ya kigeni kwa ajili ya mawasilinao hiyo sii taalumu.

Unachokosea ni kwamba kiingereza ni LUGHA kwanza, haina maana anayeongea kiingereza kasoma sana (TAALUMA). Tanzania tunaweza kutokuwa na nafasi sii kwa sababu hatuna elimu isipokuwa hatujui lugha hiyo. Ukienda UK kesho na ukakaa huko mwaka mmoja bila kwenda shule unaweza kurudi na kutuwakilisha...

Usiogope mkuu wangu hatuwezi kuharibu mada mahala tunapojifunza wote maswala mazito kama haya..
 
Then you are either "Mdini (mkristo) kutetea hadi kifo kwasababu inafaidisha miradi ya kanisa au ni mnafiki mkubwa...

Tofauti ipo kwasababu EPA/ Richmond wanatoa services kibiashara wanaibia serikali kibiashara..

MoU inaibia serikali kupitia kanisa (unaudited) bila auditing na viwango ni vilevile spririt ni ileile wahi mapema..

Hahahahaha Call me mdini ,mkabila au vyovyte lakini usipotaka kufanya analytical apprrocah kutafuta au kufafanua tatizo huwezi kujua chanzo cha tatizo. U will end fighting the right war agaisnt the wrong enemy

Ebu Nikuulize naomba unipe mtazamo wako ili tutafute jibu

  • Kwa nini ilianzishwa baada ya Nyerere na si wakati wa nyerere?
  • Kwa nini Mou Hii ilikuja wakati wa Alhaj Mwinyi?
  • Kwa nini Mkapa pamoja uwezo wa kifedha wa serikali iliyoweka hakujenga hopitali nyingine ya rufaa yenye hadhi mkoa wowote
  • Kwa nini Kikwete naye anaendeleza yale yale aliyoacha Mwinyi na kuendelzwa na Mkapa ?

katika kujibu zingatia dondooo hizi amabazo badhi yake nimezitaja wenye coment nyingine

  • Kama tunadhani chanzo halisi cha tatizo ni "mfumo kristo" kwa nini baadhi ya waaisisi wa huu mfumo wamo kina rashid, juma, bakari.? Kwa nini bado kuna kina john, Silvanus, David nao wanaathirika na huu mfumo
  • Baada ya kusoma soma Nimeona MoU sio Legal Binding document. Kwa nini Jakaya Kikwete haifuti. Kwa nini mkapa hakuifuta?
  • Priority ya Mfumo wa siasa tanzania uko wapi? kwenye huduma za jamii au kwenye siasa.?Kwa nini serikali iinaazisha wailaya au mikoa ya Kisiasa sehemu amabzo hazina huduma. Angalia kiwkete kaazisha wialaya ngapi. ulizia hizo sehemu alizoanziiha wilaya zina huduma gani.Kwa nini kabla ya kuanzisha tawala za kisiasa wasihakikkishe kuna hudum za kijamii. Nani wa kulaumiwa kama serikali inakimbilia kuanzisha wilaya na kanisa linakimbia kuanzisha hospitali.? Kipi cha muhimu wilaya moja itengwe kwenye majimbo mawili ya uchaguzi (Kisiasa) au wilaya mja ibaki ni jimbo moja na seriali ijenge hospitali. kuliko kuwa na maimbo mawili bila hospitali ya wilaya.
Kwa hiyo Topical I happened to be a christian but I can analyse any problem with an open mind

Mkuu hapa unafanya makosa makubwa sana... Kama Nyerere asingekifanya kiswahili kuwa lugha ya Taifa tusingekuwa hapa tulipo leo...Na ni makosa makubwa sana ktk ELIMU kuchukua lugha ya kigeni kufundishia..Hakuna nchi iliyoendelea inayochukua lugha ya kufundishia tofauti na lugha ya Taifa isipokuwa nchi maskini na koloniwa, ndio maana Ujinga hauwezi kwisha..

Mkuu hii ishu ni complicated kidogo, maana ukiangalia kwa mifano halisi nchi kama Zimbabwe, Botswana, Namibia, South Africa zinatumia kiingereza and they are far much better kiuchumi (ukiondoa zimbabwe kwa sasa), well educated workforce na somehow ki-utawala bora (ondoa tena zim hapa). Lakni at the same tyme Malawi na Zambia zinatumia kiingereza kufundishia na ni mskini kuliko sisi.

Nenda Jamaica, Antigua, Guyana (Georgetown), Dominica, Trinidad kiingereza ni lugha ya taifa lakni ni maskini sana tu.
 
Hapana mkuu hawa wameweza kutumia resources zao ipaswavyo na sii matumizi ya lugha ya kiingereza. Ukiwaondoa wazungu tu (waliosoma kwa lugha zao), nchi inabwaya ingawa weusi wote wanaongea kiingereza na wamekwenda shule! Halafu walioendelea zaidi yao wote ni South Africa, huko karibu kila mtu anaongea kiingereza, sasa google utazame kiwango cha elimu nchini humo ukashika tama..Wee jiulize tu kitu kimoja, inakuwaje nchi zote zilizotumia lugha zao kufundishia ndizo zimeendelea na zile tulizotumia lugha ya kigeni ndizo maskini duniani - WHY?
Mtu akinipa jibu na sababu, basi sina zaidi la kuongeza.
 
Joka Kuu.,
Ni kweli hoja kwamba waislam hawajasoma ni hoja muflisi!
Nilichokuwa nasema mimi ni kuhusu viongozi wao wa dini kwamba wengi wao hawana hiyo elimu ya ki secular. Ndiyo maana priority kubwa unaweza kukuta ni kujenga misikiti tu. Yaani unaweza kukuta katika eneo dogo kuna misikiti mingi hata kama hiyo sehemu kuna waislam wachache.
Kingine kinachowakwaza waislam ni dhambi ya ubaguzi. Siyo tu baadhi yao wanabagua wakristu lakini hata wao wenyewe kwa wenyewe wanabaguana sana. Utashangaa sana ukiona wasomi wakubwa kama akina Issa Shivji wanabezwa na baadhi ya waislam eti kwa sababu tu anayasifia mazuri aliyofanya Nyerere. Tunaona hata hapa jamvini akina Mkandara wanavyoshambuliwa wakijaribu ku acknowledge ‘machache' mazuri aliyofanya Nyerere. Kwa wao ukimsifia mtu mkatoliki kama Nyerere basi wewe siyo muislam safi.
Kifupi watu kama akina Topical, FaizaFoxy na wengine wengi wanaona matatizo yote ya waislam yamesababishwa na bado yanaendelezwa na kanisa(Mfumo Kristu). Hapa mimi nakubali kuwa wanatafuta tu kizingizio baada ya kuona udhaifu wao na kushindwa kutatua matatizo yao wenyewe.
Huu utitiri wa taasisi za kiislam kuanzia Bakwata na nyinginezo zinawakilisha vikundi gani vya waislam? Sasa kama umoja wenyewe haupo na kuna vikundi tu , hizi kelele za kupinga mfumo kristu/MoU zitafika wapi? Hivi badala ya kwenda Diamond Jubilee na kuzunguka nchi nzima kuhamasisha waislam kupinga mfumo kristu, kwanini waislam wasikae chini kwanza na kuanza mchakato wa kuunda chombo/taasisi moja ambayo itakuwa ndiyo inawakilisha sauti ya waislam wote Tanzania nzima?
Mimi nadhani haya makelele ya uhalali wa MoU na mfumo kristo tungekuwa tunayajadili katika angle tofauti kabisa kama hawa wenzetu wangekuwa na viongozi wa dini wenye uwezo wa kutoka nje ya box!
mkuu wangu narudi ktk mjadala wetu..
Umeweza kuonyesha lawama zako lakini Je, umesoma MoU na kuuelewa kiasi kwamba ukazungumza points zako kulingana ama hasira za hawa kina Tropical ndizo zinakufanya usitazame upande wa pili wa malalamishi yao..

Swala la Nyerere liweke kando wanazo sababu zao kama unavyotetea wewe huu muafaka..unavyowashangaa wao ndivyo navyokushangaa wewe pamoja na wao. Nakuomba sana usome vizuri na taratibu upate kuuelewa, utaona kwamba muafaka huu umetayarishwa na kanisa na Lowassa kenda kusaini tu. Inakuwaje serikali yetu ambayo haina dini inaingia muafaka kama huu wenye kuunda Christian Commission body yenye mamlaka makubwa kama yalivyoorodheshwa wakati wakitumia kodi ya wananchi wote - huoni tatizo hapo mkuu wangu!..

Mkuu tuwe wakweli na roho zetu wenyewe, huu muafaka wenu kama ungeandikwa kwa waislaam bila wakristu kuwa na kitu kama hiki sidhani kama tungekuwa tukiongea haya leo hapa JF. Na utanisamehe sana lakini kwa jinsi mnavyotetea na kubisha inanipa picha tofauti kabisa ya kwamba pengine ndio katika yale yale ya kusoma lakini hatukuelimika! (lugha ya kigeni)..Yaani watu wanausoma muafaka lakini hawaelewi athari zake..Imekuwa, maadam gari linakwenda basi tutafika salama kama abiria wa daladala wanavyojazana na wasijali usalama wao. Nakuomba sana usomeni kwa makini mkiwa nje ya box la udini pengine hamkuusoma ila mnachukulia vitu kwa hisia zenu zaidi..
 
Hahahahaha Call me mdini ,mkabila au vyovyte lakini usipotaka kufanya analytical apprrocah kutafuta au kufafanua tatizo huwezi kujua chanzo cha tatizo. U will end fighting the right war agaisnt the wrong enemy

Ebu Nikuulize naomba unipe mtazamo wako ili tutafute jibu

  • Kwa nini ilianzishwa baada ya Nyerere na si wakati wa nyerere?
  • Kwa nini Mou Hii ilikuja wakati wa Alhaj Mwinyi?
  • Kwa nini Mkapa pamoja uwezo wa kifedha wa serikali iliyoweka hakujenga hopitali nyingine ya rufaa yenye hadhi mkoa wowote
  • Kwa nini Kikwete naye anaendeleza yale yale aliyoacha Mwinyi na kuendelzwa na Mkapa ?

katika kujibu zingatia dondooo hizi amabazo badhi yake nimezitaja wenye coment nyingine

  • Kama tunadhani chanzo halisi cha tatizo ni "mfumo kristo" kwa nini baadhi ya waaisisi wa huu mfumo wamo kina rashid, juma, bakari.? Kwa nini bado kuna kina john, Silvanus, David nao wanaathirika na huu mfumo
  • Baada ya kusoma soma Nimeona MoU sio Legal Binding document. Kwa nini Jakaya Kikwete haifuti. Kwa nini mkapa hakuifuta?
  • Priority ya Mfumo wa siasa tanzania uko wapi? kwenye huduma za jamii au kwenye siasa.?Kwa nini serikali iinaazisha wailaya au mikoa ya Kisiasa sehemu amabzo hazina huduma. Angalia kiwkete kaazisha wialaya ngapi. ulizia hizo sehemu alizoanziiha wilaya zina huduma gani.Kwa nini kabla ya kuanzisha tawala za kisiasa wasihakikkishe kuna hudum za kijamii. Nani wa kulaumiwa kama serikali inakimbilia kuanzisha wilaya na kanisa linakimbia kuanzisha hospitali.? Kipi cha muhimu wilaya moja itengwe kwenye majimbo mawili ya uchaguzi (Kisiasa) au wilaya mja ibaki ni jimbo moja na seriali ijenge hospitali. kuliko kuwa na maimbo mawili bila hospitali ya wilaya.
Kwa hiyo Topical I happened to be a christian but I can analyse any problem with an open mind

a. Afadhali ume-admitt kwamba ni mdini so lazima utatetea as long fedha umma zitafaidisha miradi ya kanisa ..kama wadini wengine wengi walivyofanya kwenye mambo mengine na au wataendelea kufanya ufisadi huo huku wakifikiri ni jambo jema kwa dini yao kufaidi mali za umma

b. Kwanini zote ulizouliza jibu lake ni kwamba wanatumikia mfumo kristo ..of course kila fisadi anatumia ujanja mwingi ukiwemo ku-lobby political decisions..kama ambavyo wamefanya kina RA na EL hivyo hivyo wamefanya maaskofu na watetezi wao wamewaweka kila kona knowingly or unknowingly wanatetea mafisdi ..kwahiyo kanisa limelobby kufisadi mali ya umma billions @ year..unaudited

c. oh gosh kumbe bado unafikiri kila juma ni muislam na kila john ni mkristo na kwamba mafisadi wanampango wa kuwafaidisha either of them ..kwa ufupi hao wanaochukua hizo pesa si kwamba wanataka sana kuwafaidisha wakristo..kama ingekuwa hivyo wala isingekuwa ingekuwa open MoU to any institution or religious kupata fursa from very begining na ingekuwa pia open to audit hiyo mimi naitazama kama kichaka cha kufanya uchafu kama ule unaofanywa na epa/richmond in the name of church services..

d. Kwanini JK hafuti unasahau kuwa JK ni mwanasiasa na mwanasiasa anahitaji madaraka na hicho kinaweza kuwa kichaka chake cha kuvuta pesa za umma..kama ambavyo ameshindwa kufuta epa/doawans hizo weakenesses anazo bado..na ataandelea kuwa nazo..kwakuwa naona kama loophole ya kufanya ufisadi unaudited..na watu kama nyinyi mmeshakubali hali hiyo kwa hiyo kwakuwa unaamini maaskofu ni mungu fulani au dini yako ni muhimu sana (udini) wanakula kwa raha zao..

e. Hawaanzishi hospitali kwasababu ya kutumikia mfumo kristo..mkuu niliwahi kusema hapa kuwa hela za umma zinazoenda kwa mfano hospitali Muheza DDH zingetosha kujenga hospitali ya hadhi ya wilaya muheza bila kufanya utaratibu huu wa kibaguzi na kifisadi..kwanini hawafanyi wanaogopa christian lobbyist group iliyoko serikalini ambayo inafanya kazi ya kusaidia kanisa badala ya taifa.. hakuna logic yeyote ile ya ku-finance mradi wa kanisa na kuacha kujenga na ku-finance miradi ya serikali zaidi ya ufisadi na christian lobbyist for state cake..

Zing bado sana hujaweza kutoka kwenye box la udini ..safari ndefu sana..kw ataifa hili kupata watumishi wanaotumikia taifa na siyo kanisa..kwasababu hilo likitokea hiyo paradox ni very simple ku-i-ondosha..
 
Serikali iepuke Negotiations za namna hii zinatia wasiwasi. Kwa nini iwe Kanisa peke yake? Memorandum ya namna hii ihusishe Dini na madhehebu mengine. Serikali inaongoza wananchi siyo Kanisa. MoU ya Serikali ni kwa manufaa ya nchi siyo Kanisa. Serikali yetu haina Dini ila watu wake wana Dini, wakipewa madaraka ya serikali wasi assume dogma za Dini zao.Kufanya hivyo ni kukaribisha mkanganyiko wa kisiasa, kiitikadi, kifalsafa na kiutawala.Wenye nchi mpo!

Can you also say 'serikali iepuke kusaidiwa na taasisi za kidini?' Lets be constructive guys, huu si mkataba wa kuipendelea dini fulani, ni mkataba wa kuisaidia dini fulani ktk kuendesha majukumu iliyoamua kuyabeba ktk kuendesha shughuli za kijamii. Katika hizo articles sijaona sehemu iliyoandikwa tax reductions for bibles and church benches. Kwote ni education, health n.k ambazo ni huduma kwa jamii.

Sidhani km serikali yoyote yenye ugumu wa kuwapatia wananchi wake huduma hizi itakataa kusign the same MoU with other religious missions if they are not churches, or may be I don't understand ni nini manung'uniko hapa. Tutumie akili zetu kiutulivu ndio tutaelewa nani ni mnufaikaji wa hii MoU, KANISA, SERIKALI au WANANCHI.
 
Yataka moyo lakini inapolazimika hakuna budi ila kupasua ukweli. Ni kanisa
ndilo ambalo linahusika na utendaji mbovu wa serikali ya muheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete. Yawezekana ana mapungufu yake katika utendaji
lakini kuna watu wamekaa katika ofisi za serikali kwa manufaa ya kanisa hivyo
wako tayari kuvuruga mambo ili utendaji wa Kikwete uonekane mbovu na si
Kikwete tu hili ni kwa mtawala yeyote ambaye ataonekana kuwa na angalau
kaharufu ka - uislamu.

Kwa maslahi ya kanisa hilohilo hata waandishi wa habari nao wamekuwa mstari
wa mbele kumchafua Kikwete. Na hii ndiyo maana pamoja na utendaji mbovu
kabisa wa B.W Mkapa bado mapungufu yake hayaonekani na amekuwa akibeba
sifa kubwa sana za kukuza uchumi huku ufisani uliofanyika kipindi chake ukifumbiwa
macho. Ni kanisa hilo hilo ambalo limehusika na kushusha hadhi ya
Rais wa awamu ya pili ndugu A.H. Mwinyi.

SULUHISHO.Kanisa liache kufanya mambo nyuma ya pazia!
 
Kikulacho ki nguoni mwako. Kama JK kachafuka,sababu siyo makanisa. Ajiangalie wapi mambo hayaendi vile inavyotakiwa. Makanisa hayana muda huo unaofikiria wanao wa kutengeneza majungu na fitna. Sio haiba yao.
 
Back
Top Bottom