Kwa hiyo dr slaa, ukipata urais utazirudisha shule hizi kwa kanisa? Au utachukua maamuzi gani
Sidhani kama hili ni tamko la Dr.Slaa kama mtoa mada ulivyoliweka.Ingekuwa sahihi zaidi kama ungeuchukulia huu kama ufafanuzi wa Dr.Slaa.Sio tamko.Tamko is more demanding,this one here presented by him is quite descriptive.Sio kila kitu ni tamko.Hili sio tamko,huu ni ufafanuzi.
Candid Scope,Mtaongea vibaya kuhusu huduma za makanisa, lakini kesho mtapeleka wagonjwa huko, mna watoto mnaowapeleka kusoma katika shule hizo, sawa na kukata tawi ulilolikalia. Viongozi wengi waandamizi serikalini kutoka dini mbalimbali na wakana dini wengi wamepitia shule hizo. Basi waungwana na wastaarabu wanaona bora kunyamaza kwa ajili ya kutunza amani maana ukimnyanyulia jambia kichaa utaonekana we ndo mwenye tatizo.
Yeriko leo kapiga viroba dini yake na chama chake ndio zao
Unafikiri watapeleka? Watakazania kupiga domo tu. Ndivyo walivyo na bahati mbaya hata wajijui.Kikwete kishawaambia pale Dodoma kuwa pelekeni maombi yenu. Changamkieni tenda!
Nisaidieni kufahamu zaidi, hii safari ya negotiation (makubaliano) baina ya serikali na taasisi za kidini, naona ilianza na dini zote, lakini baadaye MOU imebaki kati ya taasisi za kikristo na serikali, ili hali taasisi za kiislamu hazionekani? au walijitoa? ama hawakuwa na kitu kilichotaifishwa sasa ikabidi wasihusishwe?
1) Kuhus uwezo wangu wa kufikiri kuwa mdogo, sishangai sana maana serikali iliamua kuwasomesheni nyie na ikatuacha sisi wapweke.
2) Nafasi za ualimu huwa zinatolewa kwa merit sio itikadi. Kwani wanaosoma kwenye vyuo vya ualimu si watanzania? Kwa nini kanisa litake upendeleo kwa wakristo pekee?
3) Serikali sio tu facilitator kwa Ujerumani bali na wafadhili wengine. Kwani kuna kosa gani serikali leo kujiunga na OIC, ikiwa watakaonufaika ni waislamu ambao nap ni raia wa Tanzania?
nimekuuiza serikali ya ccm/kikwete wanatetea maslahi ya kanisa? kutoupenda kwangu uislam ni sawasawa na kama yule ambaye labda hapendi kuvaa nguo ya dhambarau lakini akiona mwenzake amevaa nguo ya rangi hiyo anakuwa hana tatizo...nina maana mimi binafsi uislam haunivutii lakini sina shida na muislam ...nijibu swali langu hapo juu...Usiwe na akili fupi kama maisha ya funza, wewe unaupenda Uislam?
Dr.Tunashukuru kwa ufafanuzi wako mwanana.Serikali ya CCM inaelewa ukweli wote lakini kwa makusudi inawahadaa Waislamu kwa kutowaambia ukweli ili watu wafarakane kidini na yenyewe ipumue kwani ina stress ya kushindwa kuwaletea Watanzania Maisha Bora iliyowaahidi.Inaelewa Mashekh wengi(mf.shekh Ponda)hawana uwezo wa kufanya Research na hivyo ni wepesi wa kudanganyika.Serikali makini haiwezi kutegemea Cheap politics kama hizi.Tujiulize,Muda wote huu Waislamu wanavyopiga kelele kuhusu MOU kwa nini Serikali yenye kuujua ukweli wote isiwaambie ukweli?Hapo ndipo wenye akili huamini kwamba Waislamu hutumwa kuhubiri chuki.
Kutokana na maelezo ya Dr Slaa, inaonekana Bakwata walikuwepo mwanzoni; ila mambo yaliyokuwa yanajadiliwa yakawa hayawahusu. Maanake hapo suala ilikuwa ni kuhudumia taasisi zilizotaifishwa na serikali. Watoa misaada wakawa hawapendi tabia ya serikali kubinafsisha taasisi kiholela halafu inazitelekeza. Sasa wakaweka masharti lengo ikiwa ni kuzuia utaifishaji huu holela na utelekezaji ili huduma ziendelee. Sasa hapa ukiangalia nahisi Bakwata hawakuwa na interrest katika mambo haya - si kwa sababu hawakutaka, bali majadiliano yenyewe hayakuwahusu sana.
Mkuu weka kumbukumbu sawa sio kanisa lililotoa tamko kuwa Kikwete ni chaguo la MUngu ni Askofu Method Kilaeni halikuwa tamko la kanisa kwa mantiki kwamba alitoa kauli hiyo kwa maelekezo ya kanisa lakini pia kanisa katoliki haliwakilishi wakristo wote hata kama Kilaeni angekuwa ametoa kauli hiyo kwa niaba ya wakatoliki.
Watoto wetu na vizazi vijavyo visije kupokea kumbukumbu potofu.
Fresh,
Ukifuatilia majibu ya Mnyamahodzo na wengine utaona maswali yako 2 yamejibiwa kwa kina ila inaonekana sio majibu uliyoyataka.
Naomba nikufahamishe hivi ya kuwa ktk mikataba kuna vitu vingi vya msingi mbali na maandishi na saini ambavyo kwa pamoja huusababisha mkatana kutekelezeka na kueleweka. Moja ya kanuni za kutafsiri sheria na mikataba zinalazimisha kuheshimiwa kwa kanuni ya "Rule of Context". Huwezi kuchagua/kuchomoa sentensi fulani kisha ukaitoa nje ya muktadha na kuipa tafsiri au kutaka ipewe tafsiri kinyume na mwili wa mkataba.
Nijibu swali lako la pili, kama ulivyosisitiza hapo juu kwa kupigia mstari. Nitaenda kwa urefu kidogo.
Kanisa lilikuwa linakubaliana na serikali ya Tanzania kuhusu namna ya kutoa huduma zilizotajwa na kujadiliwa kwa kina huko juu/nyuma. Kanisa kwa vile lina utaratibu wa kutoa huduma bora likasisitiza kuwa ubora walimu watakofundisha shule (zitakazoendeshwa na kanisa) lazima uheshimiwe na kutambuliwa. Hivyo wakaleta hoja mezani kuwa serikali itoe nafasi (wewe unasoma upendeleo) kwa walimu wenye sifa kupata mafunzo.
Wewe ulitaka kuwe na kitu kama hiki'....earmarked for state (or) muslim owned schools' ndipo hisia zako zingetulia kidogo, sio?
Well, sasa kama Kanisa lingesema hiyo sentensi (nadhani ambayo wewe ulitaka iwe) je hiyo MOU ingekuwa ni baina/kati ya Serikali vs nani? i.e. offer and receivership. Kuwepo kwa hicho kipengele ktk MOU kunalazimisha kutambulika kuwa wakishahitimu wataenda wapi.
Kwa mfano Kanisa lingesema Serikali itoe mafunzo halafu lisiseme wakifuzu wataenda wapi, Serikali huenda ingekataa maana haikuwa na fedha za kutoa huduma mama husika sembuse kufikiria kutoa ajira mpya, kwani haikuwa na uwezo wa kifedha wakati. Kanisa liliweka bayana kuwa litateua watu wenye sifa na kisha litawapokea na kuwapangia kazi (ajira). Kanisa halikusema litapeleka watu wa dhehebu fulani tu, bali wenye sifa/uwezo ndio kigezo! Na hao wahitimu hawekuwa wanakwenda kufanya kazi kanisani bali mashuleni, hivyo dhana ya Kanisa kufaidika kama Kanisa ni dhaifu mno
Na kama hoja hiyo inakuumiza na kukuchefua hebu jiulize ni vipi leo inakuwa maelfu ya walimu wanahitimu kila mwaka ..... je ni % wanaopata ajira, hasa serikalini? Nadhani unaona bayana kuwa hoja yako inaelea hewani na kupotelea huko!
Kwa hivyo in context, ni kuwa Kanisa liliitaka Serikali iheshimu na kuwajibika kimkataba juu hoja muhimu ya ubora wa walimu kama sehemu ya utekelezaji wa MOU nzima. Jitahidi usisome zaidi ya kilichoandikwa.
I hope hii MOU ni Ya ukweli, sio chapisha chapisha, I question as to why the copy was never accesable to the HON DR SLAA, ikabidi iwekwe hapa na mtu mwengine, and than we suddenly see the HON Dr coming up with these full length explanations. I also wonder if the HON DR will he ever make an Impartial Leader who shall never succumb in Religion Favourism and total Nepotism like the claims of Wana CDM kuwa The First Lady to be runs the show at the CDM HQ. Lets be very coutious NDUGU WATANZANIA
Hapo mwanzo nilijua kuwa serikali haitoi fedha taslimu bali inatoa ruzuku kwa huduma za kijamii zinazotolewa na kanisa lakini sasa kuna suala la makanisa ya ujerumani limeingia ndani ya hoja hii. Inachanganya kidogo.
Mungu si Athman! Propaganda za ukanda mnazozieneza dhidi ya CHADEMA hatimae na za udini zimeanza kuwagawa Pro-CCM humu jamvini. MAMA POROJO ile kazi ya ukanda unayoifanya dhidi ya CHADEMA madhara yake ni kama haya unayoyasema.
TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
Kusema tu kuwa hana akili kwa vile anatetea haki yake hakusaidii. Mimi nimeisoma MoU vizuri na kama unaweza jibu haya maswali hapa chini yanayotoana na MoU:
By Freshthinking
Ufisadi wa MoU uko hapa ambapo DR Slaa nasikitika hakuweza kutuelezea kwa undani:
‘The government shall provide vacancies in its Teachers training colleges for training qualified persons as teachers earmarked for church owned schools'. Article xi
‘The government shall endeavour to include financial assistance for church run social services in its bilateral negotiations particularly with the Federal Government of Germany. Consideration shall be made during its bilateral negotiations with other donors'. Article xiii.
Sasa wakristo tujadiliane kwa hoja:
1)Hivi ni haki kwa serikali isiyokuwa na dini kutowa nafasi za upendeleo kwenye elimu kama artcle xi inavyosema, tena isitoshe kw manufaa ya kanisa?
2)Ni haki kwa serikali isiyokuwa na dini kuombea kanisa misaada katika Nyanja za kimataifa.
Sasa hapa ni kipi mnahitaji kuoneshwa ili muamini kwamba serikali inawazunguka waislam?
Mungu si Athman! Propaganda za ukanda mnazozieneza dhidi ya CHADEMA hatimae na za udini zimeanza kuwagawa Pro-CCM humu jamvini. MAMA POROJO ile kazi ya ukanda unayoifanya dhidi ya CHADEMA madhara yake ni kama haya unayoyasema.
TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com