Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

ni ajabu sana mohamed said hajatia neno kwenye mjadala huu wakati yeye ni mmoja wa vinara wa wahubiri mou...
 
Habari wa JF
Nadhani ni busara kujadili mada kwa uhalisia na kwa kujenga hoja. Si uuungwana hata kidogo kuacha kujadili hoja na kuanza kumjadili mtu. Kama kuna hoja ya MOU ya waislam kutokupewa nafasi ya kusikilizwa ni busara kueleza nini kilijili hadi ikawa hivyo ( na wenye kujadili sharti wawe na taarufa sahihi si hisia tu). Mwisho tukumbuke kuwa kuendekeza hisia za udini haitakuwa na TIJA kwa kundi lolote.
 
Kwa kuwa humu JF kuna wabunge tena wa pande zote: chama tawala na upinzani. Tena wapo waislamu na wakristo.

Tuwaombe John Mnyika, Zitto, Tundu Lissu, HKigwangalla, Dr F. Ndugulile n.k. walipeleke hili suala kama swali kwa Waziri mkuu, au hoja binafsi inayoomba maelezo ya kina ya serikali, na ipate muda wa kujadiliwa ili kuondoa usiri uliopo, na kuweka wazi mambo yaliyopo kama ni kwa maslahi ya watanzania wote au vikundi fulani tu.
 
Last edited by a moderator:

Ndiyo CCM wana maslahi na Kanisa wanamuenzi muanzilishi wa CCM Nyerere. Lete swali lingine.
 

Niruhusu nikuulize swali rahisi lakini litakalokupa ufahamu rafiki, swali lenyewe ni hili: Kwa mfano Tanzania wanawake wanaishi takriban miaka 54 na wanaume kwenye 50, kwa hiyo kwa kuwa tumeshindwa kuhakikisha life expectancy ya wanaume inalingana na ya wanawake, basi tuwaue wanawake wote mara wafikishapo umri wa miaka 50 for the sake of equality?

Logic ya swali hili ni kwamba idea ya kwamba MoU ifutwe ili waislam wawe sawa na wakristo haina tofauti yoyote na ile ya kuwaua wanawake mapema ili wafe katika umri sawa na wanaume. Ni jambo gani hasa gumu kwa ndugu zetu wa kiislamu kujiorganize na kujenga mashule, mahospitali, vyuo n.k na kisha kuomba serikali kusaidia? Nchi hii inahitaji huduma zaidi na zaidi na sio kubomoa zile ambazo tayari zipo. Ninyi watu wachache acheni kudhalilisha dini ya kiislamu kwa ku argue vitu ambavyo hata mtoto wa kindergaten hawezi kuargue. Ni hilo tu, ukitaka kunisikia sikia, otherwise endeleeni kujidhalilisha na kuidhalilisha dini ya kiislamu.
 
Bw. Ritz,
Wewe wasema.Mbona hata kabla Dr. hajasema neno lolote juu ya MOU bado lawama na manunguniko vilijaa kila kona?Of coz, sijaona pia alikosema (by implication) kwa kutumia nafasi yoyote iwe ya chama au kanisa, bali hayo ni maoni yake kama mwananchi mwenye kujua chochote juu ya MOU. Ritz, we can be far better without these unwarranted things.
 
All what i can see,kuna vitu vimejificha sana katika hilo,ila kiukweli we as muslims we are not stupidy to the extent of failing to realize whats going on until now,tunajua sana, MARA NYINGI USIRI WA MAAMUZ FLANI MAZITO KWENYE JAMII YA IMAN MCHANGANYIKO KAMA HII UNALETA TAHARUKI SANA HASA KUNAPOTOKEA DUKU DUKU ZA KUTORIDHIKA KWA JAMII MOJAWAPO, MAY BE NI UKWELI WA KWAMBA SERIKALI INAPOTOSHA AU LA,ILA HOJA KUU YA WAISLAM SIYO KUICHUKIA MOU HIYO,LA HASHA,USIRI WA NINI KATIKA MAAMUZ NYETI KAMA HAYO KWA JAMII YOTE KWA UJUMLA?PIA KWANINI ILIPOKUJA HOJA YA OIC WATU WAKAANGALUWA KWA JICHO LA TAHADHARI TAKITKA OMBI LAO HILO!?TUSIMEZE MEZE MANENO..
 

Shule nzuri sana jamani

Shule zilizofanya vibaya Matokeo ya Form II


Kwa upande wa shule za serikali zilizofanya vibaya ni Mihambwe, Dinduma, Kiromba, Marambo, Mbembaleo, Kinjumbi, Litipu, Luagala, Miguruwe na Napacho ambazo zote ni kutoka mikoa ya kusini – Mtwara na Lindi (KULEKULE PALIPOUNGUA SHOKA UKABAKI MPINI)



Kwa upande wa shule zisizo za serikali ni Mfuru-Kisarawe, Pwani-Kulekule, Doreta, Kigurunyembe, Ruruma-walewale, At-taaun, Jabal hira, Mkono wa Mara, Kilepile na Kiuma. (NYINGI NI ZILEZILE JANA, LEO, KESHO NA HATA KESHOKUTWA ITABAKI KUWA HIVI)
 
Waislamu wenzangu, naona hakuna haja tena ya kuendeleza malumbano kuhusu hili suala, limetolewa ufafanuzi wa kutosha na kushibisha.

Asante sana kwa mfafanuzi husika.
 

wakati mwingine kusikiliza kwingi ni kuelewa zaidi. Mchango wako umenifunza kwamba kwenye sheria na mikataba huwezi kuleta tafsiri binafsi na hiyo ni kinyume cha sheria. Mantiki ni kwamba dhana inapoteza lengo au dhamira yake.

Wanasheria hapa JF wanaweza kutusaidia zaidi kupata tafsiri bora kuliko kila mtu kutumia kiingereza alichojifunza darasani na kudhani kinatosha kutoa tafsiri fasaha.
 
Tutumie busara zaidi kujadili na kufahamishana mambo ya muhimu kama haya. Tusishambuliane kwa miamvuli ya
dini zetu. Mimi mkristo lakini nina marafiki wangu Waislamu, ambao wanajua VIZURI kuruan huwa wana argue vizuri
tofauti na wale wavivu wa kusoma ambao wanasikiliza propaganda za wachumia tumbo wa mtaani wakidhani ndio dini
inavyotaka. Nani hajui kwamba hospitali AU shule za kikristo haziko kwa ajili ya Katangaza dini ila kuhudumia watu wote (waislam,
wakristo, wahindu, ........... na wapagani). Nawaomba waislam wanaoijua vizuri dini yao waitumie vizuri elimu na karama waliyonayo
kusaidia kuwaelemisha wenzetu ambao huwa ni kufuata mkumbo tu. MUNGU NI MMOJA WOTE TU WATOTO WAKE, KWANGU
NI NEEMA YA MUNGU TU KUZALIWA KWENYE FAMILIA YA KIKRISTO NDIO NIKAWA MKRISTO, HIVYO TUSHIKAMANE KUPIGANA
NA DHULUMA YOYOTE NA TUUNGANE NA WALE WANAOTUONYESHA NJIA BILA KUJALI DINI ZAO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 

nimechelewa lakin nimekuja.....

wimbi la mbele, weka nakala ya hiyo MoU mliyopeleka serikalin ikakataliwa, sema mlimpelekea nani/ wizara gani, eleza huyo aliyekataa alitoa sababu gani kuikataa, ikiwezekana mtaja kwa jina huyo aliyekataa kwa niaba ya serikali na baada ya kuikataa eleza waislamu mlichukua hatua gan?

BTW, ni wazi, kama ilivyo ada, Mungu/Miungu ya theists, hususani Huyu/hii Mungu/Miungu ya kikoloni, ina kiu kali ya kunywa damu na nyama za wana wa Tanzania....nitarejea kufafanua
 
Well done.

Tatizo kuna baadhi ya watu wako too "isms" hapa. Lakini kama wote tungetumia bongo zetu kidogo tu tena kwa uhuru basi haya malalamiko na purukushani zote zingeshakwisha.

Sadly, the seed of hatred has been sown already. The imprint of Nape, Mwigulu & CCM and it will certainly cost this nation something valuable.
 
 


Nina mashaka kama Waziri Mkuu bungeni atakuja na majibu tofauti na ya Rais. Haya chini. kumbuka kauli ya Rais ni kauli ya serikali ingawa inaweza kutolewa ufafanuzi zaidi kama inaleta mkanganyiko kwa jamii. hata hivyo, kwa kundi la Waislamu pengine wanahitaji maelezo zaidi ingawa maelezo ya rais yanaonyesha Bakwata wamepeleka maombi ya MOU.

Mheshimiwa Mufti;


Serikali ina msimamo huo kwa sababu tunatambua na kuthamini sana nafasi na mchango wa dini na mashirika ya dini katika maendeleo na ustawi wa jamii na nchi yetu kwa ujumla. Serikali inaunga mkono mashirika ya dini katika shughuli zao kwa sababu ya manufaa ya dhahiri ya shughuli hizo kwa taifa letu. Mashirika ya dini yamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali kuwapatia wananchi wa Tanzania huduma muhimu za elimu, afya, maji n.k. Bila ya ushirikiano, upatikanaji wa huduma hizo kwa baadhi ya maeneo ungekuwa tofauti sana. Serikali kwa upande wake imekuwa inafanya kazi ya kusaidia mashirika ya dini yaweze kutoa huduma hizo kwa wananchi.

Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna kitu cho chote ambacho Serikali itatoa kwa dini moja ambacho dini nyingine itanyimwa. Kwa kweli mbele ya Serikali dini zote zina haki sawa. Kama hujaomba usimlaumu aliyeomba akapewa au aliyempa . Kama yupo anayeamini anazo sifa kama mwenzake aliyepewa aombe naamini atapewa. Iwapo itafanyika vinginevyo dai haki yako kwa mamlaka zinazohusika.
Mheshimiwa Mufti, Ndugu Zangu Waislamu;


Maelezo yangu haya yanafanana na hoja zenu katika Risala yenu kuhusu Itifaki ya Maridhiano ya 1992 baina ya Serikali na TEC na CCT. Nafurahi kwamba na nyie mmeamua kuleta maombi, yaleteni yatashughulikiwa ipasavyo.

Hotuba yote imenukuliwa hapa: HOTUBA YA MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE BARAZA LA EID-EL-FITR, DODOMA AGOSTI 2011 - Global Publishers
 
dr. kumbe nae yumo kwenye MoU?

kwa hiyo kama yumo.? Unataka kumbebesha MOU. Vipi Ali Hassan Mwinyi kama rais wakati huo, vipi Lowassa akiwa waziri alietia sain. Upeo wako umegota kwa dr.Slaa tu.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…