na ni kweli hujaelewa....nikusaidie ili uelewe ni hivi ndg.Dr. Slaa ametoa ufanunuzi wa MOU kama JF Senior Expert Member-Verified User.pitia JF a/c yake kwa uthibitisho zaidi mkuu.Mimi labda sijaelewa Slaa anatolea ufafanuzi kama msemaji wa kanisa au kiongozi wa chadema.Babu mbona unatuchanganya uko upande upi
Kwa hiyo hauna imani na serikali?Nina mashaka kama Waziri Mkuu bungeni atakuja na majibu tofauti na ya Rais. Haya chini. kumbuka kauli ya Rais ni kauli ya serikali ingawa inaweza kutolewa ufafanuzi zaidi kama inaleta mkanganyiko kwa jamii. hata hivyo, kwa kundi la Waislamu pengine wanahitaji maelezo zaidi ingawa maelezo ya rais yanaonyesha Bakwata wamepeleka maombi ya MOU.
Mheshimiwa Mufti;
Serikali ina msimamo huo kwa sababu tunatambua na kuthamini sana nafasi na mchango wa dini na mashirika ya dini katika maendeleo na ustawi wa jamii na nchi yetu kwa ujumla. Serikali inaunga mkono mashirika ya dini katika shughuli zao kwa sababu ya manufaa ya dhahiri ya shughuli hizo kwa taifa letu. Mashirika ya dini yamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali kuwapatia wananchi wa Tanzania huduma muhimu za elimu, afya, maji n.k. Bila ya ushirikiano, upatikanaji wa huduma hizo kwa baadhi ya maeneo ungekuwa tofauti sana. Serikali kwa upande wake imekuwa inafanya kazi ya kusaidia mashirika ya dini yaweze kutoa huduma hizo kwa wananchi.
Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna kitu cho chote ambacho Serikali itatoa kwa dini moja ambacho dini nyingine itanyimwa. Kwa kweli mbele ya Serikali dini zote zina haki sawa. Kama hujaomba usimlaumu aliyeomba akapewa au aliyempa . Kama yupo anayeamini anazo sifa kama mwenzake aliyepewa aombe naamini atapewa. Iwapo itafanyika vinginevyo dai haki yako kwa mamlaka zinazohusika.
Mheshimiwa Mufti, Ndugu Zangu Waislamu;
Maelezo yangu haya yanafanana na hoja zenu katika Risala yenu kuhusu Itifaki ya Maridhiano ya 1992 baina ya Serikali na TEC na CCT. Nafurahi kwamba na nyie mmeamua kuleta maombi, yaleteni yatashughulikiwa ipasavyo.
Hotuba yote imenukuliwa hapa: HOTUBA YA MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE BARAZA LA EID-EL-FITR, DODOMA AGOSTI 2011 - Global Publishers
..Well done.
Tatizo kuna baadhi ya watu wako too "isms" hapa. Lakini kama wote tungetumia bongo zetu kidogo tu tena kwa uhuru basi haya malalamiko na purukushani zote zingeshakwisha.
Sadly, the seed of hatred has been sowed already. The imprint of Nape, Mwigulu & CCM and it will certainly cost this nation something valuable.
It doesnt mattaer kinachotakiwa ni kuwa na taifa lenye usawa sio kupendelea kundi fulani na kiliacha kundi jingine huku mkidai kuwa hawataki kusoma.
Ondoeni huu ufisadi wenu, hamna hata haya. Halafu kiongozi mkubwa kama Dr Slaa anatetea MoU!
Hizo kodi zinazosomeshewa walimu wa shule za kanisa (kwa mujibu wa article ya xi ya MoU) zinatunzwa kwa kodi za wakristo peke yao?
Ukurasa wa nje wa MoU una maneno yafuatayo:wewe huna akili kabisa MOU imeisoma vizuri? pesa inatoka serikali ya ujerumani unyonyesha ni wapi serikali yetu ya tanzania ilikubali kutoa pesa.
Kimsingi mleta mada amekosea sana kuchukua bandiko la Dr Slaa alilochangia kwenye uzi mwingine na kulianzishia uzi mpya kama TAMKO LA DR SLAA KUHUSU MOU kusapori uwepo wa MOU
Dr Slaa aliandika bandiko hili kutokana na trend ya uzi ule hivyo kulifanya ndio tamko kuu lake kuu kuhusu MOU kunaacha gap kubwa sana
Ukiangalia kimantiki Dr Slaa katika bandiko lake amejaribu tu kuelezea historia ya MOU na si kujikita na contents za MOU ambazo ndio msingi mkuu wa wanaolalamikia MOU kama inapendelea upande fulani
Na ukienda mbali zaidi Dr Slaa anonyesha mshangao wa kwa mara ya kwanza ndio anauona mkataba huo wa MOU hapa JF maana hata yeye hajawahi kuwanao
Kwa mantiki hii ya kuuona hapa kwa mara ya kwanza kunatuambia kwamba hata yeye alikuwa hajui kinagaubaga cintents za MOU hii inayopigiwa kelele
Binafsi sina tatizo kabisa na Dr Slaa kwa bandiko lake kwenye uzi mwingine maana aliliweka kulingana na flow ya uzi ule lakini kulichukua bandiko hilo na kulifanya ndio uamuzi na tamko la mwisho la Dr Slaa si sahihi kabisa maana tamko hili halijajibu chochote kuhusu kilichomo ndani ya MOU zaidi ya historia ya MOU. Kinacho watatiza watu wengi si kwanini GVT imeingia MOU na makanisa isipokuwa ni MOU yenyewe ilivyokaa
Kwa mtazamo wangu labda DR aje hapa kutoa ufafanuzi zaidi juu ya "tamko" lake na kujazia yale ya msingi yanayodaiwa kupotoshwa ndani ya MOU.
Vinginevyo tuheshimu tu huu ni mchango wake kwenye uzi flani na si kuufanya ndio tamko lake kama mleta maada alivyofanya akisaidiwa na MOd
hutajibiwa! MoU ilifungwa kiusiri na kila kinachoizunguka MoU ni usiri tu!sawa kaka, iwe iwavyo, nachelea tunaanzia kufikiria kuanzia katikati badala ya kuanzia mwanzo. tutafute backgroud information ya MoU kwanza. Kama ilivyo kwenye maandishi ya Dr Slaa, haidhuru kama ni ufafanuzi au ni tamko, cha msingi ni elimu, au hata ukipenda ilmu aliyotoa. tujiulize kwanza, kwa mfano:
- MoU ni nini?
- Nini kilisababisha iwepo?
- Je hizo sababu sababishi zina ukhalali, kisheria, kimantiki na morally?
- Je uwepo wa MoU umekuwa kwa faida ya nani? yaan MoU hiyo imekuwa ikihudumia kina nan? ikiwezekana hapa tupewe data kwa majina na kila jina gharama ilizofaida kama matokeo ya uwepo wa MoU.
- Je kama MoU imeondokea kuwa na faida kwa watanzania, je kumekuwepo/kupo uwezekano wa makundi mengine nayo kuwa na kitu kama hicho? kama ni ndiyo hayo makundi mengine yaliwahi kuomba kuwa na kitu kama hicho? kama ni ndiyo walikubaliwa? kama ni hapana. je kwa nini walikataliwa? Je sababu za kukataliwa zina ukhalili kisheria, morally au vinginevyo? Kama hazina ukhalali ina maana kuna mtu alikosea, kama ndivyo jee kosa linaweza kurekebishwa sasa kwa makundi mengine nayo kuwa na MoU? Je ni sifa gani zitakiwazo kundi liwe nazo ili kwazo listahiki kuwa na MoU? (tukumbuke hata majangili mawili yakiunda umoja nayo yatakuwa ni kundi)
sawa kaka, iwe iwavyo, nachelea tunaanzia kufikiria kuanzia katikati badala ya kuanzia mwanzo. tutafute backgroud information ya MoU kwanza. Kama ilivyo kwenye maandishi ya Dr Slaa, haidhuru kama ni ufafanuzi au ni tamko, cha msingi ni elimu, au hata ukipenda ilmu aliyotoa. tujiulize kwanza, kwa mfano:
- MoU ni nini?
- Nini kilisababisha iwepo?
- Je hizo sababu sababishi zina ukhalali, kisheria, kimantiki na morally?
- Je uwepo wa MoU umekuwa kwa faida ya nani? yaan MoU hiyo imekuwa ikihudumia kina nan? ikiwezekana hapa tupewe data kwa majina na kila jina gharama ilizofaida kama matokeo ya uwepo wa MoU.
- Je kama MoU imeondokea kuwa na faida kwa watanzania, je kumekuwepo/kupo uwezekano wa makundi mengine nayo kuwa na kitu kama hicho? kama ni ndiyo hayo makundi mengine yaliwahi kuomba kuwa na kitu kama hicho? kama ni ndiyo walikubaliwa? kama ni hapana. je kwa nini walikataliwa? Je sababu za kukataliwa zina ukhalili kisheria, morally au vinginevyo? Kama hazina ukhalali ina maana kuna mtu alikosea, kama ndivyo jee kosa linaweza kurekebishwa sasa kwa makundi mengine nayo kuwa na MoU? Je ni sifa gani zitakiwazo kundi liwe nazo ili kwazo listahiki kuwa na MoU? (tukumbuke hata majangili mawili yakiunda umoja nayo yatakuwa ni kundi)
Mkuu, leta hapa thread yangu au post yoyote inayoonyesha nashabikia ukanda kwa ajili ya kuigawa nchi yetu vipande vipande. Sijakosa hoja za kukabiliana na CDM au CCM hadi nikatumia ngao ya ukanda.
Kuweni makini, mishahara, oc na deve funds serikali inatoa kwa kanisa kila mwezi. Bugando, kcmc, peramio, ifakara, bwagala nk. Lakini bado tunalipia huduma. Mbona haitoi kwa bakwata? Ushaidi ni mimi na vitabu vya bajeti
Natumia ubongo kufikiria situmii dini kufikiria. Taifa letu mbele. Nitapinga udini kwa nguvu zote na nitawapinga wote wanatumia dini kufikiri badala ya ubongo wao.
Ndiyo CCM wana maslahi na Kanisa wanamuenzi muanzilishi wa CCM Nyerere. Lete swali lingine.
Hebu waislamu tujitathmini kwanza badala ya kuhamishia makosa kwa wengine.You are missing the point. Huwezi kutuambia kwamba wakristo wana elimu sana kwa vile waliumbwa hivyo! Ni set up tu ambayo serikali kwa kushirikiana na makanisa waliamua kufanya makusudi kwa misingi ya kibaguzi. Hili lazima lijadiliwe katika national level kama ambavyo tuanjadili ufisadi mwingine.
Ritz hueleweki na unatuchanganya. Mara CDM ina maslahi na kanisa. Mara tena CCM ina maslahi na kanisa. Upo umuhimu wa kuwa na mtiririko kwenye dhana hii.
Mkuu inawezekana unalolisema ni kweli, labda walitaka mashirika ya kikatoliki yawasidie maana huko kwenye mashirika yao wanasaidiana namna ya kujilipua au kuutokomeza ukristu. Wanasahua kuwa kumwondoa anayeshikilia njia kuu za uchumi au huduma za kijamii ni ngumu. Kwa mfano leo hii ukiwaambia wakristu wafunge hospitali zao zote nchini, patachimbika. Hadi hao wanaouchukia ukristu wataathirika. Kwenye mashule na vyuo hayohayo