Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Si JK alituambia kuwa serikali ilitoa mabilioni kwa Kanisa, mbona hamkukanusha wakati ule? au tuna kosa gani kulihoji hili?!

Hiyo serikali ya Ulaya inayotoa hela za kodi za wananchi wake (ambao wamelikataa Kanisa na kulitenganisha na Serikali)na kuyapa Makanisa ya Tanzania inabidi utaratibu ufanyike ili tupate kauli yao nao wanasemaje kihusu hili.

*Wabunge wa chama tawala na upinzani hawaibui hoja za ufisadi mkubwa namna hii bungeni kutokana na kufungamana kwao na sera za vyama vyao hivyo huu ni wakati muafaka kuruhusu wagombea binafsi.
 
Swala la malalamiko ya waislamu limeshafikishwa serikali kitambo tu ila serikali inajifanya haisikii kwa kuwaogopa maaskofu.
Wasi wasi wangu ni kwamba kimya cha serikali ni hatari kwa taifa letu siku za usoni.
 
Ni full magumashi

inasikitisha hadi waislam ambao wamesoma wanaishia kulalamika badala ya kuwashauri wakina ponda kuanzisha hospitali na shule nyingi ili kuwepo MOU kati ya serikali na waislam!!
 
Wewe hujui lolote bora ukae kimya.

Lugha ya mtu asiye na hoja.

Hujui lo lote kuhusu MOU. Mbona unakimbia hoja. Wewe una chuki na makanisa. Haikusaidii, na makanisa yataendelea kustawi wakati wewe ukipiga kelele maji ya bahari yapungue.
 
Wakati wa sherehe ZA idi KWENYE msikiti wa Ghadafi Mhe Rais alisema Kama waislamu tatizo ni MOU, Nanyi leteni ya kwenu badala ya kukaa KULALAMIKA , au bado mko KWENYE mchakato wa kuandika?

Huwezi kuondoa dhulma kwa kuanzisha dhulma nyingine. MoU ni ufisadi, kabla ya kutengeneza ufisadi mwingine lazima tujue ni kwa kiasi gani serikali imechota fedha za walipa kodi wenye dini na wasio na dini kuyapa makanisa.
 
Uganda ni member wa OIC. niambie kuna sheria za kiislamu zinazotekelezwa Uganda? Ni effect ipi ya kiislamu umeiona kule ambako waislamu si zaid ya 8%?

Chuki inaweza kukufanya usione ukweli.
 
Sina hakika kama unajua unachokisema katika hiyo financial assistance:

Nimepigia mstari hilo neno, financial assistance haiko kwenye misamaha ya kodi ila ni kwenye bilateral negotiations
2) ‘The government shall endeavour to include financial assistance for church run social services in its bilateral negotiations particularly with the Federal Government of Germany. Consideration shall be made during its bilateral negotiations with other donors’. Article xiii.

Serikali ifanye juhudi kuingiza kipengele cha msaada wa kifedha kwenye mapatano yake ya kimataifa, hususan kwa Ujerumani. Pia serikali itilie maanani swala hilo kwa waadhili wengine.
 
inasikitisha hadi waislam ambao wamesoma wanaishia kulalamika badala ya kuwashauri wakina ponda kuanzisha hospitali na shule nyingi ili kuwepo MOU kati ya serikali na waislam!!

Mkuu umesema vema. Tatizo la baadhi ya wenzetu wanafurahi zaidi kulalamika na kulaumu badala ya kutafuta ufumbuzi.
 
Kwa namna yeyote mkataba huu ni mbaya na haufai kwenye nchi inayajenga demokrasia.unajenenga matabaka ya watu.anayataka usawa hawezi kuunga mkono.
 
inasikitisha hadi waislam ambao wamesoma wanaishia kulalamika badala ya kuwashauri wakina ponda kuanzisha hospitali na shule nyingi ili kuwepo MOU kati ya serikali na waislam!!
Wakristo wana MoU, Waislamu nasi tupate MoU, Wapagani nao watadai MoU, Baniani nao watataka wapatiwe MoU, Rastafarian nao watadai MoU....sasa kazi ya serikali itakuwa ni nini ikiwa huduma muhimu kama hizi itaziachia taasisi za kidini? si bora tugawaneni nchi tu kwa misingi ya kidini!

MoU ifutwe tu.
 
inasikitisha hadi waislam ambao wamesoma wanaishia kulalamika badala ya kuwashauri wakina ponda kuanzisha hospitali na shule nyingi ili kuwepo MOU kati ya serikali na waislam!!
We chakubimbi unaona waislamu tu vipi walokole,mashahidi wa yehova,masalia ya airport na kanisa la mtakatifu Mtikila?
 
Kuweni makini, mishahara, oc na deve funds serikali inatoa kwa kanisa kila mwezi. Bugando, kcmc, peramio, ifakara, bwagala nk. Lakini bado tunalipia huduma. Mbona haitoi kwa bakwata? Ushaidi ni mimi na vitabu vya bajeti
kwani nan anatibiwa bure mkuu
 
Huwezi kuondoa dhulma kwa kuanzisha dhulma nyingine. MoU ni ufisadi, kabla ya kutengeneza ufisadi mwingine lazima tujue ni kwa kiasi gani serikali imechota fedha za walipa kodi wenye dini na wasio na dini kuyapa makanisa.

Umeisoma MOU na kuielwa? Taja kifungu ambacho kinasema serikali itakuwa inatoa fedha kuendesha makanisa. wa taarifa yako 40% ya huduma za afya zinatolewa na makanisa. Mfano wilaya zote za mkoa wa Kagera, ukiacha Bukoba Mjinj, ni za "Makanisa".
Tuambie dehebu lako limejenga wapi hospitali. Makanisa yataendela kustawi
 
Dr umetoa historia lakin hata Mwl Nyerere alikuwa na sababu zake za msingi kabisa kuanzisha AZIMIO LA ARUSHA. lakin kwa sasa hakuna tena nafasi ya kuendelea kuwa na Azimio hilo.

Kwa upande wangu Dr nakushauri kwa wakti huo kulikuwa na kila sababu kama ulivyobainisha. Sasa nikuulize je Sababu hizo mpaka leo zipo? Je kwanini Serikali yenu isijenge za Kwake yenyewe kuepukana na hizo za Kukodi kwa kanisa? Je unajua Kanisa wanachukua kiasi gani kutoka Serikalini kila mwaka?
 
mnavyodai mahakama ya kadhi huoni kama dini zote ulizotaja zitataka mahakama zao?serikali(ya ccm)haiwezi kufuta MOU na wakristo sababu hawana uwezo wakutoa huduma zile bila msaada,.mnang'ang'ania mou ifutwe sababu hamna brain ya kuanzisha hospitali na shule?
 
We chakubimbi unaona waislamu tu vipi walokole,mashahidi wa yehova,masalia ya airport na kanisa la mtakatifu Mtikila?

hao wote wana-fall kwenye ukristo,mkuu you talking like you have seen a ghost
 
Wewe unanirudisha nyuma sana, kuwa composed maana yake nini? Kuna kitu gani ambacho hakieleweki?

Waislamu kama wanadamu wa kawaida wana mapungufu yao na ni jukumu lako wewe na mimi kuondoa mapungufu hayo kuanzia ngazi ya familia zetu. Issue ya msingi ni MoU ambayo vipengele vyake vinaonesha dhulma ya wazi kwa raia wasio kuwa na dini na wenye dini nyingine zaidi ya ukristo.

Serikali ni mlezi wa raia wote na penye kosa ni lazima lisemwe. Kulalamika si sifa ya waislamu lakini kuona dhulma na kuinyamazia si katika sifa za uslamu pia.
 
Kuweni makini, mishahara, oc na deve funds serikali inatoa kwa kanisa kila mwezi. Bugando, kcmc, peramio, ifakara, bwagala nk. Lakini bado tunalipia huduma. Mbona haitoi kwa bakwata? Ushaidi ni mimi na vitabu vya bajeti

Nakushauri ungekua unatibiwa kwenye hospitali za serekali kwani nako si kuna tiba na madaktari wa kitu unachoamini na usikimbilie kwenye hizi na pia yakupasa ujue hata hizo za serekali pia huwa zina pewa madawa na vifaa tiba lakini mnapoenda kutibiwa inakuaje? Na usomi wako wa vitabu umejaa enferiority complex na ndio maana ukaona ni hospitali za mission tu ndizo zinapata hiyo misaada lakini hizi za serekali na nyinginezo hukuona mwisho ukisoma vizuri jiulize kwnni hospitali, vituo vya afya na zahanati serekali zinapata vifaa tiba na madawa kisha mkakimbilia kwenye hospitali hizo mnazoona zinapendelewa?
 
najua umemuuliza dr.slaa lakini nitajibu kwa niaba yake..wakristo hawailazimishi serikali kuendelea na MOU,wanachotaka wapewe shule zao na hospitali zao,serikali haitaki sababu haina uwezo wa kujenga huduma hizo,MOU inawasaidia zaidi serikali kuliko wakristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…